Tunahangainga na viwanda tunaisahau elimu

Tunahangainga na viwanda tunaisahau elimu

Joined
Dec 23, 2017
Posts
35
Reaction score
69
Habar wadau wote.kama kawaida huwa sifumbii macho pale ninapokuwa ninaona kuna vitu vinaenda ndivyo sivyo hususani katika elimu.......

Miaka michache iliyopita serikali ili zindua sera mpya ya elimu ambapo kimsingi ni nzuri kimaandishi.Sambamba na hilo serikali ilileta mtaala mpya ambao utaenda na hiyo sera mpya ya elimu.Ndani ya mtaala mpya vimetajwa vitu vingi tena vizuri kimaandishi.........

Serikali ili peleka baadhi ya walimu kujifunza huo mtaala mpya namna ya kuutekeleza ambapo kimsingi mtaala ulianza kutumika mwaka jana kwa darasa la tatu ambapo mwaka huu wameingia darasa la nne.Cha kusikitisha mpaka leo hii hakuna hata kitabu chochote cha mtaala mpya cha darasa la nne.

Mbaya zaidi darasa la nne wanamtihani wa taifa sasa najaribu kuuliza watatumia mtaala upi kutunga huo mtihani wao.Tukumbuke hawa ndiyo watakao ishia darasa la sita ila mpaka leo hakuna hata semina ya kwa walimu wa madarasa hayo husika walioenda kufundishwa namna ys KUCHOPEKA KK......

Kimsingi sikejeli sera ya kuwa na viwanda vingi ila najaribu kujiuliza je kama hatuna elimu katika hivyo viwanda situtaenda kuwa makuli tu humo viwandani mwisho wasiku tuseme wanapendelea.....

WHAT THE SHAME wakati wenzetu wanaunda mamitambo na mamashine makubwa makubwa sisi bado mpaka leo tunamtoto yupo darasa la sita anatakiwa afundishwe kusoma na kuandika tutafika kweli dunia ya leo hii halafu unamuhimiza muwekezaji aje ajenge kiwanda kwa watu wasisoma siwataiba nyaya na chuma wakauze screpa...ELIMU,ELIMU,ELIMU NDIYO KIPAUMBELE VENGINE VITAJIPANGA TUKISHAKUWA NA WASOMI WENGI
 
Back
Top Bottom