Tunajidanganya na makusanyo ya Tax Arrears

PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,666
3,838
Hivi karibuni kumeibuka kauli za viongozi kusifia sana makusanyo ya kodi ambayo kwa miezi ya hivi karibuni yamefikia takribani shilingi trilioni 1.5 kwa mwezi. Jambo hilo limeanza kuwapa kiburi watawala kiasi cha kuanza kukashifu misaada ya washirika wa maendeleo ati kwamba tutaweza kujitegemea.

Huu ni uongo wa asubuhi kabisa, Makusanyo mengi ya kodi yalioongezeka ni tax arrears kwa walipa kodi waliokuwa wanakwepa na waliokuwa na malimbikizo na kiuchumi hayareflect ongezeko la kodi kwa sababu tax base yetu bado ni ile ile.

Ni dhahiri baada ya miezi mitatu ijayo tutarudi kule kule kwa kukusanya bilioni 900 kwa mwezi kama hapo awali sababu hadi sasa hatujatanua vyanzo vipya mapato na zaidi tunaendelea kutegemea ushuru wa forodha wakati large tax payers na domestic taxes zikibaki vile vile.

Kuhusu utegemezi wa misaada hapo ndio nashangaa watawala wetu. Kiuhalisia nusu ya bajeti yetu ni misaada sababu asilimia 30 ni wahisani wa maendeleo na asilimia 20 ni misaada na mikopo nafuu. Leo hii tunajitoa ufahamu kwa kuwatukana wafadhili sababu ya ufedhuli wetu tuliofanya Zanzibar.

Na zaidi ya yote tujiulize ni namna gani tutajitegemea kwa hiyo trilioni moja nukta tano wakati wage bill yetu kwa mwezi ni bilioni 550 jumlisha na fedha za OC ambazo nazo ni first charge utakuta ni karibu bilioni 800 sasa hiyo bilioni 700 inayobaki itaweza kuendesha Nchi kwa kugharamia miradi ya maendeleo. Mathalani kwa mwezi mmoja unaweza kuta makandarasi wameraise certificate za karibu bilioni 200 kwa kazi wanatakiwa walipwe, kwa hali kama hiyo nchi hii bila msaada haiwezi kwenda.

Nashauri Viongozi na wanasiasa uchwara wa tanzania wawe na akiba za maneno, tunahitaji sana fedha za wafadhili na tujikite kuwekeza kwenye maendeleo ya watu na sio vitu. JPM naye kishaingia kwenye kosa la watangulizi wake kuwekeza kwenye maendeleo ya vitu na sio watu na ndio sababu hadi leo pamoja na kubana matumizi hali ya watanzania imebaki hoe hae kwa sababu hatuelekezi fedha kwenye maendeleo ya watu badala yake tunawekeza kwenye vitu, kulipa deni la taifa , nkujenga barabara na mishahara.
 
Hao wanaCCM wanaokashifu misaada ndio hawa wakifurahia kupiga picha kwenye miradi ya wafadhili.....

10117439e356d80b7bda6f4859ac0324.jpg
 
Ugumu wa maisha ni kipimo cha akili,tutakaoposhindwa kununua mahitaji muhimu kwa watoto wetu mashuleni kwa ajili ya ugumu wa maisha ndo tutatia akili,kwa sasa tuendelee tu na ushabiki
 
Acha ujipu wewe!!!
Makusanyo yameongezeka!
Tangu mwezi December mnasema ni arrears mpaka March hii bado ni arrears??
Hebu ondoa tope kichwani!!!
 
Hao wanaCCM wanaokashifu misaada ndio hawa wakifurahia kupiga picha kwenye miradi ya wafadhili.....

10117439e356d80b7bda6f4859ac0324.jpg
Wamezoea kujidanganya na kudanganyika. Sasa huu ugumu wa maisha wanaouzalisha utaibua uhalifu tena wa daraja la juu. Na kwa vile hawa wahalifu wasomi wameshajua pesa haiko kwa walala hoi sasa wakubwa nao wajiandae kukabiliana na uporaji na utekaji watu wakidai ramson kubwa kutoka kwao kama inavyotokea Nigeria na kwingineko kwenye wahalifu wasomi
 
Hivi karibuni kumeibuka kauli za viongozi kusifia sana makusanyo ya kodi ambayo kwa miezi ya hivi karibuni yamefikia takribani shilingi trilioni 1.5 kwa mwezi. Jambo hilo limeanza kuwapa kiburi watawala kiasi cha kuanza kukashifu misaada ya washirika wa maendeleo ati kwamba tutaweza kujitegemea.

