Tuna lipi la kujivunia Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuna lipi la kujivunia Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Quinty, May 27, 2011.

 1. Quinty

  Quinty JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 463
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  *NI laana, ni bahati mbaya, ni “Ujinga”, ni umaskini wa fikra, ni kupumbazwa au ni kitu gani hiki kinachosababisha tusherehekee miaka 50 ya Uhuru wetu bila ya kuwa na “vitu” vya uhakika?

  Hatuna maji ya uhakika, hatuna umeme wa uhakika, hatuna barabara za uhakika, hatuna chakula cha uhakika, hatuna elimu ya uhakika, hatuna hospitali za uhakika; watu wanakufa kwa malaria na magonjwa mengine yanayotibika!

  Kama vile hiyo haitoshi, hatuna usalama wa uhakika kwa maana kwamba ajali za barabarani zinaua watu kila kukicha, treni* zetu zinarudi nyuma badala ya kwenda mbele na kupoteza maisha ya Watanzania; vyombo vya majini navyo vimekuwa chinja chinja.

  Hatuna usalama wa uhakika; kwa maana kwamba hata mabomu yetu wenyewe yakinuna yanalipuka yenyewe na kuteketeza maisha yetu na mali zetu! Hatuna nyumba salama na hatuna makazi salama; tunaishi kwenye uchafu na kipindupindu ni ugonjwa wa kudumu.

  Tuna lipi la kujivunia kwa kipindi hiki cha miaka 50? Kwamba tuna amani na utulivu? Kwamba rais wetu ana ndege ya kisasa? Kwamba watawala wetu wanaendesha magari ya kifahari? Kwamba watawala wetu hata wakiugua mafua wanakimbizwa nchi za nje? Tumevumbua nini na kuunda nini? Tuna viwanda vingapi vinavyozalisha bidhaa za kuuza nje ya nchi? Ni Huduma gani ya kijamii isiyokuwa na kasoro?

  *Tuna lipi la kujivunia? Kwamba Kiswahili ni lugha ya taifa wakati tumeshindwa hata kusema hivyo kwenye Katiba yetu? Wakati kila mtu anajivuna kuongea Kiingereza? Mikutano yote ya kimataifa inayofanyikia hapa, hata rais wa nchi anaifungua kwa Kiingereza? Ni wapi duniani ambako lugha ya kigeni inaitawala lugha ya taifa?

  Tuna lipi la kujivunia? Kwamba tunawaachia wawekezaji wanasomba raslimali zote za nchi yetu?* Kwamba wanachimba madini na kutuachia mashimo? Au tujivunie kuwa dampo la bidhaa bandia na njia kuu ya kupitisha madawa ya kulevya?

  Ni wazi kilio chetu tunakielekeza kwa Serikali yetu inayoongozwa na CCM: Tunahitaji huduma za uhakika! Tunahitaji umeme wa uhakika, tunahitaji maji ya uhakika, tunahitaji shule za uhakika, tunahitaji matibabu ya uhakika na mengine mengi.

  Tunapenda kusikia Serikali yetu ikituelezea mbinu na mikakati ya kuondoa kero hizi zinazotuzunguka.* Hatupendi kusikia nyimbo za kujibu mapigo ya kina Dk. Slaa, Mbowe na CHADEMA yao. Itatusaidia nini kujua kwamba Dk. Slaa anapata mshahara wa milioni saba kutoka kwenye chama chake? Kwani mshahara wa Dk.Slaa unatoka kwenye kodi za wananchi?

  Tunachokifahamu, na wanachokifahamu CCM ni kwamba Dk. Slaa si miongoni mwa wale waliokwapua fedha za umma. Hatupendi kusikia malumbano ya CCM na CHADEMA. Tunapenda kusikia maisha bora kwa kila Mtanzania. Kama* bei ya sukari ingekuwa chini, kama maisha yangekuwa nafuu na kama watuhumiwa wa ufisadi wangefikishwa mbele ya sheria na kuhakikisha fedha zetu zilizochotwa zinarudi na kuwekwa kwenye mfuko wa taifa, nani angeshiriki maandamano ya CHADEMA?

