Tunahitaji Rais mwanadiplomasia haraka

Tunahitaji Rais mwanadiplomasia haraka

Joined
Oct 5, 2015
Posts
90
Reaction score
483
TUNAHITAJI RAIS MWANADIPLOMASIA HARAKA.

Tundu Lissu/Augustine Mahiga/Benard Membe/Dr. Wilbroad Slaa

Viongozi wa kundi la nchi na jumuia za kimataifa zinazounda kundi la G20 (Governments of 20) wanafanya mkutano wao mjini Buenos Aires, Argentina. Agenda mbalimbali zitajadiliwa lakini ajenda kuu ni kazi na ajira, maendeleo ya miundombinu na hali ya upatikanaji wa chakula duniani kwa sasa na baadae.

Hata hivyo, ajenda hizo kuu zinaweza kuwekewa kivuli na ajenda nyingine ndogondogo.

Kuna vita ya kibiashara baina ya China na Marekani, mataifa mawili makubwa kiuchumi duniani. China Marekani wapo katika vita baridi ya kibiashara, kila mmoja akipandisha kodi ya bidhaa zinazoingia nchini kwake kutokea upande mwengine.

Vita hii inakolezwa zaidi na vuguvugu la kugombania mipaka katiba bahari ya China kusini. China inaamini sehemu ya eneo la bahari ya China kusini, ni eneo lake, na tayari wamejenga visiwa (artificial islands) na kuweka kambi za jeshi. Inaarifiwa kwamba China inajenga vituo vya kijeshi chini ya bahari katika eneo hilo.

Eneo la bahari ya China kusini linahodhi asilimia 30 ya biashara zinazotumia bahari duniani, na asilimia 60 ya biashara za China. Sehemu kubwa ya usalama wa kiuchumi (Economic Security) wa China unategemea eneo la bahari ya China kusini.

Marekani kwa upande wake inadai eneo hilo ni la kimataifa na kila taifa lina haki ya kulitumia kwa usafiri bila kuingiliwa. Mataifa ya Phillipine Vietnam, Indonesia, Malaysia, Brunei na visiwa vya Taiwan, nawo wanapambana kumiliki sehemu ya eneo hilo. Marekani imekuwa ikituma meli zake za kivita kupita eneo hilo katika kile kinachoitwa 'Uhuru wa safari za majini". Vitendo ambavyo China inachukulia kama uchokozi.

Eneo la bahari ya China kusini linatumiwa na meli nyingi za kimataifa kwa biashara inayokadiriwa kuwa na thamani ya dola trilioni 5.3 kwa mwaka.

Ajenda nyingine inayotazamiwa na wafuatiliaji wengi ni kuhusu mauaji ya mwandishi wa habari wa Saudi Arabia, na mkosoaji maarufu wa ufalme wa Saudia, Bwana Jamal Khashogi.

Khashogi aliyekuwa akiishi uhamishoni, huko mjini Washington, Marekani aliuawa na maafisa wa shirika la kijasusi la Saudi Arabia ndani ya ubalozi wa nchi hiyo uliyopo mjini Instanbul, Uturuki. Taarifa za vyombo vya usalama vya Uturuki na zile za Shirika la kijasusi la Marekani, CIA zinamtaja Mwana Mfalme wa Saudia, Mohammed Bin Salman (MBS) kuwa ndiye aliyeagiza mauaji hayo.

Mauaji ya Khashogi yametikisa mahusiano ya nchi za Magharibi na Saudi Arabia kiasi kwamba baraza la maseneta la Marekani (Senate) limepiga kura ya kuamua kuacha kuisaidia Saudi Arabia katika vita inayoendelea huko Yemen.

Mjini Washington, maofisa wa serikali ya mji huo wamepiga kura kubadili jina la mtaa ulipo ubalozi wa Saudia Arabia, na kuitwa Mtaa wa Jamal Khashogi. Lengo ni kuwakumbusha watu kila siku kuhusu unyama wa Saudia. Kikao cha halmashauri ya mji kinasubiriwa kukubali au kukataa mpango huo.

