Sitta hana issue tena Urambo, alishafika kilele cha kisiasa kwa kuwa spika na sasa amerudi kuwa waziri tena wa wizara ndogo sana!!!
Sitta Kashachoka sana kisiasa, umri nao umeshamkata pia, kufikia 2015 huenda akawa na miaka 70, ndio maana hata ubunge ameshasema hataki kugombea tena.
Kwa sasa amelenga urais ili kabla ya kuvuta naye aonje raha ya Magogoni.
Bahati mbaya sana CCM hatuna tena utaratibu wa kuandaa warithi wa kisiasa, Sitta naye hajafanya hivyo kama vile Juma Kapuya ambaye naye kakwepa kuandaa mrithi wake jimboni mwake.
CCM tuanze kujiandaa kuhesabu maumivu tena maumiivu makali sana Urambo, kwani majimbo yote mawili ya Urambo(mashariki na magharibi) tutayapoteza tu, kama itakavyokuwa kwa majimbo pacha ya Igunga na Nzega ama Tabora mjini, Bukene na Sikonge