Tunamuomba Paul Makonda mkoani Songea

Aman Ng'oma

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
954
510
Hivi karibuni nilifanya ziara ya kwenda Namtumbo my sweet home kwa ajili ya kusalimia ndugu jamaa na marafiki. Lakini kiukweli nilimmiss sana My Babu, My Mama, My Baba na wengine wengi. Nilishindwa kujizuia ilinibidi nisafiri umbali wa kilometa 780 kutoka Dodoma mjini hadi Namtumbo. Namshukuru Mwenyezi Mungu wote niliwakuta wakiwa salama salmin.

Wakati naelekea huko nilipanda basi la Superfeo wenyewe wanaliita mwamba wa Kusini. Kampuni hii kwakweli wamejipanga hasa, mabasi yao yametawanyika karibu kila kona, ni mabasi mazuri ile mbaya kwa mwanekano wa nje na hata ndani. Lakini kwa mabasi yanayofanya safari kutoka Dodoma kwenda Songea yana dosari kidogo ukilinganisha na yale yanayoenda Dar es saalam yakitokea Songea nadhani kwa kuwa njia hii ya Dodoma wako peke yao, wanakosa ushindani hivyo wanabweteka ndiyo maana wanatuletea mabasi yaliyochoka. Hakuna choice kama ilivyo kwa safari ya Songea - Dar es salaam. Ushindani umefanya kila kampuni iwe na mabasi mazuri yenye kiwango cha hali ya juu.

Kama mjuavyo, wakazi wa Ruvuma wako tofauti kidogo na mikoa mingine, wao wanahitaji zaidi value for money, ndiyo maana njia ya Songea ukitaka kusurvive kwenye biashara ya kusafirisha abilia basi uwe na mabasi mazuri vinginevyo utakufa kifo cha mende. Kwetu mabasi mangalangala hayana nafasi katika biashara ya kusafirisha abilia hapa nazungumzia root ndefu za nje ya mkoa. Hakuna hata yale ya three by two yote ni luxury na ni two by two. Tatizo la root ya Dodoma ni kukosa ushindani na hali hii inakufanya abilia kama abilia ukose alternative hivyo kulizamika kupanda magari hayo kwa maana unakuwa huna uchaguzi mwingine. Tunahitaji kampuni nyingine moja au mbili kama ilivyo root ya mbeya - Dodoma au Songea- Dsm.

Kitu kingine nilichokiona kama dosari ni barabara ya kutoka Njombe hadi Songea. Barabara hii ni mbaya sana kwa kweli inahitaji kutazamwa kwa jicho la huruma. Barabara ni finyu ile mbaya lakini vilevile imejaa viraka tele. Ni muhimu ikafanyiwa nusra kwa kutengenezwa upya kwa kiwango cha kimataifa. Ijazwe kifusi cha kutosha na vilevile itanuliwe iwe pana ili iweze kiruhusu magari kupishana kirahisi. Naamini utengenezaji mpya wa barabara hiyo muhimu itasaidia sana kupunguza ajari za mara kwa mara.

Barabara ya Njombe Songea ni barabara Kongwe hapa nchini, jinsi ilivyo ni kama nyoka, ina makona ya kutisha yaliyojikunja. Usithubutu kumpa mgeni gari yako aiendesha bila kuwa na mwenyeji pembeni atakayemuongoza vinginevyo wahehe wanasema wifa wilola, uwezekana wa kulidondosha ni mkubwa. Uzoefu wake usikupe kiburi. Jitahidi dareva mgeni akae pembeni kama kondakta kwa muda wa wiki angalau moja hivi baada ya hapo sasa wewe bosi unaweza kumwachia tu gari dereva wako alizungushe na kulala nalo katika milima ya Lukumbulu

Mara nyingi unapoenda Songea ukitokea Dsm, Dodoma au Sumbawanga kutokana na kudhibitiwa kwa mwendo kasi wa magari na askari wa usalama barabarani unatua mjini usiku wa haja kidogo kuanzia majira ya saa moja usiku na kuendelea. Sasa unapoigia mjini kitu utakachokutana nacho ni giza tele barabarani. Mji hauna hata taa. Taa pekee utakazo ziona ni zile tu za kwenye stand mpya ya daladala ambayo ujenzi wake umekamilika hivi karibuni iliyopo mjini kati mtaa wa Mfaranyaki na taa nyingine utaziona kwenye sheli za watu Binafsi.

