Tunataka elimu ya namna hii kwa watanzania

SENGANITU

Member
Sep 19, 2012
50
15
Salamu kwa wana JF wote!!!
Mimi napendekeza aina ya elimu itakayotufaa watanzania kwa wakati huu na kwa miaka mingi ya baadae.
1.Iwe ni ya lazima kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne
2.Iwe ni ya kumwezesha mtanzania kujitegemea,kujiajiri na kuwa waajiri (sio kutegemea kuajiriwa tu)
3.Masomo ya mchepuo yawepo pia ya masomo mawili mfano pc,hl...
4.Walimu wawe ni wale waliofaulu na kuthibitishwa kwa ujuzi wao,shule za msingi walimu wawe na diploma ya elimu.
5.Taasisi zote zinazotoa mafunzo ya kiweledi zihusishe kozi zinazohusu watu wenye mahitaji maalum kama vile wasioona,wasiosikia,n.k. na kwamba hizo taasisi zihusishe na watu wenye mahitaji maalum kama wawezeshaji au wasomaji
6.Kwa kuwa elimu ndiyo ngao kubwa ya kumletea mtu mwanga wa kujitegemea na kulisaidia taifa hili,hivyo kipaumbele cha bajeti namba moja miaka yote kiwe elimu
7.Umri wa kuanza darasa la kwanza uwe miaka mitano(5) kutokana na uwezo wa ufahamu wa binadamu kuongezeka,maumbile ya binadamu kukua haraka,na life span(kwa tz) kupungua
8.Somo la mahusiano ya kimataifa lifundishwe kuanzia kidato cha kwanza kwa kuwa sasa dunia inakuja pamoja kwa mitazamo na maendeleo ya kimataifa.
9.Mfumo mzima wa elimu utawaliwe na watu wenye taaluma inayohusu mambo ya kielimu(wanasiasa wasiingilie mambo ya maamuzi ya kielimu)
10.Ada ifutwe kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha sita ili watanzania wengi waweze kupata elimu bila kikwazo.
Najua wana jf mna mengi ya kuzungumza kwa hili,karibuni kuchangia mada yetu,nawasilisha kwenu.
 
Hapo umenena kabisa ila bado swali la mitihani inayoitwa ya taifa

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Elimu ya Kdato cha Kwanza mpaka cha Nne ni lazima! Ulazima huo umeleta 50% feli. Ikiwa maeneo ya mijini watoto wenye miaka 6 na waliolelewa katika mazingira mazuri ndio wameweza kuingia darasa la kwanza, je waishio kijijini itakuwaje?
Ngoja niongeze kidogo:
-mazingira ya kufundishia na kufundisha yaboreshwe ili kuleta hamasa ya kufanya kazi.
 
ndio hivyo vinatakiwa,lakini bila serikali kuona umuhimu wa bajeti ya elimu hatuwezi kusonga mbele nauzalendo unatakiwa
 
hongera kwa maono mazuri. wapeleke wahusika pale wizara ya elimu
 
Ninashukuru kwa michango yenu mizuri ya mawazo. Ninachokitafuta hasa ni mawazo yenu supportive documents ili mwisho wa siku niunganishe mawazo yenu kisha tuwapelekee wahusika wa mambo ya elimu.Kweli kabisa tunahitaji elimu bora isiyo na maigizo ili tuweze songa mbele kimaendeleo ya binafsi na kitaifa kwa ujumla. Endelea kutoa hoja,mawazo yako ni muhimu sana kwa mstakabari wa nchi yetu!!! This is the home of great thinkers,we need your valued logics.
 
Back
Top Bottom