Tunaelekea Wapi na Migogoro hii ya Kidini?

Tunaelekea Wapi na Migogoro hii ya Kidini?

Rev lusungu

New Member
Joined
Feb 12, 2013
Posts
2
Reaction score
1
Vyombo mbali mbali vya habari jana usiku na leo asubuhi wamaripoti kuhusu vurugu za kidini zilizotokea Geita. Vurugu hizo ni muendelezo wa hali tete baina ya wakristo na waislam ilioendelea hapa nchini kwa muda mrefu.

Mwaka jana ulikuwa mwaka mgumu sana na tulishuhudia hali hio ikichukua mkondo mpya. Nyumba za ibada zilichomwa moto kote Tanzania, na matukio makubwa zaidi yakiwa ni yale ya Zanzibar ambapo ndani ya wiki moja nyumba 6 za ibada ziliharibiwa mnamo mwezi Mei, na yale ya Mabagala Dar es Salaam, ambapo ndani ya siku mbili nyumba za ibada 7 ziliharibiwa vibaya.

Pia tulishuhudia kudhihakiwa kwa misaafu ya dini kule Bagamoyo kiasi cha kutumbukizwa chooni! na kukojolewa kule Mbagala.

Isitoshe shule mbili za serikali zililazimika kufungwa kutokana na migogoro ya dini ilioendelea katika shule hizo za Bagamoyo sekondari, na kibiti. Hayo yote yalitosha kutushitua na kutoonyesha kuwa hatua madhubuti zinapaswa kuchukuliwa kuzuia migogoro ya kidini kuwa mikubwa zaidi.

Hata hivyo kwa masikitiko makubwa nalazimika kusema kuwa hatua za kutosha hazikuchukuliwa. Matokeo ya kutochukuliwa kwa hatua hizo kumepelekea mwaka huu kuanza vibaya kwa migogoro ya kidini kuchukua mkondo mpya wa kugharimu maisha ya watu.

Jana mkoani Geita waislam na wakristo wamepigana na kuuana wakigombea haki ya kuchinja. Tutaendelea kuangalia hali ya nchi yetu ikiharibika mpaka lini? Tutaendelea kuruhusu migogoro ya kidini itugawe mpaka lini? Tukumbuke kuwa hakuna vita mbaya kama vita vya kidini! historia inatuonyesha kuwa wakristo na waislam kila walipopigana vita vilichukua muda mrefu sana kuisha, na hata pale vilipoisha madhara ya vita hivyo yalichukua muda mrefu zaidi kurekebishika.

Nashukuru kuwa kuna juhudi za pamoja za viongozi wa dini hizi mbili kukutana na kujadili mahusiano baina ya dini hizi mbili. Ila kwa bahati mbaya sana juhudi hizo huishia tu ngazi ya mkoa na mara chache hufika ngazi ya wilaya.

Mbaya zaidi kuna makundi ndani ya dini zote mbili ambao kwa maksudi wanapotosha juhudi hizi kwa kuziita kuwa ni juhudi za kuunda dini mseto.

Napenda kuwakumbusha kuwa nchi ikiingia katika machafulko si waislam wala wakristo watoaweza kuhubiri dini zao wala kuabudu. Tukumbuke vita daima haina mshindi, hata yule anaeitwa kuwa ameshinda huwa amepoteza mali, amepata majeraha, na amepoteza maisha ya watu anaowapenda na kuwajali.

Naamini kuwa ni wakati sasa ambapo kila msikiti unahitaji kujenga mahusiano na makanisa yaliouzunguka, na kila kanisa kujenga mahusiano na misikiti iliouzunguka.

Viongozi wa makanisa na misikiti wawe wanakutana mara kwa mara kujadili mambo yanayoendela katika eneo linalowazunguka. Kwa kufanya hivyo tunaweza kumaliza matatizo mengi kwa njia za majadiliano na sio mapigano.

Natoa wito kwa wanasiasa, mara nyingine wao ndio wamekuwa chanzo cha vurugu, wametumia tofauti zetu za kidini kama mtaji wao wa kisiasa. Ni kweli njia hii imewawezesha kupata wanachokihitaji, lakini imeiacha jamii ikiwa na mgawanyiko ambao ni hatari na mgumu kurekebishika.

Kama kweli wanasiasa wanaipenda Tanzania kama wanavyojinadi, basi wajaribu zaidi kutuunganisha kuliko kutugawa! Mtu anaeipenda Tanzania lazima atasema Tanzania kwanza maslahi yangu baadae. Mtu anaeweka maslahi yake kwanza na maslahi ya Taifa badae ni fisadi kuliko mafisadi wote unaowafahamu.