Huu ni uongo wa asubuhi kabisa, Makusanyo mengi ya kodi yalioongezeka ni tax arrears kwa walipa kodi waliokuwa wanakwepa na waliokuwa na malimbikizo na kiuchumi hayareflect ongezeko la kodi kwa sababu tax base yetu bado ni ile ile.

Ni dhahiri baada ya miezi mitatu ijayo tutarudi kule kule kwa kukusanya bilioni 900 kwa mwezi kama hapo awali sababu hadi sasa hatujatanua vyanzo vipya mapato na zaidi tunaendelea kutegemea ushuru wa forodha wakati large tax payers na domestic taxes zikibaki vile vile.

Kuhusu utegemezi wa misaada hapo ndio nashangaa watawala wetu. Kiuhalisia nusu ya bajeti yetu ni misaada sababu asilimia 30 ni wahisani wa maendeleo na asilimia 20 ni misaada na mikopo nafuu. Leo hii tunajitoa ufahamu kwa kuwatukana wafadhili sababu ya ufedhuli wetu tuliofanya Zanzibar.

Na zaidi ya yote tujiulize ni namna gani tutajitegemea kwa hiyo trilioni moja nukta tano wakati wage bill yetu kwa mwezi ni bilioni 550 jumlisha na fedha za OC ambazo nazo ni first charge utakuta ni karibu bilioni 800 sasa hiyo bilioni 700 inayobaki itaweza kuendesha Nchi kwa kugharamia miradi ya maendeleo. Mathalani kwa mwezi mmoja unaweza kuta makandarasi wameraise certificate za karibu bilioni 200 kwa kazi wanatakiwa walipwe, kwa hali kama hiyo nchi hii bila msaada haiwezi kwenda.

Nashauri Viongozi na wanasiasa uchwara wa tanzania wawe na akiba za maneno, tunahitaji sana fedha za wafadhili na tujikite kuwekeza kwenye maendeleo ya watu na sio vitu. JPM naye kishaingia kwenye kosa la watangulizi wake kuwekeza kwenye maendeleo ya vitu na sio watu na ndio sababu hadi leo pamoja na kubana matumizi hali ya watanzania imebaki hoe hae kwa sababu hatuelekezi fedha kwenye maendeleo ya watu badala yake tunawekeza kwenye vitu, kulipa deni la taifa , nkujenga barabara na mishahara.
Umeandika vyema, nikuongezee kitu hapa. Domestic na large taxpayer ndio hao hao importers, mfano Azam, Metl, MMI, Aliyekuwa Home shoping, sunda, na wengine
Tunawatoza kodi wakiimport na wanapopata faida pia (domestic). Hivyo basi adhari ya importation inaenda hadi domestic na large taxpayer
 
umesema vema sana mtaalam, ni vema tukaacha ushabiki na tuangalie njia nzuri za kuongeza mapato ya serikali badala ya kutumia media kufrastrate wafanyibiashara, wahisani na watumishi wa umma
 
Bajeti ifuatayo itakuwa takriban trillion 24,makusanyo hata yakiwa trllion1.5 kwa mwezi
1.5*12=18
Hesabu hazidanganyi
Bado tunataka kununua meli na ndege na magari zaidi ya washawasha
 
Hii mada ni murua. Tax base ni ndogo mno. Kwa taarifa tu makusanyo ya kodi Tanzania per GDP ndio yako chini kuliko nchi zote Afrika. Kwa sasa ni chini ya 12% (GDP imefikia Sh 9.0 tri/- kwa mwezi). Kiwango cha chini kinachotakiwa ni kukusanya 25% ya GDP. Ukiangalia ripoti ya hali ya uchumi ya robo mwaka iliyopita utaona sekta zilizoongoza katika kuchangia ukuaji uchumi ni mawasiliano (simu, internet, etc), fedha (mabenki), ujenzi, madini na utalii lakini cha ajabu hizi sekta sio zinazoongoza kwa ulipaji kodi! Sekta ya mawasiliano pekee ilichangia 23% ya ukuaji uchumi. Je kulikuwa na ulipaji kodi unaoendana na ongezeko hilo? Jibu ni hapana! Pia ukusanyaji kodi kutokana na majengo (rental property income tax, stamp duty and property tax) ni kiduchu (negligible). Ukifuatilia utagundua watawala na vigogo wengi wana maslahi binafsi katika hizi sekta na ndio maana hali iko hivyo. Hii ni aina ya ufisadi wa kitaasisi ambao utakomeshwa tu kwa kuweka maadili ya uongozi katika katiba (kitu ambacho CCM hawataki).
 