Barabara nyingi za mitaani ni mbaya kweli kweli. Zimejaa vumbi na mashimo yaliyotokana na kuharibiwa na mvua. Mimi najiuliza huu mkoa hauna mapato ya kuweza kuboresha miundombinu yake ya barabara na kuziwekea taa na hatimaye mji ukaonekana mzuri wenye kung'aa? Hivi mikoa mingine wanapata wapi pesa za kuwekea mataa barabarani pamoja kuboresha barabara za mitaani? Mji ukiwa unang'aa taa usiku unaleta uhai. Biashara zinaweza kufanyika vizuri lakini vilevile unapunguza vibaka mitaani.

Bado najiuliza madiwani, mkurugenzi, mafisa mipango pamoja na maafisa maendeleo wa manispaa wanafanya nini kutatua hayo matatizo, au hawayaoni?. Hivi hawaoni kwenye miji ya wenzao wanavyoenda kutembea, aibu haiwashiki kweli?. Kuhamishiwa kwa stand mpya ya mabasi ya mikoani msamala tunashukuru kwa hilo imesaidia katika ukuaji wa mji lakini vilevile kuondoa msongamano wa magari mjini kati lakini mimi tatizo langu ni moja tu uamuzi huo ulipotolewa je manispaa ilijipanga vizuri kweli au ulikuwa uamuzi wa kukurupuka? Inakuwaje stand kuu ya mabasi ikakosa taa ilihali tukijua kabisa mabasi mengi yanaanza kuingia saa kumi na nusu alfajiri ili kupakia abilia na kuelekea mikoani na yale yanayotoka mikoani yanaingia pale Msamala stand Songea mjini kuanzia saa moja usiku na kuendelea hasa yale ya masafa marefu mfano yale ya kutoka Dsm, Dodoma na Sumbawanga, hapo wageni tunawapa picha gani juu ya mji wetu? Je usalama wa abilia na wenyeji wanaokuja kupokea ndugu zao tunauangalia?

Nimeona nguzo mbili ndefu za kufunga taa zenye taa mbili kila nguzo lakini ajabu haziwaki taa hizo. Ni nani aliyekuwa mkandarasi wa ujenzi wa stand hiyo ambayo hadi leo taa zake haziwaki. Na ukitazama chini stand imejaa vumbi yaani tabu tupu. Hivi mheshimiwa Mbunge ameliona hili? Hivi Ruvuma yote tumekosa waandikaji wa proposal za kuomba ufadhili wa ujenzi wa stand mpya ya kisasa na yenye hadhi kama mikoa mingine? Songea ni makao makuu ya mkoa wa Ruvuma wanazidiwa hata na Manispaa ya Mbinga kwa kuwa smart hii ni ajabu sana kwakweli. Ni nini kinachoshindikana.

Natamani siku moja Rais Dr. John Pombe Magufuli afanye mabadiliko kidogo ya wakuu wake wa mikoa au kama ingeruhusiwa tungeazimishwa Mkuu wa mkoa wa Dar es salam Bwana Paul Makonda aje Ruvuma naamini angeitengeneza misingi mizuri na kuinyoosha Songea na Ruvuma kwa ujumla, inatia aibu kwakweli si tu kwa wageni hata wenyeji. Songea ni kioo cha mkoa wa Ruvuma. Mkoa wa Ruvuma siyo masikini hata kidogo nadhani tunakosa wapanga mipango wazuri. Ruvuma tuna kila kitu Ardhi safi inayostawisha kila mazao tatizo nini?

