Tunahitaji rais mwenye sifa zaidi ya utendaji na usimamizi...

Tunahitaji rais mwenye sifa zaidi ya utendaji na usimamizi...

Mkono

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2010
Posts
568
Reaction score
89
Moja ya changomoto ninayoiona katika uchaguzi wa mwaka huu ni pale watanzania baadhi kutumia kigezo cha kutokuwa fisadi na uchapakazi kama sababu pekee za kumpata rais tunayemtaka katika awamu hii ya tano bila kujua kuwa dunia ya sasa imebadilika sana na bila kuwa na rais mbunifu kulingana na mfumo wa uchumi wa dunia unavyoenda huko mbele tutalaumiana! Vyovyote iwavyo rais wa sasa atatoka ktk moja ya makundi haya mawili kama si UKAWA basi ni CCM na katika shaka yangu hii haimuhusu sana mgombea wa UKAWA ndg Edward Lowasa maana walau rekodi zake huko nyuma zinaonyesha uthubutu wake katika eneo hilo kuanzia tofauti na mwenzake Magufuri ambaye wafuasi wake wengi wamejikita katika eneo moja tu la utendaji.

Nakubaliana na mtazamo huo ila kwangu natamani sana watanzania waende mbali zaidi hasa kwa kutazama dunia ya sasa inavyokwenda kasi sana katika mlengo wa utandawazi,nafikiri ukichambua ufisadi uliofanyika katika utawala wa rais Mkapa ni mkubwa pengine kuliko wa serikali ya rais wa sasa Bwana JK ila watanzania walio wengi wanatamani maisha ya enzi zile za rais Mkapa kuliko JK na hii ni kutokana serikali ya rais Mkapa ilijaribu kuumiza kichwa kuona ni jinsi gani anaweza kufufua uchumi wa nchi kwa kufanya mapinduzi katika sekta za madini,mabenki ,mawasiliano nk.japo kuwa maamuzi mengi hayakuzingatia maslahi ya umma japo nia ilikuwa njema! Nani atabisha kuwa ni katika kipindi cha serikali ya Mkapa wawekezaji wengi tulionao kuanzia celtel hadi Barick walipatikana kipindi chake tofauti na mwenzie ambaye hakuna jipya zaidi katika sekta ya uiwekezaji zaidi kufisadi mamilioni ya shilingi yaliypatikana kutokana na juhudi za mwenzake hata pale alipojitutumua kutoka nje ya nchi kuwatafuta wawekezaji tuliishia kuona picha na akina J-ZAY na Beckam ambao hakuna hatua waliyoichukua kuchangia ukuaji wa uchumi wetu.

Leo tuna mawazari waliojipambanua kama wapinga ufisadi na wachapa kazi kama Dr Mwakyembe lakini tujiulize nafasi walizopatiwa tija gani imepatikana? Ni Dr Mwakyembe huyu huyu aliyekabidhiwa wizara ya uchukuzi na mawasiliano akabaki kulia lia na watumishi washirika la letu la ndege bila kuja na njia mbadala ya kulifufua shirika na kibaya zaidi ameshindwa hata kubadili mtazamo wa kifikra kwa watanzania juu ya usafiri wa anga! inawezekanaje kampuni binafsi ifanye mapinduzi katika sekta kama hiyo na waziri ashindwe?

Tunaweza kuangalia kazi iliyofanywa na FASTJET ndani kipindi kifupi kwa kubadilisha mtazamo tu wa raia katika usafiri wa ndege ktk nchi hii leo si jambo la kushangaza mtu wa wakawaida kukwambia ameshuka na ndege Songwe ,Mwanza ,Arusha nk jambo ambalo kipindi cha nyuma ilionekana kama ajabu leo watu wanaominisha watanzania kuwa ni wachapa kazi wanapewa fursa kuonyesha vipaji vyao wanaishia kufukuza wafanyakazi na kuingiza serikali ktk gharama za kulipa fidia.

Ni Dr Mwakyembe huyu huyu ambaye ambaye baada ya kukabidhiwa wizara badala ya kufikiri ni jinsi gani anavyoweza kufanya mapinduzi katika bandari na kutengeneza mazingira ya kuongeza wateja na ajira kwa watanzania akaishia kuwafukuza watumishi huku serikali ikisubiri muda wowote kulipa fidia itakapo kuwa imeshindwa kesi na kibaya zaidi hakumkumshutua rais JK kama bosi wake juu ya athari za wake na rais Kagame tukaruhusu mgogoro na Rwanda ambao mwenzake rais Uhuru akautumia kwa manufaa ya kuendeleza uchumi wa taifa lake kwa kuimarisha mahusiono na wateja wetu katika bandari yao ya Mombasa kwa kuhamisha shughuli za upokeaji wa mizigo katika bandari yetu ya Dar es salaam hadi Kenye Mombasa

Najaribu kutumia mfano wa Dr Mwakyembe kwa sababu kimtazomo huyu mtu simtofautishi sana na mgombea urais wa CCM Dr Pombe Magufuri na pengine Dr Mwakyembe anaweza akawa na unafuu kuliko mwenzie hasa linapokuja suala la mahusiano nje mipaka ya Tanzania maana nahisi Dr MAGUFURI mtu muhimu anayefahamiana naye nje ya nchi sidhani kama ni zaidi ya Raila Odinga! Ni vigumu na sioni na wala sitarajii kumuona Mgufuri akija na mkakati mpya wa kimapinduzi katika kufufua Uchumi wa nchi na bahati mbaya sana Magufuri namuona kama {M-conservative} flani anayejificha katika kichaka cha uchapakazi na inatokea anakuwa rais ni lazima watanzania wajiandae kuishi maisha taabu sana kwa kipindi chake maana atajikita katika kubana kila kona ili kuongeza pato la taifa bila kuchungulia fursa toka nje.

