Tunahoji kuhusu vyeti hadi imekua kero

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
32,239
50,412
Hehehehe!! Afrika Mashariki viongozi wanafuatwa kwa mambo ya vyeti vyeti, hakuna anayehoji kazi inafanyika vipi au uwezo wa mhusika/kiongozi kufanya kazi, imekua vyeti vyeti. Kule Tanzania wamemsakama mkuu wa mkoa wa Dar kuhusu vyeti na majina.

Huku Kenya tumekua na mijadala ya mambo ya vyeti vya wanasiasa kwa muda wa miaka mitano sasa, tulianza na Kabogo wa Kiambu. Leo hii naona tumeishia kumfuata kiongozi wa Mombasa kwa hilo hilo la vyeti.

Hivi, mbona hatuhoji utenda kazi, hamna mtu anayefuata matokeo ya hawa viongozi. Wamefaulu kuthibitisha kwamba elimu bora sio kigezo cha uongozi bora maana wamefaulu kutenda na kuboresha mikoa/maeneo yao ya uongozi. Kenya ilishapitishwa kwamba lazima uwe na shahada ili uruhusiwe kuwa kiongozi, sasa jamaa wamepambana kweli kusaka vyeti hata kwenye vyuo vya ovyo kitaa ilmradi tu awe na cheti.
 
And your point is????
 
mfano hapa kwetu Bongo land vyeti haikuwa big issue kivile sema walioanzisha hili saga wao wamekataakuhakikiwa ili hali title za elimu zao zina mashaka sikigodo mpaka kunawalio leta usahhidi lakini wao wakagoma katakata,alafukumbuka kunawaliopatikana na hatia kuwa na vyeti vya kughushi walifukuzwa kazi na wengine kushatakiwa sasa watu wanahoji kwanini haki iwe ya upande mmoja tu wa shilingi...!!!siamini kama vyeti ni issue sana kushinda utendaji ila napingana sana ulaghai katika taaluma
 
Lakini hapo Bongo mlifaa aidha mpeleke issue mahakamani, lakini sio kuongea kwenye mitandao na makanisani. Maana hadi sasa hakuna aliyehoji kwa kutumia njia muafaka ili mtuhumiwa ajitetee ipasavyo. Sasa mnamkwamisha jamaa katika utendaji kazi wake, kila siku vyeti vyeti hakuna anayemskliza hata akiongea kuhusu uzinduzi wa barabara.

Ndio taswira kule kwa gavana wa Mombasa, ambaye amefanya mengi ya kutajika lakini jamaa wamechimba hadi alikosomea sekondari.
 
kuna mdau aliye peleka kesi mahakamani anaitwa Meya Jacob wa Kinondoni baada yakuona mamlaka za uteuzi wa bwana yule ziko kimya na alitamka wazi kuwa yeye hapangiwi cha kufanya ukizingatia ndio number moja citizen hapa kwetu,huko kwingine tuliko pita tumetumia kama majukwaa ya kupaza sauti zetu ili wenye mamlaka wachukue hatua,we siumeona jamaa ikabidi akimbilie nayeye kanisani na makamera kilaupanda kwenda kulia lakini hakuna pata huruma aliyo ikusudia..
Sasa unapozungumzia kumkwamisha je wale waliofukuzwa kazi kwa kosa kama lake tuwaweke kundi gani??kingine unapokaa ofisi ya umma tuhuma pekee zinakufanya upishe ofisi ili uchunguzi ufanyike hata kabla ya kufikishwa mahakamani
 
Lakini mahakama ni mhimili tofauti, hivyo huyo asiyepangiwa hana uwezo wa kuwapangia mahakimu. Hivyo mngekomaa na mahakama badala ya kumpigia jamaa haya makelele yote.
 
ndio mazuri sasa hayo kushinda ya mahakama,siunajua sisi wabongo tukiamua kukusimanga utaona afadhali tungekupa sumu ufe...!!!tayari kuna mwananchi kashafungua kesi mahakamani
 
Ukiuliza maprofesa na madaktari Waafrika wamefanya nini cha maana hamna pamoja na mivyeti yao mingi. Hamna utafiti wa maana unaofanywa na hao Waafrika wanaojiita wasomi. Mgonjwa akipatwa na changamoto ndogo Afrika mbio anapelekwa India, halafu bado tunajiita wasomi.
Elimu ya magharibi haijatusaidia Waafrika kwa lolote zaidi ya kuleta ubaguzi mkubwa katika jamii yetu.
 
Back
Top Bottom