Tunataka katiba mpya

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
Rais wa nchi ndiye anaechagua mwenyekiti wa Tume ya taifa ya uchaguzi.
- Ndani ya ccm Rais wa nchi ndiye mwenyekiti wa chama.

Rais anapomaliza muhula wa kwanza wa uongozi wake anasifa ya kugombea muhula wa pili kwa mujibu katiba.
Hii inamaana kwamba yule unaeenda kupambana nae katika uchaguzi ndiye anaekuchagulia mtu wa kusimamia uchaguzi!

Katika Mpira ulishawahi kuona mechi ya simba na yanga.
Simba ndio awe anachagua refa wa kuchezesha mechi na Yanga halafu eti yanga wanakuja kwa mbwembwe kwamba watashinda!?.
Hiyo mechi ingevunjika kabla ya kuchezwa.
Katika mpira hilo haliwezekani lakini katika siasa tumeshuudia.

Mfumo wetu wa Katiba haupo sawa kuendana na siasa zetu za vyama vingi.
Uchaguzi mkuu tunakuwa na kura tatu.
Kura ya Diwani
Kura ya Mbunge
Kura ya Rais
Katika kura hizi tatu (3) kura mbili (2) ya diwani na mbunge mgombea wa chama (A) anaweza kwenda mahakamani kupinga matokeo ya mgombea wa chama (B) lakini katika kura ya urais matokeo yakishatangazwa huwezi kwenda kuhoji popote pale!!
Je! kuna nini hapa katikati kinachofanya hii kura ya urais isihojiwe? Mnaogopa nini!?.

Katika mazingira haya lazima tuungane kudai Katiba mpya.
Mfano leo Magufuli anabomoa reli ya kati ili kujenga reli mpya itakayokuwa na uwezo wa kuendana na treni mpya za umeme, maana reli iliyopo haiwezi kuendana na aina ya treni za kisasa zinazotumia umeme.
Kwa hiyo kama ccm ilikuwa tayari kuruhusu mfumo wa vyama vingi 1992 ilitakiwa kufumua Katiba ya 1977 ambayo ilikuwa ya chama kimoja na kutengeneza katiba mpya itakatokuwa na uwezo wa kuendana na mfumo wa vyama vingi.
Kama vile wanavyotoa reli ya zamani na kujenga mpya.
Mabadiliko makubwa kama haya huwezi kuyaendesha kiufanisi bila kuwa na misingi mizuri.
Kinyume chake Katiba imewekwa viraka. Upinzani unanyonywa sheria zilizopo haziwapi nafasi ya kukua.
Naungana na Chadema kudai Katiba mpya itakayoruhusu kuhojiwa kwa matokeo ya urais, katiba itakayo mwondolea rais haki ya kuchagua mwenyekiti wa tume ya uchaguzi.
Kupata Tume huru isiyoingiliwa na chombo chochote.
USHAURI
Vyama vya upinzani vimeshashiriki uchaguzi mkuu kwa vipindi vitano sasa kwa uvumilivu mkubwa, nadhani sasa ni wakati wa kudai Katiba mpya tu. Bila Katiba mpya tutakuwa wasindikizaji kila uchaguzi tutabakia kupata madiwani na wabunge tu, nafasi ya urais tutaisikia tu.

[HASHTAG]#AmkaMtanzania[/HASHTAG]
 
Hatuna fedha za huo Ujinga!
 
Vyama vya upinzani vyenyewe vimejaa wapigaji tu.

Katiba mpya tutaipa kupitia nia halisi ya watanzania sio hawa wanasiasa wachumia tumbo.
 
Back
Top Bottom