Tunaipeleka wapi elimu yetu ya Msingi Tanzania?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunaipeleka wapi elimu yetu ya Msingi Tanzania??

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Daady, Sep 20, 2012.

 1. D

  Daady Member

  #1
  Sep 20, 2012
  Joined: Jul 22, 2010
  Messages: 66
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  1. Kwa mara ya kwanza Tanzania ( na kwa kuweka historia) wanafunzi wa darasa la saba wafanya mitihani
  kwa kujibu majibu yaliyo sahihi tuuu ( tofauti na miaka ya nyuma).
  Je hii ina maana kuwa waalimu au wasahihishaji wetu wamechoka kusoma majibu ya kujielezea?

  Je hii ina maana watoto wetu wanaomaliza elimu ya msingi hawajui kujielezea hivyo kurahisishiwa kwa kuwekewa
  majibu ya kuchagua ( hata kwa masomo kama hesabu n.k.)?

  Je kwa mtindo huu mpya ( ambao serikali inauita ''technolojia mpya ya ujazaji wa majibu'') hatuoni tutawachukua
  wanaostahili na wasiostahili pamoja? maana tutapimaje kiwango cha elimu kwa kutumia ''multiple choice questions''
  ambayo mtu anaweza kufumba macho na akapatia jibu?

  MY TAKE: HUU NI UVIVU WA KUFIKIRI WA VIONGOZI WASIO MAKINI.

  2. NAIBU WAZIRI WA ELIMU ( kwa macho yake MWENYEWE) ameshuhudia wanafunzi wawili kati ya 35 wa darasa la saba wanaofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi katika shule moja mjini Bagamoyo kuwa HAWAJUI KUSOMA WALA KUANDIKA!!!


  Je ni hatua zipi amechukua zipi amechukua baada ya kuona hiyo hali hapo shuleni?

  Who is to blame??? Nani wakulaumiwa jamani??? Mtoto mwenyewe, waalimu wake au wazazi/walezi wake, viongozi wa serikali???

  THIS ONLY HAPPEN TO A SILLY GOVERNMENT.
  VIONGOZI WAVIVU WA KUFIKIRI HUZAA SERIKALI DHAIFU.
   
 2. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,975
  Likes Received: 1,869
  Trophy Points: 280
  hatuna haja ya kuumiza vichwa mkuu. napata picha kwamba tumeuzwa na hizi ni condition za waliotununua. wanataka kuja kututawala upya sasa wanadumaza elimu ili warudi wakiwa vifua mbele.
   
 3. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Nani alikwambia kigezo cha kupima akili yako ni mtihani tu? au ulikua Unategeneza straight A's ukajiona umewin?
   
 4. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ukweli unajulikana kuwa hakuna familia, jamii, nchi, taifa au bara lililowahi kupiga hatua bila kuwekeza na kufanya mapinduzi ya kielimu.
  Na tukumbuke kuwa hakuna (at the ground level) familia ambayo imewahi kufilisika kwa kuwekeza katika elimu!

  Sasa Tanzania either kwa ujinga wa aslili ambao hata pale Mwalimu Nyerere alipojitahidi aliishia 'kuteka maji kwenye tenga' au kwa makusudi tumeshindwa kuuona ukweli huu.

  Ni ujinga ulio mkuu kabisa kabisa viumbe asili ya binadamu wanaoishi katika karne ya 21 kutenga 1.3% (??) tu ya bajeti yake kwenye elimu wakati huo huo likitenga Sh Billion 10 kwa ajili ya matibabu tu wa viongozi wa juu wastaafu.

  Hata uandike na kueleza kurasa laki moja za tatizo hilo hutabadili lolote zaidi ya ukweli huu.
   
 5. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,975
  Likes Received: 1,869
  Trophy Points: 280
  kwani wafikir kipimo cha haraka cha kutuonyesha kwamba mwanafunzi yuko competent katika jambo fulan kielimu ni nini?
  usemapo kipimo sio mtihani tu nakushangaa, hivi utawezaje kupewa storrey building ujenge kama huwez kutafuta deflection angle? ama utapewaje mtungi wa kuchanganya bia pasi kujua namna ya kutafuta shear force? utajuaje kutengeneza maziwa mtindi ambayo yana quality kama usipoweza kufanya microbial analysis and colony counting? sasa je haya yote ujifunzie kwenye kazi ama darasani? n huku darasani tukupime kwa kutumia nini? na tukugrade kwa grade gani?
   