Tuna Mawaziri watano mkoani kwetu, tunacho waomba wawajibike kwa nchi na kwa mkoa wetu. Wasaidie kutatua kero zetu. Waone dosari zilizopo na wasaidie kutoa majawabu. Tuliwachagua ili watutumikie kwanza sisi. Tutawashangaa kama watauaha mkoa wetu ukidorora.

Timu yetu ya majimaji inasuasua katika ligi kuu kwa kukosa pesa. Lakini wananchi wako tayari kuichangia timu yao kiasi chochote kinachohitajika lakini nani wa kuwasha moto kiberiti aliye mwaminifu kusimamia zoezi hilo? Timu imekuwa ya uchaguzi. Kipindi cha uchaguzi lazima ipande daraja, kila mtu anajitokeza kuichangia na wengine kuitafutia ufadhili lakini baada ya uchaguzi hakuna anayeitazama. Majimaji ni nembo ya kuutangaza mkoa wetu lazima wana Ruvuma popote kila mtu alipo aionee fahari timu ya hiyo na kwamba ni jukumu letu kujitoa kuisaidia ili isishuke daraja.

Asante

Mwana Ruvuma Mzalendo

Aman Ng'oma

Dodoma
 
Yaani ukifika mbinga angalau kuliko songea, sijui nini kinausibu ule mkoa!
 
Elimu elimu elimu, watu wamejiridhikia na maisha hayo, wazee ni wengi, vijana wamekimbilia Dar, madiwani na wabunge, asilimia 90 ni magamba wapiga madili kiasi kwamba ukichukua Songea na Makambako, Makambako wamechagamka.
 
Shabiby analeta mabasi Dodoma -Songea.
Waambie wangoni wenzako wachague viongozi wazuri mbunge na madiwani ili waweze kuwaongoza kusukuma gurudumu la maendeleo.
 
Rushwa ni kansa kubwa kwa wote wanaokuja kuongoza Ruvuma. Kuna wafanyabiashara wanne tu pale mjini ndio wanaamua nini kiwe. Mji ule hauwezi kuendelea kwa viongozi wake kuendekeza rushwa. Mfano mzuri ni hiyo stand. Viongozi wamepokea sana rushwa toka kwa hawa wafanyabiashara kiasi kila mtu kuwa na maamuzi yake.
 
Nasikia huko kwa wangoni na wayao hawataki fujo,hata magreda yanajua ,ukilipeleka huko hata likiwa jipya linakataa kufanyakazi,hata ukitaka kung'oa mti ili uchonge barabara pia mti unagoma kung'oka.
 
1-Inabidi tubadilike sana wanaruvuma tuache Majungu na unafki, Mfano kama ndugu yetu [HASHTAG]#Lizaboni[/HASHTAG] yeye anawaza majungu na unafki 2- Ccm haiwez leta maendeleo songea
 
Hivi karibuni nilifanya ziara ya kwenda Namtumbo my sweet home kwa ajili ya kusalamia ndugu jamaa na marafiki. Lakini kiukweli nilimmiss sana My Babu , My Mama, My Baba na wengine wengi. Nilishindwa kujizuia ilinibidi nisafiri umbali wa kilometa 780 kutoka Dodoma mjini hadi Namtumbo. Namshukuru Mwenyezi Mungu wote niliwakuta wakiwa salama salmin.

Wakati naelekea huko nilipanda basi la Superfeo wenyewe wanaliita mwamba wa Kusini. Kampuni hii kwakweli wamejipanga hasa, mabasi yao yametawanyika karibu kila kona, ni mabasi mazuri ile mbaya kwa mwanekano wa nje na hata ndani. Lakini kwa mabasi yanayofanya safari kutoka Dodoma kwenda Songea yana dosari kidogo ukilinganisha na yale yanayoenda Dar es saalam yakitokea Songea nadhani kwa kuwa njia hii ya Dodoma wako peke yao, wanakosa ushindani hivyo wanabweteka ndiyo maana wanatuletea mabasi yaliyochoka. Hakuna choice kama ilivyo kwa safari ya Songea - Dar es salaam. Ushindani umefanya kila kampuni iwe na mabasi mazuri yenye kiwango cha hali ya juu.

