Tunaomba uongozi kuongoza nini?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,267
33,039
[FONT=ArialMT, sans-serif]Nilipata kuandika katika safu hii juu ya ‘kuthubutu’ kwa Rais Paul Kagame wa Rwanda. Niliandika uchambuzi wa kuthubutu kwa Kagame baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kufanya mkutano na wahariri wa vyombo vya habari ambako alizungumzia mambo mbalimbali ya utendaji wa serikali pamoja na kujibu maswali mengi kutoka kwa wahariri. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Katika mkutano huo Pinda akijibu moja kati ya maswali aliyoulizwa kuhusu tabia ya watendaji wa serikali ya kutaka kuishi maisha ya ukwasi uliopindukia kwa gharama ya kodi za wananchi itakomeshwa lini, hasa kwa kizingatia matumizi ya magari ya gharama kubwa maarufu kama mashangingi yakiwa kwenye msururu wa Toyota Land Cruiser –VX, GX, V8 VX, Mitsubishi Pajero, Nissan Patrol na mengine yanayofanana na haya. Waziri Pinda alisema serikali ilikuwa inaandaa utaratibu utakaotumika kwa manunuzi ya magari ya serikali; chini ya utaratibu huo kila mwenye hadhi ya kupewa gari la serikali itaainishwa atatumia gari gani. [/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa wastani huu ni mwaka wa nne na ushei tangu serikali ianze kufikiria uwezekano wa kuachana na anasa za matumizi ya magari hayo. Hakuna ubishi kwamba kumekuwa na matumizi mabaya ya magari haya, kwa maana kwamba yananunuliwa tu kwa sababu waliotokea kukalia ofisi za umma wanayanunua si kwa kufuata kigezo au utaratibu fulani, ila kukidhi kiu ya maisha ya ukwasi. Hakuna kuwaza yatasaidia vipi kuibadili nchi kuwa ya hali bora zaidi kiuchumi! [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa bahati mbaya, magari haya yamekuwa ndiyo rasmi ya serikali baada ya Land Rover miaka ya 80 kurudi nyuma. Siku hizi Land Rover si mali kitu tena serikalini kama ilivyokuwa wakati wa Utawala wa Mwalimu Nyerere na sehemu awali ya utawala wa Mzee Mwinyi. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wapo watu wasioelewa kwamba matumizi ya magari haya pamoja na maamuzi mengine ya ovyo kuhusu rasilimali za umma ndiyo chanzo kikubwa cha kundi kubwa katika jamii yetu kuishi katika umasikini mkubwa wa kutupwa. Nilipata kusema katika safu hii kwa mfano ofisa wa serikali anayekaa Oysterbay jijini Dar es Salaam anapewa lita 200 za dizeli kwa wiki kwa ajili ya kwenda ofisini. Ofisa huyu kwa siku hatembei na gari hilo zaidi ya km 10 kwenda ofisini na kurudi nyumbani. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hawa wako wengi wameenea nchini kote. Nilipata pia kukokotoa kiasi cha fedha kinachochomwa kwenye matumizi ya magari haya, kama vile kununua vipuri na matengenezo mengine. Kwa kifupi nilisema kwamba kuyaweka magari hayo barabarani ni sawa na kuchukua fedha za walipa kodi na kuzichoma moto! [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wakati tukielekea mwaka wa tano serikali ikiwa hajaweza kuamua kimsingi njia ya kuachana na ulevi huu wa magari ya anasa, yule Kagame niliyemzungumzia amekuja na gia mpya kuhusu magari hayo. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Baada ya kupiga marufuku ofisa yeyote wa serikali kutumia gari ya 4X4 na akaagiza kukamatwa kwa magari yote ya serikali na kupigwa mnada wa wazi na badala yake akaagiza watumishi wote wa serikali wenye kustahili kupewa magari wapewe magari madogo, yaani saluni kuanzia ngazi ya mawaziri; mapambano ya Kagame hayajaishia kwenye magari ya serikali tu bali hata yale mashirika ya wafadhili ambayo kwa hakika kwa kila dola za Marekani mia wanazoleta nchi yoyote ya Afrika huchukua kiasi cha dola 80. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mashirika haya nayo yametakiwa yaonyesha kwa vitendo halisi kwamba yanapambana na umasikini si kuishi maisha ya peponi, magari ya kifahari mishahara mikubwa, majumba ya kifahari na kila aina ya ukwasi, lakini juhudi za kupiga vita umasikini zikiwa hazionyeshi mafanikio yoyote. