Tunahitaji 'Kichwa cha Yohana'

Swadakta! Kiongozi wetu siku akiwa tayari kutenda hayo, watanzania ni wasamehevu na husahau yote. Wala suluhu si kuwateua kina fulani kutoka upinzani ili tujue kweli mkuu anafanya maamuzi magumu.
 
Mkuu sheria Mama inaweza kuwepo, lakini hakuna nchi inayoweza kuikwepa kauli kuu ya kiongozi mkuu wa nchi.

Kiongozi mkuu anaweza kuwa na udhaifu wake mwingi lakini bado hatujafikia huko ambako mamlaka ya rais yanaweza kupunguzwa kwa ghafla tu. Ni mchakato wenye kuhitaji muda. Na wakati tunaelekea kwenye ukamilifu wa mchakato huo, basi na tuwe tayati kuuishi uhalisia wa mambo.
 
Tuache unafiki wa kitoto,kwanini tulitaka uhuru kutoka kwa Mwingereza?Ili tujitawale tuweze kuondokana na dhuluma,ukandamizaji,unyonyaji.
Kudai katiba ni haki yetu,asietaka katiba ya Warioba ahamie Korea ya Kaskazini atuachie
Tanzania yetu.
 
Kauli kuu ya rais katika taifa lenye uhuru wa kikatiba itatolewa kwa adabu na kwa maslahi mapana ya taifa tu na si kwa maslahi ya chama chake kama ilivyo sasa. Pale ambapo wananchi wataona rais analeta za kuleta basi kupitia bunge lao wanaweza kumwadabisha. S. Afrika ni mfano mzuri wa nchi yenye siasa ambazo rais pamoja na mamlaka yake anaweza kuitwa na bunge na kuonywa au kufukuzwa kazi. Hapa kwa mazingira haya tutangoja sana
 
Ni kweli tutangoja sana. Siasa maandazi za kumuita mtu fisadi kwa miaka minane halafu jamii inaaminishwa kwa miezi mitatu kwamba ameshakuwa malaika, sitatufanya tungoje kwa miaka mingi ijayo.

Maslahi ya chama tawala ndio yale yale ya mwananchi wa kawaida, udhaifu fulani fulani katika utekelezaji wa lengo kuu la kuinua maisha ya kila mtanzania, sio kigezo cha kuona kila kinachofanyika hakina maana.
 
Kukwepa kauli ya mkuu wa nchi yawezekana kama "dira" ya nchi ipo imara na sahihi.Trump aweza kuwa kiongozi mpuuzi kuliko wote wa kizazi hiki lakini dira ya Marekani inamdhibiti. Hicho ndo tunataka na kukihitaji sana.
HOJA ni je,kwa aina ya wanasiasa na viongozi tulionao tunaweza?
 
Mahakama ya mafisadi ipo. Waambie wawapeleke hao mafisadi. Na maslahi ya chama hayawezi kuwa maslahi ya wananchi, labda ya wanachama. Ingekuwa hivyo basi leo huu uzi wala usingekuwepo
 
Kwahiyo kwako wewe Maendeleo kwenye Taifa ni vitu
 
Hapa ndipo mnapoharibu
Mnasema muda bado LINI??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…