Wadau!
Nimetafakari hili kwa muda mrefu lakini pia ni vema nikaona tushirikiane katika kufahamishana zaidi. Ukiitazama dunia ya leo tunaelekea katika KUTOAMINIANA, ikiwa zamani watu walikaribisha hata watu wasiwajua wakalala katika majumba yao hata kuishi kabisa leo hii kumwambia mtu alale japo upenuni ni mashaka matupu.
Hayo ni kwa kifupi katika jamii yetu, lengo langu ni kuzungumzia DUNIA kwa sababu ndio jahazi letu sote, na sote tunafanikiwa tukiwa humu ama kukwama.
LEO Kila mahala kunajengwa CHUKI, UFISADI, DHULUMA na kila aina za UFISADI, na haitoshi wanaofanya UFUSADI NDIO WENYE KUSIFIWA. Nina khofu sana CHUKI ZA KIBAGUZI zinazojengwa LEO ndizo zitakuwa MAANGAMIZI kwa KIZAZI kinachofuata.
Nimekumbuka hadithi ya Hannibal mwana wa Hamilcar aliyeishi inakadiriwa miaka 247 183 au zaidi kidogo kabla ya kuzaliwa Masihi kwanini namtolea mfano shujaa huyu? Baba yake Hannibal alizoea kumwambia mwanawe juu ya Adui zake (ambayo yalikuwa ni mataifa makubwa wakati huo) hili lilijenga chuki kubwa moyoni mwa mtoto huyo, na hatimae alikusanya maarifa mengi na hatimae kuwa jemedari mkubwa wa vita... Kwanini? Kwa sababu akiona ni vema kufa shujaa kuliko kuishi kinyonge.
Tusipoangalia NDIKO TUNAKOELEKEA, Leo wako watu kwa makusudi wanaeneza CHUKI kana kwamba wao WATAISHI katika DUNIA hii MILELE. Kesho hawatakuwepo watakuwepo watoto wao je HALI ITAKUWAJE?
LEO HII YAPO MATAIFA YANAYOONA YANA HAKI ZOTE, Na mengine ni Mataifa Manyonge, je yatakuwa hivyo mpaka lini?
Leo Idadi ya wabwiaji inaongezeka je vipi ikifika siku hizo HAKUTAKUWA NA WABWIAJI VIONGOZI WA NGAZI ZA JUU?
JE WAKIZINGUANA NINI KINATOKEA...
yako mengi mengi mengi ya kutafakari na kujiuliza lakini MIAKA 25 Ijayo....