....exactly....kuna kitu ambacho JPM na utawala wake hawajakiona....kwamba kwa kuwa tax base ya TZ iko chini sana...hata zikikusanywa fedha namna gani hazitotosheleza mahitaji kama nchi...ndio maana kumekua na kilio toka kwa watu makini kuwa serikali iongeze vyanzo vya mapato....
..pili...uchumi wa TZ unaosifiwa kukua uko mijini tu..kwa maana ya Dar....na kwa hivyo hamna uhalisia wa kukua kw uchumi na maendeleo ya watanzania kwa ujumla wao....

...tatu....katika hali hii ya kuanza mapema kuwakejeli wahisani wakati tuna ndoto eti za kufikia uchumi wa kati....wakati miundo mbinu yenyewe iko hoi...tunajidanganya sana...maana wahisani pekee ndio wanaotoa fedha za maendeleo nchi hii....na maendeleo yenyewe ndio kwenye hiyo miundombinu na basic needs ...kama umeme...barabara...maji...elimu n.k...Lazima ijulikane kuwa wakati tunaenda kwenye uchaguzi serikali ya TZ ilikuwa inashindwa hata kulipa mishahara....ukiondolea mbali madeni tele kila kona ya nchi....Leo tunatoa wapi jeuri ya kuwakejeli wahisani???
 
Hivi karibuni kumeibuka kauli za viongozi kusifia sana makusanyo ya kodi ambayo kwa miezi ya hivi karibuni yamefikia takribani shilingi trilioni 1.5 kwa mwezi. Jambo hilo limeanza kuwapa kiburi watawala kiasi cha kuanza kukashifu misaada ya washirika wa maendeleo ati kwamba tutaweza kujitegemea.

Huu ni uongo wa asubuhi kabisa, Makusanyo mengi ya kodi yalioongezeka ni tax arrears kwa walipa kodi waliokuwa wanakwepa na waliokuwa na malimbikizo na kiuchumi hayareflect ongezeko la kodi kwa sababu tax base yetu bado ni ile ile.

Ni dhahiri baada ya miezi mitatu ijayo tutarudi kule kule kwa kukusanya bilioni 900 kwa mwezi kama hapo awali sababu hadi sasa hatujatanua vyanzo vipya mapato na zaidi tunaendelea kutegemea ushuru wa forodha wakati large tax payers na domestic taxes zikibaki vile vile.

Kuhusu utegemezi wa misaada hapo ndio nashangaa watawala wetu. Kiuhalisia nusu ya bajeti yetu ni misaada sababu asilimia 30 ni wahisani wa maendeleo na asilimia 20 ni misaada na mikopo nafuu. Leo hii tunajitoa ufahamu kwa kuwatukana wafadhili sababu ya ufedhuli wetu tuliofanya Zanzibar.

Na zaidi ya yote tujiulize ni namna gani tutajitegemea kwa hiyo trilioni moja nukta tano wakati wage bill yetu kwa mwezi ni bilioni 550 jumlisha na fedha za OC ambazo nazo ni first charge utakuta ni karibu bilioni 800 sasa hiyo bilioni 700 inayobaki itaweza kuendesha Nchi kwa kugharamia miradi ya maendeleo. Mathalani kwa mwezi mmoja unaweza kuta makandarasi wameraise certificate za karibu bilioni 200 kwa kazi wanatakiwa walipwe, kwa hali kama hiyo nchi hii bila msaada haiwezi kwenda.

Nashauri Viongozi na wanasiasa uchwara wa tanzania wawe na akiba za maneno, tunahitaji sana fedha za wafadhili na tujikite kuwekeza kwenye maendeleo ya watu na sio vitu. JPM naye kishaingia kwenye kosa la watangulizi wake kuwekeza kwenye maendeleo ya vitu na sio watu na ndio sababu hadi leo pamoja na kubana matumizi hali ya watanzania imebaki hoe hae kwa sababu hatuelekezi fedha kwenye maendeleo ya watu badala yake tunawekeza kwenye vitu, kulipa deni la taifa , nkujenga barabara na mishahara.
Si kweli maneno yako. Ongezeko l
 
Si kweli maneno yako. Ongezeko la kodi limetokana zaidi na kubana mianya ya matumizi na ufisadi wa kukwepa kodi. Ngoja uone pesa ngapi zitaokolewa kwa kubana mishahara hewa. Si ajabu hiyo trl 1 ikapatikana kwenye mishahara hewa.
 
