Tunataka kiongozi wa aina gani Tanzania?

MBATATA

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
542
209
Kiu kweli kweli! Hasira sana! Kwa miaka mingi iliyopita wengi wetu tumekuwa tunaonyesha kiu kubwa ya kuona mabadiliko ya msingi nchini. Hasa baada ya kuondoka Mwalimu Nyerere madarakani, tulipitia vipindi ambavyo mamlaka zilizofuatia zikaonekana kutoweza kuhimili usmamiaji wa misingi muhimu kama vile maadili, taratibu, kanuni na sheria, na kuwaondolea watu ile kiu ya kuona mambo sasa yanaenda sawa.

Zimekuwepo dalili dhahiri za unyonge, ulegevu, udahifu ambao ukafikia hatua ya kuwa maudhi, kero na hata kufikia watu kujenga chuki za ajabu dhidi ya mamlaka zilizokuwepo! Lawama zilikuwa nyingi na watu walifika mahali wakaonekana kukata tamaa kuwa kuna tumaini ipo siku mambo yatabadilika.

Ukweli usiopingika ni kwamba watu wamekuwa wanajifanyia mambo bila woga wowote, na hata mambo ambayo yamekuwa yakionekana kabisa kuwa ni yenye ufidhuli uliopitiliza kama ufsadi na matumizi ya fujo ya rasilmali za taifa yakawa yanfanyika mchana kweupe.

Ilikuwa kawaida kusikia watu wakisema "Ah! Hii nchi bwana, yaani inavyoendeshwa, utadhani hakuna uongozi!" Mifano mizuri ni kama pale Bunge la 9 likiongozwa na Mhe Sitta na Mhe Ana Makinda, hoja zilizokuwa zikijengwa na kuonekana za kweli na za nguvu, na zenye kuonyesha kwa jinsi gani Watanzania wamechoshwa na uozo uliokuwepo na uvumilivu haupo tena kiasi cha kuilazimisha mamlaka kubadili uongozi (Baraza la Mawaziri) hadi mara 4).
Watz wengi walianza kusikika wakisema "hii nchi iinahitaji dikteta wa kunyoosha mambo" maana bila hivyo uozo huu utaendelea kuwepo, na kwa tofauti za kiustawi katika jamii za namna hii, tena zinazosababishwa kijinga jinga tu, tutafika mahala tutakulana wenyewe kwa wenyewe. Asiye nacho atamtafuna aliye nacho ili naye apate walau kidogo na aliye nacho atamtafuna asiye nacho ili kulinda maslahi yake matamu.

Huyu bwana aliyekuja awamu hii binafsi sijaelewa nimweke kundi lipi, labda ni mapema bado kumfanyia tathmini. Yapo mambo ambayo anayafanya yanayoashiria ana nia njema ya kurekebisha mambo, lakini yapo vile vile mengine yanayoashiria kukosekana kwa umakini, au niseme, kukosekana kiwango stahili cha hekima? Lakini tayari kuna lawama, kwamba mtu huyu nii dikteta na anatuburuza watanzania visivyo sahihi na kujenga hofu.

Sasa, iwapo weeengi tulifika mahala tukasema ni bora tuwe na dikteta ili mambo yaweze kunyooka Tanzania maana yake nini? Ni namana tunavyoelewa hii dhana ya Dikteta? Na kwa maana hii, bado hatujampata Dikteta tunayemtaka?
 
Back
Top Bottom