Tunapenda sana vya bei ndogo na wachina wametujua na kutajirika sana.

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
China wanalipenda sana soko la Afrika la bidhaa zao. Kuanzia Nigeria mpaka Msumbiji wameuza na wanaendelea kuuza kuanzia vifaa vya pikipiki mpaka simu za mikononi.

Teknolojia inavyobadilika na aina fulani ya bidhaa zinavyozidi kuondoka kwenye mzunguko wa mahitaji ndivyo wachina wanavyoinua mikono juu na kusema Mungu asante kwa soko zuri la Afrika.

Wachina wametujua vizuri sana kuwa tupo tayari kununua kitu cha bei rahisi chenye kufanana kile kinachouzwa bei ghali, hivyo wanatengeneza kopi kwa ajili ya soko la Afrika. Matokeo yake mtu ananunua vifaa feki vya umeme halafu siku moja akiwa amelala nyumbani na familia yake, nyumba nzima inaungua moto!.

Tabia hiyo ya kupenda vya bure, kupenda kupita vichochoroni imeingia mpaka kwenye siasa. Tunataka wanasiasa wa bei karibu na bure, matokeo yake wale wa bei ghali tunawaacha na tunavuna matunda ya bure ni ghali kuliko ghali yenyewe.

Wanasiasa wetu ambao wanafunga safari kwenda kujifunza mambo mbalimbali ya kisekta huko Ulaya, Marekani na kwingineko halafu tija ya safari yao inashindwa kuonekana, wana tofauti gani na bidhaa feki ambazo wakati mwingine huwa na madhara ya moja kwa moja kwenye afya zetu?.

Lipo somo kwa kila mtanzania, kwenye suala la kuchagua kiongozi wa jimbo ambaye atawawakilisha wananchi kwa miaka mitano, ni bora kuwa makini sana vinginevyo madhara ya bidhaa feki ni kuendelea kuwepo kwa umaskini wa jamii nzima.

Wachina wametujua vyema sana, jinsi tunavyopenda kukatiza vichochoroni (kupenda vya bure), na wametajirika sana barani Afrika.
Ifike mahali tusikubali kuendelea kuongozwa na wanasiasa ambao kwa asilimia nyingi sana wanafanana na bidhaa feki za kichina.
 
Nilisikitika sana kwenye taarifa ya habari star tv. Huko mbeya wahina wanaingiza samaki kutoka china. Samaki wanaokuzwa kwa madawa. Hivyo wakazi wametahadharishwa kuto wanunua kwani wanamadhara kiafya.
 
Nilisikitika sana kwenye taarifa ya habari star tv. Huko mbeya wahina wanaingiza samaki kutoka china. Samaki wanaokuzwa kwa madawa. Hivyo wakazi wametahadharishwa kuto wanunua kwani wanamadhara kiafya.
Unayo haki ya kusikitika, ni hali halisi ya maisha yetu, tumechagua ujinga na ndio unaotuumiza.
 
Hili la kuchagua viongozi wabovu wa kulaumiwa sio wananchi tu, hata tume ya uchaguzi na jeshi la polisi wanashiriki sana kwenye hili. Unakuta kiongozi anashinda kwa kusaidiwa na taasisi hizi, matokeo yake kiongozi akishachaguliwa hana wa kuwajibika kwake kwani amepata madaraka hayo kwa kutumia pesa yake. Ujinga uliotamalaki kwa wapiga kura nao ni mtaji tosha tena ujinga wenyewe umewekewa mpaka na mikakati kabisa.
 
Kichwa cha habari kinajitosheleza.
Kama kuna watu wanaponda simu za tecno kwa ubovu wake au kutokidhi viwango huku wakisahau kuhoji juu ya uimara na ubora wa barabara na majengo yanayojengwa na wachina watakuwa wanasahau jambo nyeti sana. Uchina imeshatujua si ni wapenda bei cheeeee na hapa ndo tunaenda kuangamia. Siku haya maghorofa yameanza kuporomoka ndo tutaamka narefer majengo pale udom.
Hawa jamaa watatuua siyo siri. Leo hii wanachinja punda wetu wakidai wanapeleka nyama hiyo kwao hali nyama ya punda kila kona katika mkoa huu, hotel na vyuo vingi watakua wanakula bila kujua kisa wenye hizi hotel au cafeteria wanapenda nyama bei cheee
 
Back
Top Bottom