Tunachagua chama au mtu?

Tunachagua chama au mtu?

aminiusiamini

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2011
Posts
3,577
Reaction score
2,226
Wanajamvi,

Mimi naanza kuona kabisa kuwa elimu yetu Tanzania imegawanywa na kurubuniwa kwa makusudi makubwa sana,huku wale waliokuwa nazo wanapeleka watoto wao shule private huku mtoto wa maskini akibaki kurudi nyuma;na hawa maskini ndio walio wengi na wapiga kura.

Kwanini nasema hivi?.Nimeona watanzania tulio wengi hatujui nini tunataka,sio kazi tu na na kwenye maisha yetu binafsi bali hata kwenye hatima ya nchi yetu sote;ni vipi tunawezaje kuchambua jambo kwa urefu na mapana,na vipi tunawezaje kufikia jambo bila woga.

Tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu,nimeona na kugundua chama cha mapinduzi kwa miaka hamisini na ushehee,kimedidmiza elimu kwa mtanzania wa kawaida, ilikusudi wao waendele kula na kutawala nchi kwasababu wajinga ni wengi na wengi ambao hawajui kupembua mambo, huku wakisubiri kupewa kofia na kanga na matajiri ,masikini wakieka fursa zao kubwa na maisha yao rehani.Elimu ni kitu cha msingi sana katika maendeleo popote pale duaniani.

Mtanzania leo ukimuuliza unamchagua nani atakuambia magufuli au lowassa.Ukiuliza kwa lipi anasimamia msimamo wake,unakuta hawana majibu ya msingi.Wasanii wetu nao njaa imewazidi.Tena inawazidi inapofikia kipindi cha uchaguzi.

Washasahau shida na mambo mengi ambayo serikali haiwasaidi kuleta maendeleo yao binafsi zaidi matumbo ya wachache wanaohodhi nafasi kubwa kwenye sekta hio.Nimefathaishwa na kushanganzwa na diamond ambaye ametoka kwenye shida sana tena hata kunizidi leo anasimama na kusema anasmimia chama fulani,kwa lipi?kwasababu yey anazo sasa? vip wale alio waacha nyuma? vip je,kama angeulizwa wakati ule bado yuko muuza mitumba na mtoto wa uswazi,leo hiii angesema anasimamia CCM?

Watanzania wenzangu,tusiwe waoga wa jambo na mabadiliko.Sio ni yangu kujarirbu kushawishi chama gani kinafaaa ila kama mtanzania kweli na unaipenda nchi yako,chukua muda utafakari kidogo juu ya hatima ya nchi yako.Tusisubiri kuambiwa na kikwete nani atuongoze,au NEPI na wengine wote ambao wanajua kuongea bila matendo na wasiojali hatima ya nchii.

Sote tuchague kiongozi na sio chama.Tusiwe watu wa mazoea tu kwamba ccm ndio chama na hakuna chama zaidi ya ccm au chadema ndio tu ina kiongozi imara,lazima tufikiri kidogo ndugu zanguni.
 
Tunajaribu maisha
hakuna cha chama wala mtu,
tukachoambiwa ni
tutawajengea nyumba kubwa sawa kilimanjaro(wimbo wa Dr remmy ongala)
 
CCM tuna kauli mbiu: Chama kwanza , Mtu baadaye!!

CCM kwanza, kupitia kwa wagombea wake kuanzia Urais mpaka Madiwani.

Mandla.
 
Tunahitaji mabadiliko, mabadiliko haya si ya Kiongozi tu. Kwani tukiweka tumaini kwa kiongozi(kitu ambacho hatupaswi kufanya) anaweza kurubuniwa au akaweza kusimama thabiti lakini kufanyiwa fitina na watu walio chini yake.

Mabadiliko tunayoyahitaji sasa ni ya CHAMA, nothing else.

Endapo tutabadilisha Chama watu watagundua wamiliki wa nchi hii ni WANANCHI wenyewe na si viongozi wa chama tawala. Na kutokea hapo tunaweza kutengeneza Tanzania tunayoitaka, ni lazima tufanye hivi kuleta ushindani ili kwamba chama kilichopo madarakani kisibweteke(kama ilivyo kwa miaka mingi sasa) na kujitahidi kufanya majukumu yake kwani watajua wasipofanya hivyo nchi itachukuliwa na Chama/vyama pinzani.

So principally, tunahitaji mabadiliko ya CHAMA kwanza.

Over 20years CCM hiyo hiyo katika nchi hiyo hiyo na watu wale wale, kwa ahadi zile zile wame fanya yale yale then tutegemee mabadiliko, Dunia itatushangaa!

Tutakuwa wapumbavu kufikiri kufanya jambo lile lile kwa namna ile ile tutapata majibu tofauti.
 
Je ile vita yenu ya ufisadi imeishia wapi? Mnalo mwaka huu
 
UKAWA KWANZA THEN TUTAJIPANGA MBELENI..
1.TULIPOPATA UHURU NI WAPI WALIOTUONGOZA WALIWAHIKUONGA NCHI KABLA?
2.TANU ILIKUWA NA MIAKA SABA TU TOKA KUUNDWA KWAKE.
3.CHADEMA WANAZAIDI YA 20yrs..Now..
TANZANIA KWANZA CHAMA KITAFUATILIA HUMOHUMI KULIKO MATAKWA YA WANANCHI YAO...
 
Nyumbu ndo wa fikira hizo za kuchagua chama huku kiongozi wa chama ameoza..very naive way of thinking
 
Hayo maswali hayana kichwa wala miguu,nikama na swali la kuku na yai kipi kimetangulia.NINACHOJUA MM NAMPA KURA YANGU LOWASA,MABADILIKO NI SASA,
 
Kuhusu vita ya ufisadi ni kwamba,
1.tunatoa kundi kubwa mno la ufisadi then tuchambue wema wengine kando..
2.vipi vita yenu ya kulifanya taifa hili masikini wa kutupwa duniani?
 
Back
Top Bottom