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mafanikio hayaji kwa sababu wanachofanya ni kuleta fedha Afrika kuja kuzitafuna wao wakiwa Afrika. Asilimia zaidi ya 80 ya fedha wanazoleta huzichukua wao kwa mlango wa nyuma (mishahara minono, magari ya kifahari, posho nzito, majumba ya kifahari, maofisi yaliyosheheni samani za bei mbaya, ni kila aina ya anasa). [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Picha hii ya Kagame ikiwa imeganda ndani ya akili zangu kwa muda sasa, wiki iliyopita nilijisikia mnyonge baada ya kutembelea baadhi ya wilaya za mkoa wa Songea, Rukwa, Morogoro, Shinyanga na Mwanza. Ni vigumu kusadiki kwamba viongozi wetu huwa wanatembelea maeneo haya na bado wakarejea Dar es Salaam kuendelea kuishi maisha ya ukwasi wanayoendelea nayo bila kuwaza jinsi ya kuwakomboa watu hawa. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Akiahirisha mkutano wa 19 wa Bunge mwezi uliopita Waziri Mkuu Pinda alisema inakadiriwa kwamba ifikapo mwaka 2018 makao makuu yote ya mikoa ya Tanzania yatakuwa yameunganishwa kwa barabara ya lami. Niliposikia mwaka uliotajwa nikiwa safarini Sumbawanga, nilijiona mnyonge kiasi cha kutamani kulia kwa niaba ya wakazi wa mkoa wa Rukwa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif] Kwa kuwa aliyosema Waziri Mkuu bungeni ndiyo mipango ya serikali katika ujenzi wa barabara nchini ina maana wakazi wa mkoa wa Rukwa wataendelea kupata tabu wanayopata sasa hadi utawala wa awamu ya nne unamaliza muda wake na miaka mingine mitatu ya awamu ya tano ndipo wataweza kusafiri kwa lami kutoka Tunduma hadi Sumbawanga. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Jaribu kufikiria safari ya basi kutoka Tunduma hadi Sumbawanga, kiasi cha km 225 huchukua saa saba! Mateso makubwa ndani ya nchi ambayo wapo wengine wanaishi kama wapo peponi. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Ni kweli tunasema Tanzania ni masikini, na kwa ujumla wananchi wameimbiwa wimbo huo kwamba tu masikini kiasi cha kushindwa kujenga barabara za lami ambazo zitafungua nchi kwa shughuli za maendeleo nao wamesadiki. Lakini wakati wimbo huu wa umasikini unapoimbwa hakuna uwiano wa moja kwa moja wa maisha wanayoishi baadhi ya watu waliotokea kukalia ofisi za umma na nyimbo hizi. Mojawapo ya vielelezo hivyo ni matumizi ya serikali na maofisa wake hasa katika vitu vya anasa, mashangingi yakichukua nafasi kubwa katika upondaji wa raha hizi. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Huwezi kujua ni kwa nini Rwanda ambayo mwaka 1994 ilikaribia kabisa kufutika kwenye uso wa dunia kutokana na mauaji ya kimbari, leo hii hatufui dafu kwao kwa kasi ya maendeleo? [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Yaani wameweza kuunganisha vipande vipande vya nchi na sasa inasonga mbele kwa kasi kubwa. Sisi pamoja na kuwa na rasilimali nyingi zaidi, kwa maana ya ardhi, madini, maji, watu, mbuga za wanyama na kila aina ya kivutio cha utalii, milango ya kuingia baharini, tukiwa tumezingirwa na maziwa kila kona; hatuwezi kusonga mbele kwa kasi inayoonyesha matumaini ya kutia moyo! [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Tafakari kila siku iendayo kwa Mungu sarafu yetu inazidi kudidimia dhidi ya dola, huo maana yake ni uchumi tete, hakuna kinachofanyika kwa maana ya kusaidia nchi hii isisimke kwa kasi na mwendo uliotarajiwa. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Pengine sasa ni wakati wa kujiuliza kama taifa tumefungwa na nini kiasi cha kushindwa kuchukua maamuzi mazito na magumu kwa ajili ya kuiponya nchi? Tujiulize maswali haya huku tukitafakari kwamba tunatamani vipi kuishi kwenye ukwasi wakati umma ukiendelea kutopea katika lindi la umasikini mwaka hadi mwaka?[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif] Tujiulize tena tena kuna maana gani basi ya kuwa kiongozi, kama hatuwezi kubadili hali za watu wetu kutoka maisha ya adha na mashaka makubwa ili kuwapa neema na nafuu zaidi ya maisha yao . [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Ukitembelea wilaya nyingi za nchi hii hata makao makuu ya mikoa mingi, hakika utagundua viongozi wetu wengi wameamua kufumba macho kwa hali duni za wananchi wetu, hawana nia wala msukumo wowote wa kuwakwamua hapo walipo alimradi wao wanapata maisha yao ya ukwasi hapa Dar es Salaam. Kwa nini basi tuombe uongozi kama hatuwafikirii wananchi hawa? [/FONT]



CHANZO: NIPASHE
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom