Tunajiandaa kusherehekea nini miaka 50 ya uhuru? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunajiandaa kusherehekea nini miaka 50 ya uhuru?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MPIGA ZEZE, May 21, 2011.

 1. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  Ukisoma tahariri ya gazeti la Nipashe (May 19, 2011) iliyobeba swali la “Aibu hii ya ukosefu madawati hadi lini?” kama kweli una moyo wa binadamu utasikia machozi yanakububujika kama sio kwa nje, basi ni kwa ndani. Tahariri inajadili kwa kina na kutumia mifano halisi kama mojawapo ya shule ya jijini Dar kwamba “Watoto wa Kitanzania 2,346 wananolewa bongo zao katika shule hiyo, yenye wavulana 1,135 na wasichana 1,211. Idadi halisi ya wanafunzi wanaokalia madawati machache 200 yaliyopo huku kukiwa na upungufu mkubwa wa madawati 578. Kwa maelezo mengine ni asilimia 38.8 tu ya wanafunzi wote wanaokalia madawati, ambayo hata hivyo si madawati bora kwa maana halisi ya ubora.” Niliisoma nikabubujikwa na machozi. Nilibubujikwa na machozi kwa sababu siku chache kabla ya hapo niliishakutana na picha katika blogu ya Father Kidevu (mrokim.blospot) iliyokuwa ikionesha darasa la shule moja ya msingi jijini Dar likiwa na watoto waliobanana katika madawati machache yaliyomo na wengine wakiwa wamekaa sakafuni!!! Kwa hakika nilijiuliza 'ninasikia kelele nyingi za miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika – je tunafurahia nini?
  tanzania miaka 50 ya uhuru 2011.jpg

  Hoja: kwa nini tusiishinikize serikali kutumia theluthi mbili ya mabilioni walioyatenga kwa ajili ya ‘kuserebukia’ miaka 50 ya uhuru ikatumika kununulia madawati ya watoto wa shule za msingi kama njia sahihi ya kusherehekea uhuru wa Tanganyika? Kauli mbiu iwe “Kila mtoto wa shule ya msingi akalie dawati”.
   
 2. T

  T.K JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 345
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Halafu mtu anasimama jukwaani anaahidi eti kila mwanafunzi atapatiwa Laptop na watu wenye akili wanamshangilia!.....haina maana kufanya bethdei ya marehemu, hiyo Tanganyika ni marehemu tulishaizika bora hata wanzanzibari wanayo zanzibar yao, so ni upuuzi tu kusherekea nchi ambayo haipo
   
Loading...