tajirijasiri
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 2,863
- 3,851
Kwa mujibu wa report ya CAG, kuna kasoro kadhaa katika utengenezaji wa Marine Vessel (MV) Dar Es Salaam maarufu kwa jina la "Kivuko Chakavu" kilichonunuliwa na aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, ambaye sasa ni Rais wa nchi Mh. Magufuli kwa jumla ya Tsh bilioni 7.9, na ili hali hakifanyi kazi mpaka sasa.
Ili ukweli ujulikane zaidi, tunaomba tuwekewe hadharani, ile Inspection and Acceptance report (Taarifa ya Ukaguzi na Makabidhiano) ya meli hiyo, baina ya Serikali na Mtengenezaji. Humo ndimo tutagundua ukweli zaidi juu ya hali halisi ya kivuko hicho.
Hizi sio fedha za CCM au za Magufuli, Bali ni fedha za walipa kodi ambao ni wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nikiwemo Mimi, wewe na yule.
Nawasilisha.