Tunapopanda uozo kwa shangwe na kuvuna uvundo kwa kilio

fellali

Member
Aug 14, 2013
17
2


Tunapopnda uozo kwa shangwe na kuvuna Uvundo kwa kilio

Miaka michache iliyopita tulishuhudia chama cha upatu (DEC) ambapo wanachama waliweza kupanda mbegu chache na kuvuna mbegu nyingi zaidi kwa imani. Punde wanachama wakaanza kuangua vilio baada kutaifishwa fedha zao ambazo hadi sasa ni kitendawili juu ya urejeshwaji mbali ya kuwa serikali iliingilia kati lakini bado baadhi ya mbegu za wanachama hazikuonekana zilipokuwa.
Yuachane na DEC maana siyo mada yetu ya leo ila tu ila tu nimependa kuanza na mfano huo ili kujenga kwa umakini zaidi hoja yangu. Ni kwa muda mrefu sasa watanzania wamekuwa wanashuhudia vioja kwenye tasnia ya elimu, hasa pale tunaposhuhudia watoto wa watanzania wakimaliza elimu ya msingi na sekondari huku hawajui kusoma wa kuandika.
Kama ilivyokwaida lawama zote huiendea serikali kwamba haijali sekta ya elimu. Huku walimu wakija juu kuwa hawapewi maslahi ya kutosha na hivyo kupoteza molali wa utendaji kazi au kutofundisha kabisa.
Hivi kweli kutopewa maslahi stahiki yanasababisha mwanafunzi asijue kusoma wala kuandika tangu darasa la kwanza hadi la saba? je, mitihani yake anashinda vipi? Anaruhusiwa vipi kuendelea na darasa lingine wakati hajui chochote kwenye darasa la nyuma?
Kimsingi haiingii akilini ila itakuwa ndiyo matunda ya kumruhusu aliyeshindwa masomo ya kidato cha nne au sita kusomea ualimu. Tujaribu kufikiria mtu kashindwa amsomo yake kwa maana ya kwamba anakosa vigezo vya kuendelea na masomo ya juu labda arudie tena/ akaririshwe darasa na kushinda ndipo aruhusiwe kuendela. Lakini hapa kwetu ni kinyume, tunamruhusu mtu huyo huyo aliyeshindwa kwenye masomo yake asomee ualimu ili afundishe wenzake alichoshindwa, hivi kweli inawezekana?
Jamani mtu akishindwa jambo inamaana halijui, sasa inawezekanaje mtu huyo huyo apewe kibali cha kufundisha kutoka kwenye ombwe alilo nalo kichwani mwake? Hivi mtu huy atafundisha au atapotosha? atazalisha wasomi au atazalisha wajinga?
Mwanzoni nilianza na mfano wa DEC kwamba wanchama walipanda mbegu kwa shangwe, zilipotapeliwa wakaanza kuomboleza; sasa tujiulize hawakujua kwamba kile ni chama cha kitapeli? Hivi ni nani awezaye kukupa mara tatu ya fedha unazompa kwa hiari ndani ya muda wa majuma matatu (3) huku na yeye anatafuta fedha hizohizo?
Mfano huu hautofautuiani na mfumo wa elimu yetu watanzania. Mtu kashindwa kidato cha nne au cha sita laikini sisi tunaona huyo huyo anafaa kufundisha baada ya kushindwa kundelea na elimu ya juu. Tena anaruhusiwa kusomea ualimu kwa shangwe na vifijo pasipo kuangalia upande wa pili wake. Mtu huyo huyo anapoazna kuzalisha ombwe la wasomi tunalaumu tena kwa jadhba, inamaana hatukulijua hilo kuwa ukipandacho ndicho ukivunacho? Tumesahau kuwa matunda ya uozo ni uvundo?
Ili tuepukane na hili ombwe la wasomi feki, ni vema kurudi mezani na kubadili upya mfumo wa elimu wa nchi yetu kwa hali hii tutaendelea kupanda uozo kwa shangwe na kuvuna uuvundo kwa kilio na kusaga meno. Ni wakati sasa tujipange kuinusuru nchi yetu ili kurejesha heshima yake ilikwisha kupotea.
Na Felix Lugeiyamu.
 
Back
Top Bottom