Watazania tumuogope na tusikubali atugawe. Kumbuka salamu ya waislam kote duniani ni asalm aleykum maana yake ni amani iwe nawe, kama wewe ni muislam jaribu kujenga hiyo amani kama dini yako inavyokutaka, na wakristo wote wanaitwa wakristo kwa sababu ni wafuasi wa Yesu Kristo ambae ni mfalme wa amani.

Mkristo anae vuruga amani anafanya uhaini dhidi ya mfalme wake Yesu kristo. Mungu Ibariki Tanzania
 
Vyombo mbali mbali vya habari jana usiku na leo asubuhi wamaripoti kuhusu vurugu za kidini zilizotokea Geita. Vurugu hizo ni muendelezo wa hali tete baina ya wakristo na waislam ilioendelea hapa nchini kwa muda mrefu. Mwaka jana ulikuwa mwaka mgumu sana na tulishuhudia hali hio ikichukua mkondo mpya. Nyumba za ibada zilichomwa moto kote Tanzania, na matukio makubwa zaidi yakiwa ni yale ya Zanzibar ambapo ndani ya wiki moja nyumba 6 za ibada ziliharibiwa mnamo mwezi Mei, na yale ya Mabagala Dar es Salaam, ambapo ndani ya siku mbili nyumba za ibada 7 ziliharibiwa vibaya. pia tulishuhudia kudhihakiwa kwa misaafu ya dini kule bagamoyo kiasi cha kutumbukizwa chooni! na kukojolewa kule mbagala. Isitoshe shule mbili za serikali zililazimika kufungwa kutokana na migogoro ya dini ilioendelea katika shule hizo za bagamoyo sekondari, na kibiti. Hayo yote yalitosha kutushitua na kutoonyesha kuwa hatua madhubuti zinapaswa kuchukuliwa kuzuia migogoro ya kidini kuwa mikubwa zaidi. Hata hivyo kwa masikitiko makubwa nalazimika kusema kuwa hatua za kutosha hazikuchukuliwa. Matokeo ya kutochukuliwa kwa hatua hizo kumepelekea mwaka huu kuanza vibaya kwa migogoro ya kidini kuchukua mkondo mpya wa kugharimu maisha ya watu. Jana mkoani Geita waislam na wakristo wamepigana na kuuana wakigombea haki ya kuchinja. Tutaendelea kuangalia hali ya nchi yetu ikiharibika mpaka lini? Tutaendelea kuruhusu migogoro ya kidini itugawe mpaka lini? Tukumbuke kuwa hakuna vita mbaya kama vita vya kidini! historia inatuonyesha kuwa wakristo na waislam kila walipopigana vita vilichukua muda mrefu sana kuisha, na hata pale vilipoisha madhara ya vita hivyo yalichukua muda mrefu zaidi kurekebishika.
Nashukuru kuwa kuna juhudi za pamoja za viongozi wa dini hizi mbili kukutana na kujadili mahusiano baina ya dini hizi mbili. Ila kwa bahati mbaya sana juhudi hizo huishia tu ngazi ya mkoa na mara chache hufika ngazi ya wilaya. Mbaya zaidi kuna makundi ndani ya dini zote mbili ambao kwa maksudi wanapotosha juhudi hizi kwa kuziita kuwa ni juhudi za kuunda dini mseto. Napenda kuwakumbusha kuwa nchi ikiingia katika machafulko si waislam wala wakristo watoaweza kuhubiri dini zao wala kuabudu. Tukumbuke vita daima haina mshindi, hata yule anaeitwa kuwa ameshinda huwa amepoteza mali, amepata majeraha, na amepoteza maisha ya watu anaowapenda na kuwajali.
Naamini kuwa ni wakati sasa ambapo kila msikiti unahitaji kujenga mahusiano na makanisa yaliouzunguka, na kila kanisa kujenga mahusiano na misikiti iliouzunguka. Viongozi wa makanisa na misikiti wawe wanakutana mara kwa mara kujadili mambo yanayoendela katika eneo linalowazunguka. Kwa kufanya hivyo tunaweza kumaliza matatizo mengi kwa njia za majadiliano na sio mapigano.
Natoa wito kwa wanasiasa, mara nyingine wao ndio wamekuwa chanzo cha vurugu, wametumia tofauti zetu za kidini kama mtaji wao wa kisiasa. Ni kweli njia hii imewawezesha kupata wanachokihitaji, lakini imeiacha jamii ikiwa na mgawanyiko ambao ni hatari na mgumu kurekebishika. Kama kweli wanasiasa wanaipenda Tanzania kama wanavyojinadi, basi wajaribu zaidi kutuunganisha kuliko kutugawa! Mtu anaeipenda Tanzania lazima atasema Tanzania kwanza maslahi yangu baadae. Mtu anaeweka maslahi yake kwanza na maslahi ya Taifa badae ni fisadi kuliko mafisadi wote unaowafahamu. Watazania tumuogope na tusikubali atugawe. Kumbuka salamu ya waislam kote duniani ni asalm aleykum maana yake ni amani iwe nawe, kama wewe ni muislam jaribu kujenga hiyo amani kama dini yako inavyokutaka, na wakristo wote wanaitwa wakristo kwa sababu ni wafuasi wa Yesu Kristo ambae ni mfalme wa amani. Mkristo anae vuruga amani anafanya uhaini dhidi ya mfalme wake Yesu kristo. Mungu Ibariki Tanzania
Ukweli ni kwamba mzee ''MUDI''ALITULETEA JANGA DUNIANI!! Kila mtu anaejua mafundisho ya mudi na aya zake hatoona shaka kuniunga mkono kwa hili, dunia karibu yote ni matatizo hasa sehemu zenye wafusi wa ''MUDI'' WAFUASI WA MZEE MUDI JITAHIDINI KUSOMA NA KUTAFAKARI BADALA YA KUKARISHWA BILA KUJUA.
 
