Tuna viongozi wa aina gani tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuna viongozi wa aina gani tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kingfish, Apr 19, 2012.

 1. kingfish

  kingfish JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Jana nilifuatilia kikao cha bunge kikijadili taarifa ya C.A.G,ni jambo la kushangaza kuona waziri wa fedha hakuwepo na waziri Lukuvi kudai Mkulo kuwa yupo U.S.A. "kuandaa bajeti". Kama alivyosema zitto kuwa mkulo ilitakiwa awepo kwa sababu taarifa ya c.a.g na taarifa za kamati zilihusu moja kwa moja wizara yake.Mimi binafsi nasikitishwa na kitendo cha waziri wa fedha kutokuwepo kwa sababu kuna madudu mengi yaliyobainika katika taarifa hizi ambapo fedha nyingi za umma zimeliwa,sioni sababu ya Mkulo kwenda huko,la muhimu angekuwepo ili kupata taarifa hizo na kupata ushauri namna ya kutatua matatizo hayo.kwenda kuomba misaada huko nje hakutusaidii kwa sababu hata misaada hiyo ikija bado italiwa tu, muhimu ni kiziba mianya hiyo inayovujisha fedha za umma.Mawaziri wetu wameonyesha dharau kubwa hata naibu spika amesema mawaziri wanaposafiri ni vema waijulishe ofisi ya bunge.Viongozi wetu hawako serious na matatizo yanayoimaliza nchi yetu.
   
Loading...