Hata hivyo, Rais Donald Trump ameonesha nia ya kuendeleza kufanya biashara kati ya Marekani na Saudia. Biashara hiyo yenye thamani ya Dola bilioni 110 (Tsh. Trilioni 250) inatengeza ajira 17000 kwa vijana wa Marekani, faida ambayo Donald Trump hataki kuikosa. Huko barani Ulaya, viongozi wa mataifa mbalimbali wamelaani mauaji ya Khashogi, na kutaka uchunguzi wa wazi na huru kisha wahusika wachukuliwe hatua.

Waziri mkuu wa Uingereza, Bi. Theresa May amerudia kueleza msimamo huo alipohojiwa na waandishi wa habari huko mjini Buenos Aires. Tukio la mauaji ya Jamal Khashogi limeharibu mahusiano ya Saudi Arabia na nchi za Magharibi, na zaidi linatishia nafasi ya mwanamfalme Mohammed Bin Salman ya kurithi ufalme wa Saudia.

Ajenda nyingine nzito ni kuhusu tukio la Meli tatu za kivita za Ukraine kudhibitiwa na majeshi ya majini ya Urusi huko katika bahari ya Azov inayotenganisha ardhi ya kusini mwaka Urusi na Ukraine. Novemba 25, mwaka huu, meli tatu za kivita, mali ya Ukraine zilikuwa zikivuka kutoka bahari nyeusi kuingia bahari ya Azov kupitia mlango bahari wa Kerch. Mlango wa Kerch ni mahala pembamba sana, ni mlango unaounganisha bahari nyeusi (the black sea) na bahari ya Azov, na kutenganisha ardhi ya Urusi na Peninsula ya Crimea

Meli zinapopita eneo hilo, sharti ziruhusiwa na jeshi la maji la Urusi kwa ishara maalum baada ya kuwasiliana. Lakini kwa tukio la Novemba 25, Urusi wanadai kwamba Meli hizo hazikutoa taarifa, na hivyo ikatafsiriwa kama uvamizi. Baada ya kudhibiti Meli hizo, mataifa ya magharibi yamekuja juu kwa ukali, na Donald Trump ameamua kufuta mkutano wake na Rais wa Urusi, Vladimir Putin uliopangwa kufanyika huko Buenos Aires, kunakoendelea mkutano wa G20.

Nchini Ukraine, baada ya tukio hilo, Rais wa nchi hiyo Bwana Petro Poroshenko ametangaza hali ya hatari, na sheria za kijeshi (martial law) kutumika kwa siku 30. Pia ameondoa ruhusa ya wanaume kuanzia miaka 16 hadi 60, raia wa Urusi kuingia nchini humo. Serikali ya Urusi inadai, Rais wa Ukraine Petro Poroshenko alitengeneza makusudi tukio hilo ili atangaze hali ya hatari kwa kisingizio cha kukwepa uchaguzi wa Rais Unaotarajiwa kufanyika Machi 2019.

Umaarufu wa Rais Poroshenko umeshuka hadi asilimia 7, hali inayoifanya akose nafasi ya kushinda. Katika kile kinachoonekana kuwa ni mpango wa makusudi, Poroshenko ameomba meli za kivita kutoka nchi za Magharibi, na kuomba Urusi wawekewe vikwazo zaidi vya kiuchumi. Urusi kwa upande wake wamewafikisha mahakamani, wanajeshi waliokuwa ndani ya meli hizo za Ukraine.

Viongozi wa magharibi wameilaumu Urusi kwa tukio hilo, lakini wanadiplomasia huru wanaona kwa huo ni mpango wa makusudi wa Ukraine kutumiwa na mataifa ya Magharibi dhidi ya Urusi. Isipokuwa kwa Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel ambaye amedai uchunguzi zaidi kabla ya kuilaumu Urusi.

Angela Merkel pia amepinga wazo la kuiwekea Urusi vikwazo zaidi.
Bila shaka kutakuwa na ajenda nyingine ndogo ndogo, tukio la mauaji ya Jamal Khashogi, Mgogoro wa Urusi na Ukraine pamoja na vita ya kibiashara ya Marekani na China na Mgogoro wa mipaka ya bahari ya chuma kusini ni ajenda nzito, zinazoendelea hata baada ya mkutano.