Kama mjuavyo, wakazi wa Ruvuma wako tofauti kidogo na mikoa mingine, wao wanahitaji zaidi value for money, ndiyo maana njia ya Songea ukitaka kusurvive kwenye biashara ya kusafirisha abilia basi uwe na mabasi mazuri vinginevyo utakufa kifo cha mende. Kwetu mabasi mangalangala hayana nafasi katika biashara ya kusafirisha abilia hapa nazungumzia root ndefu za nje ya mkoa. Hakuna hata yale ya three by two yote ni luxury na ni two by two. Tatizo la root ya Dodoma ni kukosa ushindani na hali hii inakufanya abilia kama abilia ukose alternative hivyo kulizamika kupanda magari hayo kwa maana unakuwa huna uchaguzi mwingine. Tunahitaji kampuni nyingine moja au mbili kama ilivyo root ya mbeya - Dodoma au Songea- Dsm.

Kitu kingine nilichokiona kama dosari ni barabara ya kutoka Njombe hadi Songea. Barabara hii ni mbaya sana kwa kweli inahitaji kutazamwa kwa jicho la huruma. Barabara ni finyu ile mbaya lakini vilevile imejaa viraka tele. Ni muhimu ikafanyiwa nusra kwa kutengenezwa upya kwa kiwango cha kimataifa. Ijazwe kifusi cha kutosha na vilevile itanuliwe iwe pana ili iweze kiruhusu magari kupishana kirahisi. Naamini utengenezaji mpya wa barabara hiyo muhimu itasaidia sana kupunguza ajari za mara kwa mara.

Barabara ya Njombe Songea ni barabara Kongwe hapa nchini, jinsi ilivyo ni kama nyoka, ina makona ya kutisha yaliyojikunja. Usithubutu kumpa mgeni gari yako aiendesha bila kuwa na mwenyeji pembeni atakayemuongoza vinginevyo wahehe wanasema wifa wilola, uwezekana wa kulidondosha ni mkubwa. Uzoefu wake usikupe kiburi. Jitahidi dareva mgeni akae pembeni kama kondakta kwa muda wa wiki angalau moja hivi baada ya hapo sasa wewe bosi unaweza kumwachia tu gari dereva wako alizungushe na kulala nalo katika milima ya Lukumbulu

Mara nyingi unapoenda Songea ukitokea Dsm, Dodoma au Sumbawanga kutokana na kudhibitiwa kwa mwendo kasi wa magari na askari wa usalama barabarani unatua mjini usiku wa haja kidogo kuanzia majira ya saa moja usiku na kuendelea. Sasa unapoigia mjini kitu utakachokutana nacho ni giza tele barabarani. Mji hauna hata taa. Taa pekee utakazo ziona ni zile tu za kwenye stand mpya ya daladala ambayo ujenzi wake umekamilika hivi karibuni iliyopo mjini kati mtaa wa Mfaranyaki na taa nyingine utaziona kwenye sheli za watu Binafsi.

Barabara nyingi za mitaani ni mbaya kweli kweli. Zimejaa vumbi na mashimo yaliyotokana na kuharibiwa na mvua. Mimi najiuliza huu mkoa hauna mapato ya kuweza kuboresha miundombinu yake ya barabara na kuziwekea taa na hatimaye mji ukaonekana mzuri wenye kung'aa? Hivi mikoa mingine wanapata wapi pesa za kuwekea mataa barabarani pamoja kuboresha barabara za mitaani? Mji ukiwa unang'aa taa usiku unaleta uhai. Biashara zinaweza kufanyika vizuri lakini vilevile unapunguza vibaka mitaani.

