Tuna Tatizo la Mawasiliano-kiuchumi, kijamii na kisiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuna Tatizo la Mawasiliano-kiuchumi, kijamii na kisiasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Iga, May 5, 2010.

 1. I

  Iga Senior Member

  #1
  May 5, 2010
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tuna Tatizo la Mawasiliano-kiuchumi, kijamii na kisiasa

  YAPO madai kwamba Tanzania hivi leo ina tatizo kubwa la mawasiliano ya umma yanayowajulisha watu kwa wakati wategemee kitu gani kutokea siku fulani. Hapa hatuzungumzii idara fulani au vyombo vya habari binafsi maana hawa kwa upande wao wanajitangaza hata zaidi ya kujitangaza. Tatizo ni kwa upande wa serikali na vyombo vyake.Kwamba, pamoja na kuwa na idara za habari kila wizara tatizo la mawasiliano limezidi kuwa kubwa siku hata siku. Pamoja na serikali kuwa na Wizara ya Habari na mambo mengine mawasiliano kati ya dola na wananchi bado ni dhaifu. Isipokuwa kwa bunge tu, mahakama, polisi na taasisi nyingine za serikali kama magazeti ya serikali bado pamoja na kuwa na dhima ya kufahamisha na kuhabarisha watu mawasiliano ya moja kwa moja au kwa njia ya matangazo ni duni.

  Mifano kadhaa inatolewa kujenga ithbati juu ya lawama hizi za mawasiliano duni katika serikali ya awamu ya nne:

  Mkutano wa WEF haukutangazwa ipasavyo. Baadhi ya watu wamejua juu ya mkutano huu pale ambap Bwana Lukuvi na kisha Rais walipofahamisha umma kuwa kuna kitu kama hicho. Taarifa zingelikuwepo watu wengine wasiopenda maudhi na usumbufu wangeamua kuchukua likizo ya wiki moja au mbili wakatulie mahala tulivu na kula maisha kisha ndio usumbufu ukiondoka na wao warudi mjini.

  Ndivyo ilivyo pia kwa mikutano, semina, warsha na shughuli nyingine kimkoa, kitaifa na kimataifa wengi huwa tunapata habari baada ya jambo lenyewe kufanyika.

  Kwa kiasi fulani vyombo vya habari kwa kujikita kwenye habari za 'kiuchuro uchuro' kumechangia hili lakini hili halijaizuia serikali kututaarifu kupitia kwenye bodi za daladala ndani na nje ambako wachache wetu watakosa kuzijua taarifa husika kwa jinsi tunavyokaa muda mrefu kwenye vyombo kama hivyo vya usafiri.
  Kuhamia Dodoma. Hakuna anayejua kinachoendelea kuhusu serikali kuhamia Dodoma na kwa ishara na dalili zote ikiwemo hii ya mkutano wa WEF kufanyika Dar badala ya Dodoma kunaonesha kama awamu ya tano itaingia bila mtu kuwa kahamia Dodoma.

  Viongozi hawajulikani na kubwa zaidi haijulikani wanatoa mchango gani katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya wizara zao na kuwawezesha wananchi kunufaika na fursa zilizopo katika eneo lao la utawala. Dai la kuwa wananchi hawawajui viongozi wao ni kina nani. Iwe wale wa serikali kuu, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wenyeviti wa mitaa na madiwani linatia shaka kama kuna mshikamano wowote wa maana unaoweza kuikwamua nchi kiuchumi. Kijamii inaashiria kuwa wakati wowote nchi inaweza ikachanika vipande vipande maana hakuna nta au gundi inayowashikiza Watanzania pamoja na sasa ni kila mtu na lwake.

  Tumeona jamaa wa TBC walivyoteseka kupata majibu ya mitihani ya kidato cha sita wakati jambo hili linatakiwa kuwa katika almanac ya NECTA na sio kuwa lifanyike kama jambo la kushtukizia. Pengine siku moja kabla ya matokeo yenyewe NECTA ingeliwajibika kutoa matangazo kwenye magazeti, redio na televisheni kuwafahamisha wote wazazi kwa wanafunzi kuwa kesho wakifungua simu zao, intaneti na magazeti wataanza kukuta matokeo husika.