Viongozi wa nchi mbali mbali wamehudhuria mkutano wa G20, wapo viongozi wa serikali za nchi zinazounda G20 na wengine walioalikwa. Nchi na serikali zinazounda kundi la G20 ni Argentina, Australia, Brazil, Canada, China, Umoja wa Ulaya, Ufaransa, Ujerumani, India, Indonesia, Italy, Japan, Mexico, Urusi, Saudi Arabia, Afrika Kusini , Korea kusini, Uturuki, Uingereza na Marekani.

Viongozi wa Afrika waliohudhuria ni pamoja na Cyril Ramaphosa, Rais wa Afrika kusini, kama mwanachama wa G20, Paul Kagame, Rais wa Rwanda na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Rais Macky Sall wa Senegal ambaye ni mwenyekiti wa mpango wa maendeleo wa Afrika (NEPAD).

Tanzania na Diplomasia ya kimataifa.

Ajenda nilizoweka hapo juu, ambazo nyingi zinahusu migogoro kati ya mataifa makubwa, ni ajenda ambazo Taifa lolote duniani linaloshirikiana na mataifa yanayohusika katika migogoro hiyo, linapaswa kuzijua, kuzichunguza, na kuzitathimini, ili kuwa na taarifa za uhakika zinatakazosaidia maamuzi sahihi katika mashirikiano yake na mataifa hayo. Tanzania inashirikiana na Marekani, China, Urusi, Saudi Arabia, Uturuki na mataifa ya Ulaya mgharibi (Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, nk). Ni lazima, kuwa na kiongozi anayejua kucheza michezo ya kidiplomasia.

Kiongozi mwenye utambuzi wa masuala ya kimataifa, ambaye atazungumza lugha ya kidiplomasia bila kuhatarisha mahusiano yetu na mataifa hayo, lakini bila kwenda kinyume na misingi ya kusimamia haki na usawa ulimwenguni kote, kama ilivyowekwa na Baba wa Taifa, Mwl Julius K. Nyerere.
Bila kupepesa macho, Rais aliyepo madarakani, hana uwezo wa kidiplomasia, achilia mbali utayari wake. Kauli zake na matendo yake katika mambo yanayogusa mahusiano ya kimataifa ni dhahiri kwamba, yupo nje ya ulingo wa tasnia hiyo. Ni wakati wa kuanza kufikiri, pamoja na sifa zingine, umuhimu wa sifa ya uwezo wa kidiplomasia kama ilivyokuwa awali.
Diplomasia inataka akili na hekima kubwa, na ufikirifu wa hali ya juu, hasa kwa nyakati tunazoekea ambapo migogoro ya kimataifa inaweza kuongezeka maradufu.

Tayari kuna hisia za kuibuka kwa vita kuu ya Tatu ya dunia. Leo tunashuhudia majigambo ya vifaa vya kivita kati ya Urusi na Marekani, nchi ambazo tunashirikiana nazo. Mgogoro mkubwa wa kibiashara kati ya Uchina na Marekani, Nchi ambazo tunashirikiana nazo. Ikitokea nyakati za kuchagua upande, tutachagua wapi? Itategemea na ufahamu au ujinga wa kidiplomasia. Mashirikiano yetu na nchi mojawapo, yanaweza pia kuathiriwa na migogoro baina ya nchi hizo, ni vema kujua namna ya kucheza karata ili kuepuka matokeo hasi, kwetu na kwa vizazi vijavyo.

Rais aliyepo Madarakani, anapotoa kauli hadharani, zinazoonesha chuki dhidi ya mataifa tunayoshirikiana nayo katika mambo mengi, ni hatari. Mathalani, Rais Magufuli anapowasema vizuri Wachina, na kuwasema vibaya mataifa ya Magharibi, kwa sababu moja ya masharti ya mikopo au misaada, ni matokeo ya kukosa utashi wa kidiplomasia. Tanzania inashirikiana na mataifa ya Magharibi katika maeneo mengi; Elimu na Tafiti, Ulinzi na Usalama, Vita dhidi ya ugaidi nk. Rais mwanadiplomasia anapaswa kujua namna ya kuepuka migogoro zaidi badala ya kuikuza. Ndio dunia inavyoenda.

