BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,020
Video iliyoambatanishwa hapo chini ni ya Dkt. Wilson Mahera alipokuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Mjini alipokuwa akiongea na Makada na Viongozi wa CCM na kusisitiza kuwa yeye [na Wakurugenzi wenzake] hawakuokotwa tu bali walipelekwa kule [katika majukumu ya Ukurugenzi] kikazi zaidi.
Kwa sasa Dkt. Wilson Mahera ndiye Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Huyu ndiye anayetakiwa k...uongoza Utendaji ndani ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi inayotarajiwa na kutegemewa kutenda haki kwa kuendesha na kusimamia Uchaguzi ulio Huru na wa Haki. Lakini kauli zake kwenye video hii zinakinzana kabisa na dhana ya Uchaguzi Huru na wa Haki. Kauli zake zinaendana kabisa na kusawiri yanayoendelea sasa katika Majimbo na Kata mbalimbali nchini ambapo idadi kubwa ya Wagombea wa Upinzani wameenguliwa. Huyu ndiye mtu ambaye anashughulikia rufaa zote katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi!
Sasa tunapenda Dkt. Wilson Mahera na wenzake wote wasikie sauti ya Askofu ambayo inawakilisha watetezi wa haki wote nchini. Ni sauti inayowakilisha wale wote wanaoporwa haki zao kwa hila, nguvu na ubabe! Kwamba Mungu ndiye aliyetoa afya, uzima na uhai kwa Dkt. Mahera na wenzake. Mungu mwenye haki anatarajia watu wote wenye mamlaka akiwemo Dkt. Wilson Mahera watende haki. Kinyume cha hapo ni kuamsha hasira za Mungu dhidi yao. Dkt. Wilson Mahera na wenzake ndani ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wanayo nafasi ya kurekebisha makosa yaliyofanywa na Wasaidizi wao (Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi Wasaidizi) na wao wenyewe. Ujumbe huu pia uwafikie Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar. Kwamba Tume zote mbili ziache kiini macho cha kupitia rufaa za walioenguliwa, bali ziwarejeshe wote katika kinyang'anyiro.
Wasihangaike kumtafuta Askofu bali wahangaike zaidi kutafuta namna ya kurekebisha makosa yaliyofanywa kwa makusudi au kwa kutokukusudia. Njia nyepesi na salama zaidi katika kurekebisha makosa hayo ni kushauri na kushinikiza Tume zote mbili kuwarejesha Wagombea wote walioenguliwa Bara na Visiwani bila masharti ye yote na pasipo kupoteza wakati.
Askofu anatimiza wajibu wake. Ole wake Askofu asipowoanya wanaotenda maovu kwa kufinya na kupora haki za wengine katika nchi (Ezekieli 33:1-20). Sambazeni ujumbe huu hadi katika sebule za watu wote wa Tume, waliowateua, watoto wao, jirani zao, kwa viongozi wao wa kiroho (Makasani na Misikitini), kwa madereva wao, na kwa kila mtu ili ikawe ushahidi juu yao kuwa sauti ya Askofu haikunyamaza juu ya watu hawa na juu ya nchi!
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani