Tunahitaji Mapinduzi ya Viongozi (eviction) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunahitaji Mapinduzi ya Viongozi (eviction)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shaycas, Jun 16, 2009.

 1. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mapinduzi yana sura mbili:ama kutumia majeshi au kuunda serikali mbadala).
  Je Tanzania tunahitaji ipi kati ya aina hizo.
  LABDA NIDOKEZE MAHITAJIO YA KUFANIKISHA AINA YOYOTE YA MAPINDUZI.
  1.Uongozi mzuri wa anayetaka kupindua.
  2.Muda wa kutosha kufanya maandalizi na mipango ya kupindua.
  3.Ardhi(terrain) itakayotumika kuanda mipango yao bila kuingiliwa na serikali iliyopo madarakani.
  4.Intelijensia,itawezesha kujua mienendo ya serikali dhidi yao na mipango mingine.
  5.
  MAMBO AMBAYO YANACHANGIA MAPINDUZI.
  1.Utawala mbovu na ubadhirifu.
  2.Tofauti kubwa ya kipato kati ya tajiri na masikini.
  3.Ukabila na Udini ama ktk serikali au jamii husika inapohisi tofauti.
  4.Ubaguzi hasa wa rangi.
  5.
  Je kwa mambo hayo,tunahitaji mapinduzi?Kama jibu ni ndio ni aina ipi ianze?
  Kama ni hapana,kwanini?
   
 2. SYLLOGIST!

  SYLLOGIST! JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2009
  Joined: Dec 28, 2007
  Messages: 306
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Wewe umefanya mangapi? hayo mapinduzi?

  "Tunahitaji"?

  "Mapinduzi yana sura mbili:ama kutumia majeshi au kuunda serikali mbadala"

  Sasa kama mapinduzi yamelengwa kwa viongozi? Bado tuna sababu ya hayo hapo chini?

  Kutumia Jeshi au Serikali mbadala ndio nini?

  Wacha usaliti! Kwa njia uliyotumia uko evicted!
   
 3. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mapinduzi yanayohitajika kwa sasa ni ya fikra za Watanzania ili washiriki uchaguzi 2010 na kuchagua viongozi waadilifu,kama fedha za ufisadi zitaendelea kutumika na kupatikana viongozi wabadhirifu basi mapinduzi ya aina nyingine yachukue njia yake.
   
 4. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  PIA USISAHAU HITAJIO LA KUUNGWA MKONO NA UMMA(popular support) na UUNGWAJI MKONO TOKA NJE(external support)
   
 5. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  USIWE UNA KURUPUKA,KAMA ULIKUWA NA SWALI UNGEULIZA KABLA.
  Viongozi ina maana ya serikali iliyopo madarakani,serikali mbadala ni kwa namna ya kikundi chenye nguvu ya hoja na ushawishi ili ipate kuungwa mkono na wengi,hatimae atwae madaraka
   
 6. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Assume wewe ndio kiongozi wa wanamapinduzi na umefanikiwa kuipata nchi nini utakifanya ili uwaletee maendeleo wananchi wako?
   
 7. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45

  Mimi nimetoa mada wanajamii watafakari kama kuna haja ya kufanya mapinduzi au la na nimetoa walau sababu zinazochangia kuwepo mapinduzi ktk sehemu nyingi za dunia.
   
 8. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mimi na fikiri kutoa sababu si mwarobaini inabidi utoe sababu na baadae utoe majibu .

  Ndio maana nafikiri mapinduzi mengi hapa duniani tumeyaona na huwa yanavuruga zaidi hali kuliko ilivyokuwa awali kwa sababu wenda nao huwa wana sababu tu na hawana majibu.
   
Loading...