Ndio maana, pamoja na uhasimu wa Marekani na Urusi, lakini wanashirikiana katika teknolojia ya uchunguzi wa anga. Septemba mwaka 2017,Mashirika makubwa ya uchunguzi wa anga duniani, Roscosmos la Urusi na NASA la Marekani yalitia saini muendelezo wa ushirikiano katika kuchunguza anga za mbali. Mashirikiano ya kisayansi hayajaathiriwa na uhasimu wa kisiasa, kwa sababu ya utashi wa kidiplomasia.

Na ni vema kujua, lengo la utashi wa kidiplomasia sio kujifanya mnyonge, bali kuboresha ushirikiano. China inaihitaji Tanzania, Marekani inaihitaji Tanzania, Uturuki inaihitaji Tanzania, Urusi inaihitaji Tanzania, kwa faida zao, na Tanzania inazihitaji nchi hizo, kwa faida yake, katika maeneo tofauti tofauti. Hakuna nchi inaweza kusonga bila kushirikiana na nchi zingine.
Je! Mwaka 2020, tutahitaji Rais Mwenye utashi wa kidiplomasia?
 
I do not agree, hizi dhama zimebadirika, marais wa sasa wanalazimika kuwa manationalists who selects important international allies carefully & silently.
 
Alishapatikana 2005-2015 tukasema tunahitaji Rais Dikteta

Yaan kati ya Mvua Na Jua wengine wanasema bora Jua wengine bora Mvua

Mie nasema Rais Mwana diplomasia hafai Kwa Kuwa tunamchukulia Kama Fala bora tupate Hawa Hawa Makomando kipensi
 
Ha ha ha komando kipensi
 
Zile akili zinawaza Rais atakaye uwa vyama vya upinzani achilia mbali wapinzani wenyewe. Tuna safari ndefu mzee. ..!
 
Alishapatikana 2005-2015 tukasema tunahitaji Rais Dikteta

Yaan kati ya Mvua Na Jua wengine wanasema bora Jua wengine bora Mvua

Mie nasema Rais Mwana diplomasia hafai Kwa Kuwa tunamchukulia Kama Fala bora tupate Hawa Hawa Makomando kipensi
Kama ndo huu udikteta mlisema basi nyie wagonjwa
 
TUNAHITAJI RAIS MWANADIPLOMASIA HARAKA.