  TFF pamoja na kuwa na wasomi kadhaa wamekalia matangazo kuhusu kombe la dunia ikiwemo upatikanaji tiketi kwenye mtandao. Hili limefanyika TFF ikiwa inapewa mamilioni kama sio bilioni na FIFA baadhi yake ikiwa kwa ajili ya mambo kama haya ya mawasiliano.
  Achilia mbali uvurugaji mawasiliano mengine ambayo pengine hufanyika kwa sababu ambazo viongozi na wanaoshika fedha huko wanajua sababu yake ni nini!

  Wizara ya Elimu ambayo inasemekana ndio hupewa mialiko ya masomo kwa Watanzania kwenda kusoma nje inadaiwa hutoa tu asilimia ndogo ya nafasi hizo na kuzificha zingine kisha kuzigawa kwa watoto, ndugu na jamaa zao. Huko nyuma wakati nafasi za kusoma China zilikuwa nje nje, hivi leo nafasi hizo zinamezwa na watoto wa watumishi wizarani humo tu.

  Misiba isipokuwa kwa vibabu vya TANU na CCM haina mawasiliano ya kuridhisha na wengi wetu hupata taarifa baada ya marehemu kuzikwa. Hii pengine ni kwa sababu watumishi wa serikali wanadhani wote tuna uwezo wa kununua magazeti ambayo yamekuwa ghali mno kutokana na kodi ya serikali kwenye mali ghafi za uchapaji na uchapishaji. Au pia kudhani wote tuna umeme na tutasisikiliza redio au kuona taarifa kwenye televisheni kumbe sivyo. Bado upo umuhimu wa kubandika taarifa sehemu muhimu vijijini na mjini ni muhimu na vilevile kutumia taasisi za dini kutangaza habari za msiba ni jambo la busara.

  Mikutano na warsha nyingi ndani na nje ya nchi hufanyika kinyemela na hivyo kukaribisha zaidi watu wasiohusika na makanjanja-yaani-watu waliojikita katika kujua mikutano au warsha gani zitafanyika lini na wapi ili wakashike mshiko huko. Mambo yakiwa wazi zaidi mikutano na warsha nyingi zitahudhuria na wanaohusika na sio vinginevyo.

  Mashirika kama TANESCO, mahospitali, shule na vyuo vimeanza tabia ya kubadilisha bei za huduma au bidhaa zao au ada zinazolipwa bila wananchi kuarifiwa. Matokeo ya hili imekuwa ni migogoro isiyoisha kati ya walaji na wazalishaji au watoa huduma. Ikiwa mashirika na mashule yatakuwa wazi zaidi migogoro kama hiyo inaweza kuepukwa.

  Mradi kama ule wa Malaria unatangaziwa zaidi katika redio na TV ambazo watu wengi vijijini hawamudu au hawana muda wa kufuatilia. Ingelikuwa ni uzuri jambo hili lingepitishwa kwenye magazeti na hasa kwa kutumia michoro ya katuni au kwa sinema za bure ambazo zingeoneshwa na magari yanayozunguka huko vijijini.

  Fursa nyingi za kiuchumi nchi za nje zimekuwa hazitolewi na wizar a husika. Inaelekea wanaozipata ni wale walio karibu na viongozi wa wizara au wakubwa wengine nchini. Laiti hili lingefanyika basi wizara husika ingelikuwa na wavuti yake yenyewe na mambo haya yote yakawa wazi.
   
 2. Kobe

  Kobe JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 1,756
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Naunga mkono hoja yako 100%
  kwa kweli nchi imo gizani tumebakia kuishi kwa mazoea tu.
   
 3. Suki

  Suki JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 373
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Dang!
  Do you do lunch?On me.
   
Loading...