Tunafanya maombi huku tunaendekeza uzembe. Tutatoboa kweli na hii Corona?

twende kazi

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,520
459
Wakuu wasalaam,

Naandika kwa masikitiko makubwa sana nikiwa kwenye Coaster moja kuelekea mji fulani. Nilichoshuhudia humu ndani ni upumbavu wa kiwango cha juu sana raia hawajionei huruma kabisa kama kuna janga la corona.

Gari haipo "level siti", watu wanaminyana na kusogeleana sana, watu wanaongea hovyo na kutema mate, watu hawatumii sanitizers kwa kifupi watu wamejiachia mno.

Ole wetu wadanganyika Mungu yu pamoja nao na wale watu wenye maarifa na wanaotumia akili zao kwa ufasaha. Tukiendekeza huu upumbavu hakika tutaangamia. Mungu tusaidie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una uhakika gani kama hawatumii sanitizer?

Ulitaka wanywe humo kwenye gari ndio uone kama wanatumia?

What if kama wanapakaa wakiwa wanatoka majumbani mwao kisha wanazihifadhi kwenye mapochi? Ama ulikagua coaster nzima ukaprove kuwa hawana?

Huu miongoni mwa hao wapumbavu, hata we pia hujionei huruma na ndio maana ukathubutu kupanda bus iliyojaa na pia kwanini usitulie nyumbani? Kama huwezi kupanda hata boda uwe peke yako?

Haya mambo ni kuchukua tahadhari na kuendelea kumuomba Mungu. Period
 
Back
Top Bottom