Tundu Lissu/Augustine Mahiga/Benard Membe/Dr. Wilbroad Slaa

Viongozi wa kundi la nchi na jumuia za kimataifa zinazounda kundi la G20 (Governments of 20) wanafanya mkutano wao mjini Buenos Aires, Argentina. Agenda mbalimbali zitajadiliwa lakini ajenda kuu ni kazi na ajira, maendeleo ya miundombinu na hali ya upatikanaji wa chakula duniani kwa sasa na baadae.
Hata hivyo, ajenda hizo kuu zinaweza kuwekewa kivuli na ajenda nyingine ndogondogo.
Kuna vita ya kibiashara baina ya China na Marekani, mataifa mawili makubwa kiuchumi duniani. China Marekani wapo katika vita baridi ya kibiashara, kila mmoja akipandisha kodi ya bidhaa zinazoingia nchini kwake kutokea upande mwengine. Vita hii inakolezwa zaidi na vuguvugu la kugombania mipaka katiba bahari ya China kusini. China inaamini sehemu ya eneo la bahari ya China kusini, ni eneo lake, na tayari wamejenga visiwa (artificial islands) na kuweka kambi za jeshi. Inaarifiwa kwamba China inajenga vituo vya kijeshi chini ya bahari katika eneo hilo. Eneo la bahari ya China kusini linahodhi asilimia 30 ya biashara zinazotumia bahari duniani, na asilimia 60 ya biashara za China. Sehemu kubwa ya usalama wa kiuchumi (Economic Security) wa China unategemea eneo la bahari ya China kusini.
Marekani kwa upande wake inadai eneo hilo ni la kimataifa na kila taifa lina haki ya kulitumia kwa usafiri bila kuingiliwa. Mataifa ya Phillipine Vietnam, Indonesia, Malaysia, Brunei na visiwa vya Taiwan, nawo wanapambana kumiliki sehemu ya eneo hilo. Marekani imekuwa ikituma meli zake za kivita kupita eneo hilo katika kile kinachoitwa 'Uhuru wa safari za majini". Vitendo ambavyo China inachukulia kama uchokozi.
Eneo la bahari ya China kusini linatumiwa na meli nyingi za kimataifa kwa biashara inayokadiriwa kuwa na thamani ya dola trilioni 5.3 kwa mwaka.
Ajenda nyingine inayotazamiwa na wafuatiliaji wengi ni kuhusu mauaji ya mwandishi wa habari wa Saudi Arabia, na mkosoaji maarufu wa ufalme wa Saudia, Bwana Jamal Khashogi.
Khashogi aliyekuwa akiishi uhamishoni, huko mjini Washington, Marekani aliuawa na maafisa wa shirika la kijasusi la Saudi Arabia ndani ya ubalozi wa nchi hiyo uliyopo mjini Instanbul, Uturuki. Taarifa za vyombo vya usalama vya Uturuki na zile za Shirika la kijasusi la Marekani, CIA zinamtaja Mwana Mfalme wa Saudia, Mohammed Bin Salman (MBS) kuwa ndiye aliyeagiza mauaji hayo. Mauaji ya Khashogi yametikisa mahusiano ya nchi za Magharibi na Saudi Arabia kiasi kwamba baraza la maseneta la Marekani (Senate) limepiga kura ya kuamua kuacha kuisaidia Saudi Arabia katika vita inayoendelea huko Yemen. Mjini Washington, maofisa wa serikali ya mji huo wamepiga kura kubadili jina la mtaa ulipo ubalozi wa Saudia Arabia, na kuitwa Mtaa wa Jamal Khashogi. Lengo ni kuwakumbusha watu kila siku kuhusu unyama wa Saudia. Kikao cha halmashauri ya mji kinasubiriwa kukubali au kukataa mpango huo.
Hata hivyo, Rais Donald Trump ameonesha nia ya kuendeleza kufanya biashara kati ya Marekani na Saudia. Biashara hiyo yenye thamani ya Dola bilioni 110 (Tsh. Trilioni 250) inatengeza ajira 17000 kwa vijana wa Marekani, faida ambayo Donald Trump hataki kuikosa. Huko barani Ulaya, viongozi wa mataifa mbalimbali wamelaani mauaji ya Khashogi, na kutaka uchunguzi wa wazi na huru kisha wahusika wachukuliwe hatua. Waziri mkuu wa Uingereza, Bi. Theresa May amerudia kueleza msimamo huo alipohojiwa na waandishi wa habari huko mjini Buenos Aires. Tukio la mauaji ya Jamal Khashogi limeharibu mahusiano ya Saudi Arabia na nchi za Magharibi, na zaidi linatishia nafasi ya mwanamfalme Mohammed Bin Salman ya kurithi ufalme wa Saudia.