Katika siasa za Kenya Uhuru alionekana kama" mshikaji" sana na hakuwa msafi kihivyo mtakumbuka tuhuma za kujilimbikizia ardhi kubwa na kumiliki viwanda vingi vikiwemo vya maziwa ni tuhuma zilizo msumbua sana japo wakenya walifumbia macho na kuziba masikio na kuamua kumchagua leo tunaona ndugu zetu wakenya walifanya uchaguzi sahihi kwa jinsi uchumi wa taifa hilo unavyozidi kuimarika pamoja na changamoto za usalama nk.Mwaka jana kama sio juzi rais wa China alifanya ziara yenye mbwebwe kibao hapa nchini ikiambatana na taarifa za kusaini mikataba 17 kama sehemu ya uwekezaji hapa nchini ,baada ya ziara hiyo rais Uhuru yeye akafunga safari hadi huko China nakufanikiwa kuishawishi serikali ya china kufadhili miradi kadhaa ikiwemo ujenzi wa reli ,miradi hiyo kwa Kenya tayari imeanza huku kwetu miradi yote 17 hakuna hata mmoja ulioanza! Hii maana yake nini? Kwamba rais Uhuru hakuishia kwenye kushangilia mikataba alienda mbele zaidi kuhakikisha anatengeneza mazingira ya taasisi za fedha za China zinatoa fedha kwa ajili ya miradi hiyo wakati hapa kwetu ikiwa haijulikani itaanza lini na rais ajaye ataanza na kipaumbele gani? Mtwara corridor ,Bagamoyo Corridor,North Corridor au Like Victoria Corridor?

Mtu mwingine anaweza kuhoji mbona rais Kagame ameweza? Pamoja na sifa nzuri ya usimamizi pamoja na uchapakazi kwa rais Kagame anajiongezea sifa nyingine ambayo mgombea wa CCM hana ''kujiongeza'' inaweza isionekane kama sifa nzuri kwa taifa lililokulia katika misingi ya UJAMAA ila ni lazima tukumbuke dunia ya ujamaa haipo tena ni Zitto tu anayejaribu kuihubiri huku yeye akijua anahubiri asichotenda,Uchumi wa taifa la Rwanda umejengwa na nguvu ya Wanyarwanda wenyewe kwa kufanya kazi kwa bidii ila zaidi umejengwa kwa gharama ya raslimari za watu wa DRC kupitia mgogoro alioutengeneza makusudi rais Kagame,sidhani na sitegemei kama Dr Magufuli anaweza kuruhusu mawazo ya namna hiyo katika serikali yake zaidi ya kutafuta sifa za kupeleka jeshi letu kupambana DRC kwa gharama za Watanzania wenyewe kama alivyofanya Nyerere na harakati za ukombozi huko nchi za kusini mwa Afrika.
 
mkuu Mkono,shukrani sana kwa uchambuzi uliokwenda shule kama huu. Maana sisi tangu tuingie kwenye harakati za kampeni,mtizamo wetu umeishia kumtambua fisadi na asiye fisadi ilihali mambo muhimu baada ya uchaguzi tunashindwa kujua kama taifa. Bado tunaaminishana kuhusu ufisadi lakini mwisho wa siku akishachaguliwa huyo msafi, anaishia kuzindua miradi ya ufugaji kuku kwa maandalizi ya gharama kubwa kuliko miradi yenyewe halafu tunaweka kwenye rekodi kufanyia reference kipindi kijacho cha uchaguzi.
Kwa mtizamo wangu,tulitegemea kama wagombea wameshindwa kujiainisha katika eneo la ukuzaji uchumi kwa vitendo kulingana na atmosphere yenyewe,basi nafasi hiyo ichukuliwe na wasomi kulielezea hilo kwa maana pana zaidi kwa maslahi ya taifa. Kuna watu wamezaliwa kuongoza na kuna wengine ni watekelezaji kiasili. Nafasi ya kuongoza inaenda kwa lowasa na magufuli anafaa kwa upande huu wa pili. Ndio maana napendekeza serikali ijayo ya ukawa imtumie magufuli katika utekelezaji na lowasa abaki ofisini kuwa mbunifu maana eneo hili ndilo anafaa zaidi.

PEOPLES.
 
Sifa kuu ya rais awe mtendaji na msimamizi zaidi ya hapo labda awe mwizi kama lowassa
 
Back
Top Bottom