Sesten Zakazaka
JF-Expert Member
- Sep 10, 2017
- 10,729
- 19,615
Nimerudi kutoka safari ya maziko nilipomsindikiza rafiki yangu kwenye kijiji kimoja kipo wilaya ya Mahenge kinaitwa Mwaya, ni mbali kiasi kutokea Dar ambapo mnakwenda hadi Ifakara mnavuka mto Kilombero na kisha mnapanda milima kadhaa (mmoja unaitwa mlima nyoka) kabda ya kufika huko.
Huyu rafiki yangu ni wakabila la Wandamba, sasa watu wanaotokea maeneo hayo wamejipanga ambapo ikitokea maafa au msiba hata kama alieyefariki hakai Dar maadhali wanamjua basi wanajichanga na kutuma wawakilishi ambapo wao ndio wanasimamia na kugharamia msiba mwanzo mwisho.
Miaka yoote wanasema wakienda msibani wanagharamia kuanzia usafiri wa wanaokwenda na krudi kuzika, chakula kwa waombolezaji wanaofika msibani kwa siku zote za msiba hadi matanga, sanduku na mapambo mengine pamoja na gharama za kaburi(kwa wale wakristo) na anasema hua wanafanya mazishi yenye hadhi kwa watu wote wanaobahatika kuchangiwa na kikundi chao.
Kutokana na shughuli kua nyingi na mambo mengi siku za karibuni wamefanya mabadiliko ambapo wameamua wanapopata taarifa ya msiba ni bora wachange pesa na wamtume mtu hata mmoja awakilishe na kuwasilisha michango iloyopatikana kwa kamati ya Wazee iliyoteuliwa ambao wapo hukohuko kijijini, na hii ndio mara ya kwanza kutokea msiba toka waamue hivyo
Rafiki yangu ndio aliteuliwa kuwakilisha na akaniomba nimsindikize nikakubali kwenda.Tulipofika fedha kiasi cha shilingi 3,150,000.00 wakakabidhiwa ile kamati ya wazee. Yalifanyika mazishi ya kawaida kabisa. Chakula kilikuwepo kwa siku ile ya kwanza na watu wengi wa jirani wana kawaida ya kuchangia vyakula na kuja kufanya kazi mbalimbali kwenye msiba.
Mwisho wa siku zile pesa kuna watoto wawili wa marehemu wanasoma sekondari walilipiwa ada na kununuliwa baadhi ya mahitaji ya shule, yule mjane kanunuliwa bodaboda iwe inamuingizia kipato na kiasi cha laki tatu amepewa kama akiba. Njia nzima wakati wa kurudi jamaa yangu akawa anajicheka na kuwacheka wenzake kua siku zote walidhani wao wana akili kwa vile wanaishi mjini ila safari hii wazee wa kijijini wamewaingiza darasani na kuwafundisha kitu chenye manufaa sana hasa kwa wafiwa na mimi nimefurahishwa sana na busara za wazee wale