Ajenda nyingine nzito ni kuhusu tukio la Meli tatu za kivita za Ukraine kudhibitiwa na majeshi ya majini ya Urusi huko katika bahari ya Azov inayotenganisha ardhi ya kusini mwaka Urusi na Ukraine. Novemba 25, mwaka huu, meli tatu za kivita, mali ya Ukraine zilikuwa zikivuka kutoka bahari nyeusi kuingia bahari ya Azov kupitia mlango bahari wa Kerch. Mlango wa Kerch ni mahala pembamba sana, ni mlango unaounganisha bahari nyeusi (the black sea) na bahari ya Azov, na kutenganisha ardhi ya Urusi na Peninsula ya Crimea. Meli zinapopita eneo hilo, sharti ziruhusiwa na jeshi la maji la Urusi kwa ishara maalum baada ya kuwasiliana. Lakini kwa tukio la Novemba 25, Urusi wanadai kwamba Meli hizo hazikutoa taarifa, na hivyo ikatafsiriwa kama uvamizi. Baada ya kudhibiti Meli hizo, mataifa ya magharibi yamekuja juu kwa ukali, na Donald Trump ameamua kufuta mkutano wake na Rais wa Urusi, Vladimir Putin uliopangwa kufanyika huko Buenos Aires, kunakoendelea mkutano wa G20.
Nchini Ukraine, baada ya tukio hilo, Rais wa nchi hiyo Bwana Petro Poroshenko ametangaza hali ya hatari, na sheria za kijeshi (martial law) kutumika kwa siku 30. Pia ameondoa ruhusa ya wanaume kuanzia miaka 16 hadi 60, raia wa Urusi kuingia nchini humo. Serikali ya Urusi inadai, Rais wa Ukraine Petro Poroshenko alitengeneza makusudi tukio hilo ili atangaze hali ya hatari kwa kisingizio cha kukwepa uchaguzi wa Rais Unaotarajiwa kufanyika Machi 2019. Umaarufu wa Rais Poroshenko umeshuka hadi asilimia 7, hali inayoifanya akose nafasi ya kushinda. Katika kile kinachoonekana kuwa ni mpango wa makusudi, Poroshenko ameomba meli za kivita kutoka nchi za Magharibi, na kuomba Urusi wawekewe vikwazo zaidi vya kiuchumi. Urusi kwa upande wake wamewafikisha mahakamani, wanajeshi waliokuwa ndani ya meli hizo za Ukraine. Viongozi wa magharibi wameilaumu Urusi kwa tukio hilo, lakini wanadiplomasia huru wanaona kwa huo ni mpango wa makusudi wa Ukraine kutumiwa na mataifa ya Magharibi dhidi ya Urusi. Isipokuwa kwa Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel ambaye amedai uchunguzi zaidi kabla ya kuilaumu Urusi. Angela Merkel pia amepinga wazo la kuiwekea Urusi vikwazo zaidi.
Bila shaka kutakuwa na ajenda nyingine ndogo ndogo, tukio la mauaji ya Jamal Khashogi, Mgogoro wa Urusi na Ukraine pamoja na vita ya kibiashara ya Marekani na China na Mgogoro wa mipaka ya bahari ya chuma kusini ni ajenda nzito, zinazoendelea hata baada ya mkutano.
Viongozi wa nchi mbali mbali wamehudhuria mkutano wa G20, wapo viongozi wa serikali za nchi zinazounda G20 na wengine walioalikwa. Nchi na serikali zinazounda kundi la G20 ni Argentina, Australia, Brazil, Canada, China, Umoja wa Ulaya, Ufaransa, Ujerumani, India, Indonesia, Italy, Japan, Mexico, Urusi, Saudi Arabia, Afrika Kusini , Korea kusini, Uturuki, Uingereza na Marekani.
Viongozi wa Afrika waliohudhuria ni pamoja na Cyril Ramaphosa, Rais wa Afrika kusini, kama mwanachama wa G20, Paul Kagame, Rais wa Rwanda na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Rais Macky Sall wa Senegal ambaye ni mwenyekiti wa mpango wa maendeleo wa Afrika (NEPAD).
Tanzania na Diplomasia ya kimataifa.
Ajenda nilizoweka hapo juu, ambazo nyingi zinahusu migogoro kati ya mataifa makubwa, ni ajenda ambazo Taifa lolote duniani linaloshirikiana na mataifa yanayohusika katika migogoro hiyo, linapaswa kuzijua, kuzichunguza, na kuzitathimini, ili kuwa na taarifa za uhakika zinatakazosaidia maamuzi sahihi katika mashirikiano yake na mataifa hayo. Tanzania inashirikiana na Marekani, China, Urusi, Saudi Arabia, Uturuki na mataifa ya Ulaya mgharibi (Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, nk). Ni lazima, kuwa na kiongozi anayejua kucheza michezo ya kidiplomasia. Kiongozi mwenye utambuzi wa masuala ya kimataifa, ambaye atazungumza lugha ya kidiplomasia bila kuhatarisha mahusiano yetu na mataifa hayo, lakini bila kwenda kinyume na misingi ya kusimamia haki na usawa ulimwenguni kote, kama ilivyowekwa na Baba wa Taifa, Mwl Julius K. Nyerere.
