Tunapomkumbuka Hayati Mwl Nyerere, tunajua hofu na uoga?

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
Na Elius Ndabila
0768239284

Maendeleo ya taifa lolote yakijawa na uoga na nguvu dhidi ya hofu ni ngumu sana kuyafikia. Tukiwa tunaendelea kuiangazia Tanzania baada ya miaka bila Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere tunaweza kumuona yeye kama shujaa wa Taifa hili. Ni mtu ambaye hawakuwa kutikiswa na nguvu yoyote iwe ya nje au ndani, alisimamia kile alichoamini ni sahihi. Misimamo yake iliisaidia sana Tanzania kukua kiuchumi na achano la dollar na shilingi halikuwa kubwa kwani taifa lilikuwa na viwanda vingi vilivyoruhusu ushindano kwenye masoko ya kimataifa.

Ni vigumu sana kumfananisha Mh Mafufuli Rais wa JMT na Hayati nyerere kwani pamoja na falsafa zao kwa kiasi kuendana, lakini dunia imebadirika. Jambo kubwa ambalo Mh Rais analifanya sasa kwanza ni kuondoa watanzania mentality ya hofu/uoga ambao hupelekea mkwamo katika maendele duniani kote.

Labda tujiulize hofu ni nini tunapozungumzia maendeleo ya mtu mmoja mmoja ambayo ndiyo nguzo ya uchumi wa taifa? Hofu ni hali ya kuwa na wasiwasi wa kitu fulani kibaya kutokea lakini kitu hicho huwa bado hakija tokea.Kama binadamu kila mmoja hupatwa na woga kwa nyakati tofauti. Woga huu hugusa maeneo mbalimbali katika maisha ya kila siku yaweza kuwa kazini, katika mahusiano, katika matembezi,kwenye ndoa nk.

Hakuna mtu anayependa kushindwa maishani kila mtu anapenda kuwa na mafanikio makubwa maishani. Ninakumbuka zamani tukiwa watoto kijijini Babu zetu walitutia moyo katika kutokataa tama. RIP Ngigana Shibanda ambaye akiwa mwenyekiti wa kijiji miaka ya 70 walikuwa wakitoka na tofali Lubanda hadi Ibaba umbali wa Km 54 kwa ajili ya kujenga shule ya msingi Ibaba. Wao hawakuwa na hofu, kwani walitazama hatua nyingi mbele, yaani walifikiria kesho na hawakufikiria leo tu. Leo hii tunasahau kuwa mafankio huja kwa kuyahahagaikia na siyo kitu cha mara moja.

Wakati ninaendelea kuandaa makala hii nikakumbuka mwanazuoni mumoja aliwahikuandika kwa kusema yeyote ambaye hatakikufanya makosa hawezi kufanikiwa. Yaani ni lazima ushindwe mara kadhaa ndipo uweze kufanikiwa na hii ndiyo principle ya success. Ni kawaida kwa motto anapoanza kutembea huanguka na huumia sana, lakinipamoja na kuumia huwa hawakati tama kuendelea kujifunza kutembea. Hivyo tunaweza kujifunza kwa watoto kuto kata tama. Mtoto anapojifunza kutembea pamoja na kuanguka hakati tama kwa kuwa lengo lake ni kujifunza kutembea na mwishowe huwa anafanikiwa kutembea. Don’t give up, try and try, fear can rise you down and destract your dream. Kwa maana hii motto angetawaliwa na roho ya hofu na akaacha kutembea kwa sababu ya maumivu anayopata anapotembea, basi asingejifunza kutembea. Hivyo hivyo na kwetu ukiogopa kufanya jambo kwa hofu yako huwezi kufanikiwa. We learn through mistake.

Woga ni kitu ambacho watu wote wanacho, hakuna mtu anayeishi duniani na ikawa hakuna kitu asichokiogopa na kama yupo mtu wa aina hiyo basi atakuwa ana matatizo ya akili. Lakini kwa wenye akili, kila binadamu duniani lazima atakuwa ana kitu kinachomfanya awe na woga fulani. Wengi wetu huwa tunafikiria kuwa woga ni kitu kibaya, lakini ukweli ni kwamba woga si kitu kibaya, kwa kweli woga ni kitu kizuri na ni ishara ya kuwa unatakiwa kuchukua tahadhari au kujiandaa na hilo jambo linalokutia uwoga. Kwa mfano kama huna kazi na umeishiwa na pesa na unatakiwa ulipie pesa ya chumba unachoishi uwoga unakuja. Hivyo unatakiwa ujiandae kwa kwenda nje kupambana na kutengeneza pesa ambayo itakuwezesha kulipa kodi ya chumba unachoishi. Huo ndio uwoga.

Lakini cha ajabu na tofauti ya watu wanaofanikiwa na watu wanaohangaika katika kupata mafanikio ni kwamba watu wenye mafanikio huwa wanajua kwamba kitu ambacho naogopa kufanya ndio natakiwa kukifanya ili kupata mafanikio. Na wale ambao hawafanikiwi huwa wanakimbia ule woga wao, yaani hawapo tayari kufanya kile wanachokiogopa. Kwa kiingereza uwoga unajulikana kama FEAR[false evidence appear real].

