Tunamsaka RAIS WA 2015: Ulimboka STYLE au Zitto STYLE..

TAMKO

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
1,090
762
Ndogu Watanzania wenzangu..

hususan watu makini nguli wa mitazamo humu Jamvini, tutafakari hili kwa uzito unaostahili, Tanzania Tuliyonayo leo, Tanzania iliyopoteza Muelekeo, Tanzania tajiri iliyobatizwa jina la maskini, Tanzania inayoongozwa na makatili, wauaji, watu wa Damu , wasiojali utaifa wala wataifa, inahitaji Raisi mpya 2015. na raisi wetu tuangalie je ni kweli bado tunahitaji raisi mwenye mlengo wa Ulimboka style au Zito Style?.

Kifupi Ulimboka style of President candidate ni mtu mwenye vitu Vingi vya kupoteza, ni jasiri wa kuanzisha au kuibua hoja nzito lakini si jasiri wa kuziendeleza hadi ukomo, akitishiwa kidogo huftata mkia akaogopa kutulia kwa kuhofia kupoteza malavidavi ya mkewe, watoto, familia, nyumba, mali, kazi eeee na mengi tu. Utaskia "bora ujikalie kimywa mkeo asijekuwa mjane bure..watoto wako watasomeshwa na nami au watakuwa wanamwita dady!!Dady!! nani?, he mkeo ataolewa na jamaa zako na mali zako jamaa waliomuoa mkeo wataziinjoi na hao jamaa zako au mkeo atawalazimisha watoto wako wawaite dady!! wewe ukiozea udongoni!!" sentensi kama hizo lazima zimpate na tusimlaumu sana akizithamini, Ukombozi wa Taifa letu unahitaji mtu hasa wa kujitoa sio hizi blabla.


Zitto style of President candidate ni mtu asiye vitu Vingi vya kupoteza, ni jasiri wa kuanzisha au kuibua hoja nzito akazisimimamia bila kuangalia uso mbuzi wa mtu. sisemi kwamba Zitto ana wasifu wa namna hii lakini kidogo anakaribia, si kama Mtu ambaye usiku anaambiwa na mkewe "Honey achana nao hao watakufanya nijiskie mnyonge wakikuua, je wewe unapenda kitanda hiki Deo aje akilalie na kuninanihii wewe ukifa?, je unapenda malavidavi yote haya nije kumgawia Mwaikonde wewe wakikuasasinate, achana nao honey tulee watoto wetu"..Hoja yangu naikita zaidi kufikiria kwamba yamkini tunahitaji candidate ambaye hana Mke wala watoto kwa sasa, Jasiri asiyeogopa, mwenye uzalendo wa kweli..

sred zangu, na mamia ya post zangu humu JF nimekuwa nikiwapinga vikali viongozi sampuli ya Zitto, kwa kijimsemo kwamba kama huna familia unayoiongoza (hasahasa mke na watoto) utawezaje kuongoza jamii, lakini kwa sasa tukio la ulimboka kutekwa na kupigwa na watu ANAOWAJUA yeye Ulimboka, hiyo june 28, 2012 na kutibiwa anakujua yeye hadi kurejea nchini Agost 12,2012.. na ukimya aliokuwa nao hadi leo tunakaribia kufunga jamvi la mwaka, kinyume na matarajio ya jamii yote kwamba angeunguruma kwenye media na kuweka mambo yote hadharani na kutuachia kazi wananchi, badala yake kachikichia, lazima mtu uwe na kitu cha kujiuliza hapa, kitu gani kilichomfanya aisaliti matarajio ya jamii na je tuna haja ya kuhitaji viongozi wa sampuli hii?..

ni hoja yangu tu waweza kuijadili kwa hoja pia na mtazamo wako..
 
mzee tupatupa mnamo 13 sept alipost kitu hiki


lakini Boss ukaja ukihemea juu juu this way



hapo kwenye Red Ulimaliza kila kitu mkuu

mwingine tena akaja na hii



Ukiskia umaskini wetu wa mawazo ndo huu sasa.

huyu nae akabisha
Dr. Ulimboka is sufferring from amnesia. Amekwishawasahau watu waliomtesa Hata wewe ungekuwa na amnesia kama ungeng'olew kucha na jino. We mwache huyo ndugu akae kwa amani.


mwenzangu huyu mwenye akili za kijiko cha chai nae akaona achangie maada hiyo hiyo



huyu asiyejua maaana ya mapinduzi nae akaona heri alete hoja yake


huyu akawa kama mie hivi
Nilikua mshabiki wake,
Lakini kwa sasa nishajitoa. Naamini atakua kadakishwa zake, katulia!!
 
Ulimboka na Zitto wote vigeugeu.
Anayefaa kuwa rais 2015 ni
Dr.Slaa au Tundu Lissu.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Mnashangaza sana watz. Mlitaka Ulimboka aseme nn zaidi muamini?Aliitaja namba ya mtesaji wake na ku-confirm kuwa ndie. Mwanahalisi wakatoa wasifu na kazi ya mtu huyo....vyombo vyote viliona,wanachi, wanaharakati na hata wanajamvi hapa JF waliona.

Sasa mlitaka Ulimboka afanye nn zaidi? Afanye nn zaidi ya yy kuitwa tu kumtambua mtesaji wake? Afanye nn zaidi? Wale madaktar wenzie aliowapigania maslahi ba mazingira bora ya kazi wamerudi nyuma, wamemtenga hatujui, wamemsaliti hatujui au wameridhika hatujui

Wananchi ambao Ulimboka aliwapigania wapate huduma bora na matibabu ya uhakika yanayotofautisha daktari na mganga mpiga ramli wako wapi? Wameridhika na huduma za hospitali zetu? hatujui..wanaogopa kuacha wajane? au kung'olewa meno? hatujui...

Mlitaka Ulimboka afanye nn?ageuke polisi mkamataji,mwendesha mashtaka na hakimu ili amfunge mtesaji wake?


Poor Tanzania, Poor people..


Ulimboka did his part, and he didu it well enough....
 
mh, Zitto style anafaa saaana , ila ulimboka style nayo si mbaya maana naye ameonyesha usikivu, baada ya kuface the music, naaamini ana siri nzitto na watesi wake hivyo kwa ule usikivu na maonyo aliyopata toka kwa watesi wake na ametii basi si vibaya tumpe umakamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…