Tunapendana sana ila hakuna anaemwambia mwenzie.

Villky_J

JF-Expert Member
Mar 14, 2017
492
609
Habari wadau.
Mitihani ya Dunia haiishi.

Mimi nipo sehemu nimepanga nina takribani miezi minne tangu nihamie...yupo binti mmoja nilimkuta kwenye hiyo nyumba yani mpangaji mwenzangu ila yeye anaishi na dada yake, mwanzon sikuwa na hisia zozote juu yake..ila kadri siku zilivyo kuwa zikienda nilijikuta navutiwa zaidi na tabia yake..kwani ni mpole, mnyenyekevu, anajiheshimu na zaidi anampenda Mungu.

Ila utofauti yeye ni muislam mimi ni mkristo. Hisia za kimapenz zikaanza kunitawala juu yake. Siku moja nikaamua kuvunja ukimya, nikamwita na kumuomba tuonane faragha kwa ajili ya mazungumzo kama hutojali atakapopata muda,

Kweli alikubali na tukafanikiwa kuonana mwanaume bila shida nikaanza kutema madini majibu hayakuja kama nilivyotarajia kwani alinieleza wazi. Kwamba mapenzi ni hisia hvy hawez ruhusu hisia zake ikiwa yupo mwanaume ambae tayar ameshaanza taratibu za kufunga nae ndoa, hivyo jambo langu halitowezekana.

Mimi nikapokea majibu kama ilivyo ada, na kwa jinsi alivyokuwa akijiheshimu haikuwa rahisi kumfananisha na mabinti wengine wa kihuni hivyi niliheshimu hisia zake na nikaahidi kumuheshimu na kuishi naye kama kaka na dada.

Hivyo basi tangia hapo, nikaamua kubadilisha mind yangu nakuona kama watu wengine. Lakini kadri siku zilivyokuwa zikienda yule dada akaanza kunielewa mimi ni mwanaume wa aina gani. Mara akawa akiniona nimesimama na mwanamke mwingine hata kama tu naongea vitu vya kawaida roho ilikuwa ikimuuma sana kwan hata sura yake haiku onesha kufurahishwa na jambo hilo.

Lakini pia, amekuwa akinihoji mara nyingi pindi ninapochelewa kurudi ingawaje anaongea kama utani lkn ana onesha wazi ni mtu anae maanisha, huwa ananiambia..umetoka kwa wifi enh?

Mimi nacheka wakat mwingine na namtania kwamba wewe si ulinikataa hivyo nahangaika kutafuta na mimi nipate wa kwangu, anasemaga haya ila angalia wanawake wa sasa hivi hawana mapenz ya kweli wengi waigizaji.

Wakati mwingine nikiwa naenda bafuni kuoga nikiwa nimejifunga taulo..huwa anaonesha wazi hapendi kwani nyumba tunayokaa wanawake wasioolewa ni mwengi hivyo huwa nahic anafikiri nafanya kusudi kuwaonesha kifua changu...

Juzi ndo kaniacha hoi kabisa yupo next door mmoja hapa wa kike huwa anapenda sana movie na kwa kuwa na mimi ni mdau wa movie nikipataga muda sometimes naangalia..hivyo nikiwa nazo mpya huwa namhabarisha . .

Sasa Juzi alikuja gheto kuchukua movie..Alivyokuwa akitoka ni kasi kuwa yule binti akimuuliza..kwani ungempa flash akakuwekea zisingeingia mpk ukamsumbue kaka wa watu ametoka kazini amechoka...yule dada ilibidi acheke tu na kuondoka zake...

Sasa jamani, nishaurin tabia anazonionesha huyu binti..nikimpitia nitakuwa nina makosa kweli..eeenh mimi nasubir tu mfungo uishe maana naheshimu dini..
 
Back
Top Bottom