Philosophical thoughts by Bishop Benson Kalikawe Lwakalinda Bagonza (PhD)
WOTE TUKO NJIAPANDA: Tupande gari gani?
Humphrey Polepole ametuweka njia panda sote. Anayedhani hayuko njia panda, yawezekana tayari ni abiria wa gari la mbele. Tutafakari:
1. Kuna watu usipowasikiliza, ni hasara. Ukiwasikiliza ni hasara pia. Humphrey Polepole ni mmoja wao. Usipomsikiliza unakosa mengi. Ukimsikiliza, anakushawishi kutenguka katika basdhi ya misimamo yako. Chagua kwa hekima.
2. Nani ni bora? Shetani aletaye habari njema au malaika aletaye habari mbaya?
Tuangalie kwa makini vipa umbele vyetu:
-Mungu/Taifa/Chama
Vs
-Chama/Taifa/Mungu
Chagua kwa hekima.
3. Twaweza kumpuuza Humphrey Polepole. Je tutapuuza madhara ya kumpuuza? Chagua kwa busara kati ya kupuuza huku usiweze kupuuza madhara ya upuuzi wako.
Kama anasema uwongo anamdanganya nani? Mungu? Wananchi? Yeye mwenyewe?
4. Kama ni kweli tufanyeje? Kama ni uwongo tufanyeje? Kwa nini aliyoyasema yanafanana na imani na uzoefu wetu? Kwa nini wanaosema aliyoyasema ni uwongo hata wao wanajiona ni waongo?
5. Viapo vyetu viko njiapanda: kukiuka kiapo kwa kusema kweli au kutunza kiapo kwa kuficha ukweli? Tunapoapa twamwapia mwanadamu au Mungu? Tukishupaza shingo (Impunity), twamfanyia Polepole, Katiba, Katiba, wananchi?
6. Hatujui tumefikaje hapa. Tuna uwezo wa kujua tutokeje. Tulinde kura moyoni? Tutiki wakati imeishatikiwa? Tusubiri reform?
Tupige kura kuamua kama tuchague au tusichague?
Unyenyekevu si udhaifu
TURUDI MEZANI
UKWELI ULIOCHELEWA NI BORA KULIKO UWONGO UNAOFARIJI.
HAKUNA TOBA ILIYOCHELEWA