Si ajabu hiyo trl 1 ikapatikana kwenye mishahara hewa

Ni muhimu kwa serikali kuangalia ulipaji wa madeni yetu yote ya nje na ndani; kuna wizi wa hali ya juu kwa kulipa madeni hewa!!! Magufuli should form a multi disciplinary team to supervise this exercise. Kuwaachia wale wale wa zamani kuifanya hii kazi ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
 
Nashauri Viongozi na wanasiasa uchwara wa tanzania wawe na akiba za maneno, tunahitaji sana fedha za wafadhili na tujikite kuwekeza kwenye maendeleo ya watu na sio vitu. JPM naye kishaingia kwenye kosa la watangulizi wake kuwekeza kwenye maendeleo ya vitu na sio watu na ndio sababu hadi leo pamoja na kubana matumizi hali ya watanzania imebaki hoe hae kwa sababu hatuelekezi fedha kwenye maendeleo ya watu badala yake tunawekeza kwenye vitu, kulipa deni la taifa , nkujenga barabara na mishahara.

Wewe Hauna Akili!
Ulitegemea maisha ya Watanzania yabadilike kwa kipindi hiki raisi wa nchi amekuwa madarakani? Hii iliwahi kutoke wapi? Unaweza kunipa hata mfano mmoja tu popote pale Dunia hii ambapo Serikali iliweza kubadilisha maisha ya wananchi wake kwa miezi michache madarakani ?

Bado narudia hauna Akili! Kazi ya Serikali siyo kukupa fedha bali kazi ya Serikali ni kuweka mazingira ili kumuwezesha Mwananchi aweze kujisadia sasa hayo mazingira ni yapi? Ni kama barabara leo hii Kandarasi wote waliokuwa wamesimamisha kazi kwa kukosa fedha wamelipwa na kazi zinaendela, Mwisho wa Mwaka Ziwa Nyanza(Viktoria) linapata meli mpya na kuunganisha Bandari zote na Meli mpya yenye ufanisi na ya kisasa, Miezi miwili ijayo ndege mpya mbili zitawasili kwa shirika letu kufufuliwa upya, Mishahara hewa imedhibitiwa au inaendela kudhibitiwa ambapo hizo fedha zitapelekwa mahali kwingine kuleta maendeleo, ada imeondolewa kwa watoto wa Shule changamoto bado zipo ikiwa ni pmj na Shule kuzidiwa na watoto lkn linashugulikiwa, Ujenzi wa Reli Mpya uko mbioni kuanza, Tumeweza kufanikiwa kupistiah Bomba la Mafuta nchini mwetu Ujenzi kama mambo yakienda vizuri unaanza mwezi Agosti hii itatoa ajira ya Watanzania zaidi ya 10 000, kuanzia mama lishe , wabeba zege, wasafirishaji, wauza chakula mpaka Wahandisi na watu IT wote watashiriki kwenye huu mradi utafungua Bandari yetu ya Tanga na kuwa busy hii itachangia uchumi wa Tanga na maeneo ya jirani ambapo tutapata fedha na kujenga Reli ya kuunganisha Tanga na Mikoa ya kaskakzini mpka Uganda, Rwanda na Burundi na hii mipango yote Serikali imefanya chini ya miezi 6 tangu kuingia madarakani!
Hii ni rekodi hata zilizoendelea haziwezi kutekeleza mambo kwa haraka na kwa kasi kama hii yetu!
 
Jitahidini kumuelewa rais anaposema nchi hii ni tajiri..watanzania wengi walikuwa gizani na kudhani nchi ilivyokuwa ikienda ndiyo ilitakiwa iende vile..kwa maana ya kuwa nchi ya misaada, rasilimali kuu kushikiliwa na wageni, viongozi na watumishi wengine kupaa kila siku kwa pesa za walipa kodi..ifike mahali watz mjiamini..nchi hii INA vyanzo vingi vya mapato sio kodi ya TRA tu, tuna gesi, mafuta, utalii na madini..hivi vyote vilikosa msingi mzuri wa usimamizi..now we start the new beginning..tunatakiwa kuwa donor country.. Tuondoe hiyo mentality ya kuamini kuwa bila misaada nchi haiendi kwa sababu Tanzania haikuumbwa kuwa nchi ya kusaidiwa..
 
Hizo arrears mpaka leo?

Ni dhahiri kodi itapungua lakini bado itakuwa kubwa kuliko ile ya awamu ya nne. Pia ukumbuke kukusasnya ni jambo moja na kutumia ni jambo lingine kabisa. Matumizi ya kipuuzi kwa kiasi kikubwa yameondolewa na maana yake ni kwamba fedha inaelekezwa kwenye matumizi ya kusaidia wananchi na kuweka mazingira ya watu kujitegemea.

Wizi wa mchana kweupe umepigwa stop japo hauwezi kuishia kabisa. Muda ambao Magufuli kakaa madarakani awamu ya nne wangekuwa wametumia kiasi gani kwenye uzururaji nchi za nje?
 
Back
Top Bottom