 6. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Wanofanya hayo yote uliyoyataja ni students waliokuwa na average pass marks, na waliotahiniwa kwa namna mbali mbali sio mtihani peke
   
 7. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,975
  Likes Received: 1,869
  Trophy Points: 280
  what do you mean by average passmark Watu? do you want to tell me wote wenye gpa za 5 sio bora? na kwamba hawawez kudeliver kazini?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Yap, wengi niliokuwa nao shule wa hivyo siwaoni wakideliver in life pamoja na elimu zao, wengi wako kwenye quadrant ya kutumwa(ajiriwa) - ref: cash flow quadrant
   
 9. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,975
  Likes Received: 1,869
  Trophy Points: 280
  wewe kudeliver unakuweka katika mtazamo upi? wa kujiajiri ama wa kuajiriwa peke yake? je wataka kuniambia mathalan am a microbiologist, where should i practice it kama sio lab? na je pale nitatakiwa kudeliver ama vipi? manake nijuavyo mimi i have to perform my lab experiments at my clients perfection tena kwa kufollow recommended standards sasa hapo wewe utaniambiaje?

  what i know mtu anaweza kudeliver vizuri sehem yyte ya kazi provided kwamba anajua anachokifanya na yuko competent nacho iwe amejiajiri ama ameajiriwa. Na hapo performance yake itapiwa kwa ubora wa kazi yake sasa usione kwakua wewe umejiajiri labda kwasababu fani yako inakuruhusu basi walioajiriwa hawadelivi simply kwasababu wameajiriwa.

  ungejitetea labda wapo watu ambao wamefaulu vzr sana darasan lakni kwenye ajira wanashindwa kabisa kuonyesha uwezo wao hilo ningekuelewa.
   
 10. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  and the argument here, is 'exams' kama ndio kipimo peke cha kujua uelewi wa mtu?
   
 11. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #11
  Sep 21, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kuna nchi nyingine pia zinazotumia mfumo huu.Kwahiyo Tanzania siyo nchi ya kwanza.Kupata jibu sahihi kwa kiasi fulani mpaka uwe na idea ya concept.Kama ni guess work huwezi kuguess kiviiile.
   
 12. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,643
  Likes Received: 1,433
  Trophy Points: 280
  No wonder tuna njuka wasiojua soma wala kuandika... kwa style hii ukijua kupiga chabo tu unapass with distinctions tena unaenda vipaji maalumu kabisa

  Manina walahi naskia mpaka hesabu multiple choice siku hizi.. enzi zetu tulikua tunapiga swali,kazi jawabu
   
 13. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #13
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  MKuu kama nime elewa vizuri ni kwamba utaratibu wa kusahihisha umekua computerized. Sio rahisi computer kusoma maelezo na kweza ku-mark.

  Watahiniwa wa darasa la saba ni wengi kiasi cha kufanya zoezi la usahihishaji kuwa gumu na kuchukua muda mrefu. Na huu ni utaratibu unaotumika nchi nyingi duniani. Tuseme Tanzania wamechelewa sana kuanza huu utaratibu.

  Mitihani ya certification za Microsoft, Cisco na mingineyo mingi duniani ni multiple choice. Na mitihani hii inaheshimika duniani kote. HIvyo sioni kama kufanya multiple choice mitihani wa darasa la saba uta-comprimise ubora kiasi hicho.

  Isitoshe atakaefaulu kwa kubahatisha ataangukia pua form two ambapo. Mitihani iko mingi ya kutosha kuchuja vya kutosha.

  By the way, hivi kweli unadhani wasahihishaji wa wizara walikua wanafuatisha njia wakati wa kusahihisha hesabu? Kama sikosei, kila swali moja la hesabu lina alama moja. Sasa akifuatisha njia ndo ili atoa alama ngapi? Huwa katika swali ama mtu anapata 1 au 0, kwa mantiki hiyo hakuna alama za njia.
   
 14. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #14
  Sep 21, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  we like simple tasks, that is it!?
   
 15. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #15
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu ukisoma vitabu vya Robert T. Kiyosaki uvisome kwa umakini kidogo maana kuna contents ambazo zina apply kwao tu. Mfano anaposema Nyumba USA sio assert, utasema na Tanzania nyumba sio assert? Ukumbuke kule kwao bei za nyumba zina flactuate lakini hapa kwetu zina appreciate kila kukicha.

  Haya sasa, kama ujanja ni kumiliki biashara yako mwenyewe, niambie utakua una ajiri kwa vigezo gani? Kama hutatumia hivyo vyeti vya shule please let me know altenative method unayotumia.
   
 16. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #16
  Sep 22, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  I take those who have failed in exams and teach them to do what i want, they perform wonders .....
   
 17. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #17
  Sep 22, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,738
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Moja ya malengo ya Elimu ya Msingi ni mwanafunzi kuweza kusoma na kuandika Kiingereza na Kiswahili. Je mfumo huu wa maswali unapima vitu hivyo?
  Kwa kuzingatia vigezo vya kutunga maswali mafupi (objective questions), mitihani ya kuhitimu Elimu ya Msingi haikidhi vigezo.
   
Loading...