Ukweli ni kwamba mzee ''MUDI''ALITULETEA JANGA DUNIANI!! Kila mtu anaejua mafundisho ya mudi na aya zake hatoona shaka kuniunga mkono kwa hili, dunia karibu yote ni matatizo hasa sehemu zenye wafusi wa ''MUDI'' WAFUASI WA MZEE MUDI JITAHIDINI KUSOMA NA KUTAFAKARI BADALA YA KUKARISHWA BILA KUJUA.

we! Box.
 
CCM ndo ilikuwa ajenda yake 2000 kwa cuf 2005 na 2010 kwa chadema sasa madhara yake tunayaona halafu waislamu waache ubabe wa kijinga wa kuanzisha vujo huko buselesele kama wakristo waliamua kujichinjia nyie inawahusu nini mlilazimishwa kuinunua.
 
Hakuna sehemu yenye waislamu iliyowahi kuwa na amani. Waislam hawana neno amani, na wala wajibu. Wamekariri neno haki wakimaamisha matakwa!. Inatakikana kiongozi imara ya kudhibiti akili mbofumbofu kama za hawa jamaa.
 
Nchi yeyote ikishakuwa na waumini wa Moh.. Kwa kweli ni janga, ebu angalia jinsi nchi ambazo hazina waumini hao kwa wingi utagundua zina amani sana, mfano South africa,zimbabwe, zambia, msumbiji,malawi, namibia, na nchi nyingi tu zina amani lakini tukichanganyana tu basi ni laana, hata ukienda nchi ambayo wako wao wenyewe tu ni majanga tu!
 
Hakuna sehemu yenye waislamu iliyowahi kuwa na amani. Waislam hawana neno amani, na wala wajibu. Wamekariri neno haki wakimaamisha matakwa!. Inatakikana kiongozi imara ya kudhibiti akili mbofumbofu kama za hawa jamaa.
Asilimia 80% ya waislamu hawaijui qruani zaidi ya kusomewa na viongozi wao, ambao hata wao wenyewe si waelewa, kwa kweli ni dini yao inavyofundisha, ukisikia tu jinsi watoto wao wadogo wanavyofundishwa dhidi ya mkristo utashangaa! Ni chuki tu tena wakiwa watoto! Unayegemea watakuwaje wakikua, ni full ujinga, mapepo yanaruka na.........
 
Jamani marehemu mudi alileta mafundsho mazuri tu.. Ila hawa wenzetu wameyafanyia tafsiri mbovu na ndio maana haya yote yanatokea
 
Asilimia 80% ya waislamu hawaijui qruani zaidi ya kusomewa na viongozi wao, ambao hata wao wenyewe si waelewa, kwa kweli ni dini yao inavyofundisha, ukisikia tu jinsi watoto wao wadogo wanavyofundishwa dhidi ya mkristo utashangaa! Ni chuki tu tena wakiwa watoto! Unayegemea watakuwaje wakikua, ni full ujinga, mapepo yanaruka na.........


mmmmhhhh! naona hapa nipite bila kutia neno
 
Mnahangaishwa na mafunzo ya mababu wa kiarabu na kiyahudi na kizungu. Mkielewa hilo kwamba mmefanywa watumwa we imani za kikoloni basi upuuzi huu huwezi kuuona. Umewahi kuona wasio na dini au wapagani wakihangaika na kuuana Kama nyie wenye dini?
 
Back
Top Bottom