Bila kupepesa macho, Rais aliyepo madarakani, hana uwezo wa kidiplomasia, achilia mbali utayari wake. Kauli zake na matendo yake katika mambo yanayogusa mahusiano ya kimataifa ni dhahiri kwamba, yupo nje ya ulingo wa tasnia hiyo. Ni wakati wa kuanza kufikiri, pamoja na sifa zingine, umuhimu wa sifa ya uwezo wa kidiplomasia kama ilivyokuwa awali.
Diplomasia inataka akili na hekima kubwa, na ufikirifu wa hali ya juu, hasa kwa nyakati tunazoekea ambapo migogoro ya kimataifa inaweza kuongezeka maradufu.
Tayari kuna hisia za kuibuka kwa vita kuu ya Tatu ya dunia. Leo tunashuhudia majigambo ya vifaa vya kivita kati ya Urusi na Marekani, nchi ambazo tunashirikiana nazo. Mgogoro mkubwa wa kibiashara kati ya Uchina na Marekani, Nchi ambazo tunashirikiana nazo. Ikitokea nyakati za kuchagua upande, tutachagua wapi? Itategemea na ufahamu au ujinga wa kidiplomasia. Mashirikiano yetu na nchi mojawapo, yanaweza pia kuathiriwa na migogoro baina ya nchi hizo, ni vema kujua namna ya kucheza karata ili kuepuka matokeo hasi, kwetu na kwa vizazi vijavyo.
Rais aliyepo Madarakani, anapotoa kauli hadharani, zinazoonesha chuki dhidi ya mataifa tunayoshirikiana nayo katika mambo mengi, ni hatari. Mathalani, Rais Magufuli anapowasema vizuri Wachina, na kuwasema vibaya mataifa ya Magharibi, kwa sababu moja ya masharti ya mikopo au misaada, ni matokeo ya kukosa utashi wa kidiplomasia. Tanzania inashirikiana na mataifa ya Magharibi katika maeneo mengi; Elimu na Tafiti, Ulinzi na Usalama, Vita dhidi ya ugaidi nk. Rais mwanadiplomasia anapaswa kujua namna ya kuepuka migogoro zaidi badala ya kuikuza. Ndio dunia inavyoenda.
Ndio maana, pamoja na uhasimu wa Marekani na Urusi, lakini wanashirikiana katika teknolojia ya uchunguzi wa anga. Septemba mwaka 2017,Mashirika makubwa ya uchunguzi wa anga duniani, Roscosmos la Urusi na NASA la Marekani yalitia saini muendelezo wa ushirikiano katika kuchunguza anga za mbali. Mashirikiano ya kisayansi hayajaathiriwa na uhasimu wa kisiasa, kwa sababu ya utashi wa kidiplomasia.
Na ni vema kujua, lengo la utashi wa kidiplomasia sio kujifanya mnyonge, bali kuboresha ushirikiano. China inaihitaji Tanzania, Marekani inaihitaji Tanzania, Uturuki inaihitaji Tanzania, Urusi inaihitaji Tanzania, kwa faida zao, na Tanzania inazihitaji nchi hizo, kwa faida yake, katika maeneo tofauti tofauti. Hakuna nchi inaweza kusonga bila kushirikiana na nchi zingine.
Je! Mwaka 2020, tutahitaji Rais Mwenye utashi wa kidiplomasia?
Watanzania tunabahati kwani tumeonja marais wa namna mbalimbali. mwanadiplomasia JK kaondoka juzi juzi tu hivi katuachia nini cha maana? Tuache kujifanya tumezaliwa jana. Kama huna la kusema hata kukaa kimya pia ni kufikisha mawazo
 
Aliyekutuma akupe na pesa zakutosha maana utaungua jua sana kumnadi mtu wako
 
Hizi hoja mnazojenga kutuaminisha watanzania tutoke kwenye mstari hatuwezi kuwaelewa.

Sisi watanzania kumchagua Magufuli tuliangalia vitu vingi hasa matatizo yetu ya ndani. Masuala ya misuguano baina ya Marekani na China kwetu ni vitu minor sana ukizingatia matatizo mengi tuliokuwa nayo ambayo Magufuli anayamaliza.
 
Dah hii kampeni mliyoianza mtamuingiza ndugu yenu kwenye matatizo makubwa. Mambo yoote uliyoyaeleza yanawahusu mabalozi wa tz katika nchi husika zaidi ya hapo kwani hayo matatizo ya China Na marekani yanatuhusu nini. Mnataka mturudishe kwenye ombaomba
 
CHADRAMA MCHARUKO KWISHNEY
 
Back
Top Bottom