Bado najiuliza madiwani, mkurugenzi, mafisa mipango pamoja na maafisa maendeleo wa manispaa wanafanya nini kutatua hayo matatizo, au hawayaoni?. Hivi hawaoni kwenye miji ya wenzao wanavyoenda kutembea, aibu haiwashiki kweli?. Kuhamishiwa kwa stand mpya ya mabasi ya mikoani msamala tunashukuru kwa hilo imesaidia katika ukuaji wa mji lakini vilevile kuondoa msongamano wa magari mjini kati lakini mimi tatizo langu ni moja tu uamuzi huo ulipotolewa je manispaa ilijipanga vizuri kweli au ulikuwa uamuzi wa kukurupuka? Inakuwaje stand kuu ya mabasi ikakosa taa ilihali tukijua kabisa mabasi mengi yanaanza kuingia saa kumi na nusu alfajiri ili kupakia abilia na kuelekea mikoani na yale yanayotoka mikoani yanaingia pale Msamala stand Songea mjini kuanzia saa moja usiku na kuendelea hasa yale ya masafa marefu mfano yale ya kutoka Dsm, Dodoma na Sumbawanga, hapo wageni tunawapa picha gani juu ya mji wetu? Je usalama wa abilia na wenyeji wanaokuja kupokea ndugu zao tunauangalia?

Nimeona nguzo mbili ndefu za kufunga taa zenye taa mbili kila nguzo lakini ajabu haziwaki taa hizo. Ni nani aliyekuwa mkandarasi wa ujenzi wa stand hiyo ambayo hadi leo taa zake haziwaki. Na ukitazama chini stand imejaa vumbi yaani tabu tupu. Hivi mheshimiwa Mbunge ameliona hili? Hivi Ruvuma yote tumekosa waandikaji wa proposal za kuomba ufadhili wa ujenzi wa stand mpya ya kisasa na yenye hadhi kama mikoa mingine? Songea ni makao makuu ya mkoa wa Ruvuma wanazidiwa hata na Manispaa ya Mbinga kwa kuwa smart hii ni ajabu sana kwakweli. Ni nini kinachoshindikana.

Natamani siku moja Rais Dr. John Pombe Magufuli afanye mabadiliko kidogo ya wakuu wake wa mikoa au kama ingeruhusiwa tungeazimishwa Mkuu wa mkoa wa Dar es salam Bwana Paul Makonda aje Ruvuma naamini angeitengeneza misingi mizuri na kuinyoosha Songea na Ruvuma kwa ujumla, inatia aibu kwakweli si tu kwa wageni hata wenyeji. Songea ni kioo cha mkoa wa Ruvuma. Mkoa wa Ruvuma siyo masikini hata kidogo nadhani tunakosa wapanga mipango wazuri. Ruvuma tuna kila kitu Ardhi safi inayostawisha kila mazao tatizo nini?

Tuna Mawaziri watano mkoani kwetu, tunacho waomba wawajibike kwa nchi na kwa mkoa wetu. Wasaidie kutatua kero zetu. Waone dosari zilizopo na wasaidie kutoa majawabu. Tuliwachagua ili watutumikie kwanza sisi. Tutawashangaa kama watauaha mkoa wetu ukidorora.

Timu yetu ya majimaji inasuasua katika ligi kuu kwa kukosa pesa. Lakini wananchi wako tayari kuichangia timu yao kiasi chochote kinachohitajika lakini nani wa kuwasha moto kiberiti aliye mwaminifu kusimamia zoezi hilo? Timu imekuwa ya uchaguzi. Kipindi cha uchaguzi lazima ipande daraja, kila mtu anajitokeza kuichangia na wengine kuitafutia ufadhili lakini baada ya uchaguzi hakuna anayeitazama. Majimaji ni nembo ya kuutangaza mkoa wetu lazima wana Ruvuma popote kila mtu alipo aionee fahari timu ya hiyo na kwamba ni jukumu letu kujitoa kuisaidia ili isishuke daraja.

Asante

Mwana Ruvuma Mzalendo

Aman Ng'oma

Dodoma
kaka unazungumzia Mbunge? kwanza akifika yupo kwenye kiyoyozi hakuna anachokijua nakwambia; ila pia kuhusu nani aliazisha ni bwana Chale Mhagama aliyekuwa meya wa manispaa ya Songea na ndiye aliyefuja fedha nyingi sana za maendeleo pamoja na aliyekuwa mkurugenzi wa manispaa hiyo bwana Zacharia
 
Back
Top Bottom