Tunamuenzi vipo Edward Moringe Sokoine?

Gagurito

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
5,600
804
Ni miaka 28 sasa imetimia tangu sisi kama taifa tuondokewe na Waziri Mkuu wetu kipenzi cha wengi, Mzalendo wa kweli, Mchapa kazi, Kiboko cha Mafisadi, wala Rushwa na wahujumu uchumi Hayati Ndg. Edward Moringe Sokoine.

Kwa Moyo wa dhati nathubutu kusema katika list ya Mawaziri wakuu wa Tanganyika/Tanzania tukiondoa Mwl. Julius Kambarage Nyerere na wale waliomtangulia kabla yake, hawa wote waliomfuatia hakuna hata mmoja aliyeweza ama kuthubutu Kuziba pengo lake.

Katika kumuezi mchango wake ktk maendeleo ya Taifa letu, Je tunamuenzi vipi? Tumuenzi vipi? Hapa nazungumzia pande zote, 1. Kwetu sisi wananchi na 2. Jitihada za Serikali, kwani ipo wazi huyu bwana kasahaulika. Mungu Amlaze mahala pema peponi.

Amen!
 
Back
Top Bottom