Tukimwacha Baba wa taifa kama nilivyoeleza awali, lakini pia mfano mkubwa wa JPM na Nyerere ni kuto kata tama. Nikupambana hadi dakika ya mwisho. Miradi mikubwa inayotekelwazwa nchi nzima ni mifano tosha kuwa JPM angesikiliza kila mtu, basi watumishi hewa wasingeondoka, barabara zinazojengwa wilaya zote nchini zisingejengwa, vituo vya afya na hospital zinazojengwa nchi nzima zisejengwa.

Si hivyo tu, bali hata meli, ndege na viwanja vya ndege tusingevipata. Inawezekana ukadhani hayo ni machache, lakini kumbuka kuna elimu bure bilioni 23+ kila mwezi zinaenda mashuleni, mikopo ya wanafunzi vyuo vikuu imeongezeka kwa asilia kubwa, mahakama za kanda zinajengwa na kuboreshwa, nidhamu kazini kila mtu anamwogopa mwenzake, terminal three utadhani tupo dunia ya kwanza.

Yapo mengi ya kumzungumzia JPM anayemuenzi hayati Nyererekwa vitendo. Angejawa na hofu na uogo dhidi ya maneno ya watanzania tusingekuwa huku. Lakini haogopi na hahofii kukosea kwani anatambua makosa ndiyo yanasaidia kukufanikisha na kukujenga, lakini hofu na woga zinakurudisha nyuma.
 
Jiwe hana hofu mpaka kabadilisha mkurugenzi wa tume ya uchaguzi ili kutenda haki
 
Kwani nafasi ya Ukurugenzi ni ya kudumu?
kwa hiyo kwa upeo wako wa kuelewa mambo unaona ni haki kabisa kwa mwenyekiti wa chama cha kisiasa kuteua chairman wa NEC? NA tutegemee NEC itaamua kwa usawa kwenye masuala ya uchaguzi,tatizo la working class yetu tumelose touch kabisa na yanayotokea on the ground,wewe unaona ni haki kwa CEO wa club kuteua mwamuzi wa mechi zake!!!!
 
Mnakosea Sana Kumlinganisha Baba Wa Taifa Na Vitu Vya Kipumbavu"

Baba Wa Taifa Miaka 24 Aliyokaa Ikulu Hajawai Hata Kutuhumiwa Kijiusisha Na Wizi Au Ufisadi Au Matumizi Mabaya Ya Madaraka.

Hakuwahi Kuiba Ata Sent Ya Nchi Hii Sasa Uyu Unayemlinganisha Naye Uhadirifu Wake Ni Ziro Achilia Mambo Yake Ya Udicteta.
 
Kumsifia mtu huyu nikunichefua kwani ninavyoamini mimi alitufelisha na atakae mfata atafeli balaa kielimu na kimaendeleo ukweli mchungu huo
 
Mnakosea Sana Kumlinganisha Baba Wa Taifa Na Vitu Vya Kipumbavu"

Baba Wa Taifa Miaka 24 Aliyokaa Ikulu Hajawai Hata Kutuhumiwa Kijiusisha Na Wizi Au Ufisadi Au Matumizi Mabaya Ya Madaraka.

Hakuwahi Kuiba Ata Sent Ya Nchi Hii Sasa Uyu Unayemlinganisha Naye Uhadirifu Wake Ni Ziro Achilia Mambo Yake Ya Udicteta.
Hujui sio kilakilicho andikwa kwenye vitabu nikweli vingine vimeandikwa ili nawao wapate kujiburudisha au kuburudika tumia uwezo wako usikubali kulainishiwa kila kitu
 
Ka
kwa hiyo kwa upeo wako wa kuelewa mambo unaona ni haki kabisa kwa mwenyekiti wa chama cha kisiasa kuteua chairman wa NEC? NA tutegemee NEC itaamua kwa usawa kwenye masuala ya uchaguzi,tatizo la working class yetu tumelose touch kabisa na yanayotokea on the ground,wewe unaona ni haki kwa CEO wa club kuteua mwamuzi wa mechi zake!!!!
Kali hiyo
 
Wazembe Ndio watavaa viraka
Ardhi ipo mvua inanyesha Kazi kwako

Kwenda kulima kilimo cha mvua ni kufunga ndoa na umasikini. Ni bora niwe barmaid hapa mjini kuliko kwenda kufanya huo ujinga. Kama huamini kachukue mabarmaid kumi hapa mjini, wafananishe na wakulima kumi, kisha ulete mrejesho nani mwenye afadhali kimaisha.
 
Wanachofanana Mwalimu Nyerere na JPM ni ule uthubutu, kuamini na kusimamia katika kile unachokiamiani.

Nyerere ni mwanadiplomasia wa kuzaliwa, mtu mwenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja ziwe za kitaifa au kimataifa.

JPM ni mfuatiliaji na mtendaji wa kile kinachokubaliwa kufanyika katika vikao vya pamoja, sio mwanadiplomasia na hatakuja kuwa.
 
Inategemea unaongelea wakulima wa maeneo gani. Mkuu tindo punguza dharau kwa sababu unaishi jijini.
 
Wanachofanana Mwalimu Nyerere na JPM ni ule uthubutu, kuamini na kusimamia katika kile unachokiamiani.

Nyerere ni mwanadiplomasia wa kuzaliwa, mtu mwenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja ziwe za kitaifa au kimataifa.

JPM ni mfuatiliaji na mtendaji wa kile kinachokubaliwa kufanyika katika vikao vya pamoja, sio mwanadiplomasia na hatakuja kuwa.

Lkn kwa Makonda amegonga mwamba.
 
Back
Top Bottom