  Kero zinazotuzunguka zikiendelea, umeme unakatwa siku nne bila ya maelezo, hata punguwani ataandamana!
   
 2. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwanaza ungeandika vitu vilivokuwepo wakati mkoloni anaondoka na ndio uandike mambo ambayo tangu wakoloni watoke hatujafanya! Lakini kwa jinsi ulivyo andika ni sawa na mlevi kuongea jinsi anavyo jisikia kuropoka! Tuna barabara kutoka mtwara hadi sirari ya lami,dar hadi babati lami,na barabara nyingine nyingi za lami na nyingine zinajengwa,tuna chuo kikuu chenye uwezo wa chukua wanafunzi 40,000,tuna uwanja wa mpira wa kuchukua watu 60000 ambao wachina wamechangia nusu ya gharama,huduma za upasua na madaktari wameongezeka, Wazawa tuna pata fulsa za kufanya biashara,idadi ya watanzania walio na degree ikilinganishwa tangu uhuru na mambo mengine mengi usiwe na mtizamo hasi tu! Demokrasia imekua hapa nchini hadi kiongozi wa upinzani Nchi haita tawalika na hakamatwi ana achwa tu,idadi ya watanzania wenye simu ya mkononi ni 6 kati ya 10 zamani mawasiliano ilikua hakuna! Vyombo vya habari viko huru zaidi,fursa za kibiashara kwa wenye akili timamu ni nyingi sana! Wakulima wetu wanapewa pembejeo,hospital na zahanati zimeongezeka!
  My take: tathimini ya miaka 50 iwe tunalinganisha baada ya mkoloni kuondoka tumefanya nini na siasa isitumike!
   
 3. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Tuna uhuru wa bendera - cha kwanza cha kujivunia
  tulishiriki kikamilifu kuwakomboa wenzetu waliokuwa bado chini ya ukoloni mkongwe - cha pili
  tunatawaliwa na chama kile kile kikijivua magamba kwa namna tofautitofauti ktk historia yake - cha tatu
  Tunauawa na dola letu wenyewe kiaina na kila mara - cha nne
  Usalama wa raia unategemea hali yako duni ya maisha. ikibadilika kidogo ujue ushakuwa target ya kila mtu kukumaliza - cha tano
  miji iliyoshindikana kupangiliwa - cha sita
  elimu yenye mitaala ya ajabu yenye nadharia zenye kuwalenga wanafunzi kukariri badala ya kutafakari - cha saba
  hospitali za umma ambazo ni hatari kumpeleka mgonjwa wako - cha nane
   
 4. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Tumeuza Tanganyika
  Hatuna Katiba
  Hatuna shule nzuri
  Mikataba mibovu hasa ya madini
  Siasa mbovu
  CCM imepoteza dira (Ujamma si sera ya ccm kwa sasa)
  Migomo mingi
  Mabingwa wa kuchakachua katika sadec
  Waongo wa kutupwa
  Amani na mshikamano feki
  Chuki kwa vyama vya upinzania
  Upandikizaji wa chuki za ukabila, dini NK
  Maisha Magumu kwa kila Mtanzania
  Bunge lisilojali maslahi ya umma
  Rushwa iliyokithiri
  Elimu kwa matajiri


  Na mengine mengi:pound:
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,847
  Trophy Points: 280
  CCM ionedoke t u na hakuna lingine w, wanaoitetea ccm hapa ni watoto wa wakubwa
   
 6. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ya kujivunia tunayo mengi. Ukijiflushia perfum unaisikia harufu yake mwanzoni tu, baadaye wewe huisikii bali wanaokujia karibu wataisikia. Unaponawa uso unajiona kwenye kioo mara moja, baadaye anayekuona ndiye atakayesema unapendeza au la.Mkeo unaweza kumwona hafai kabisa, lakini wenzako kila wanapomwona wanajigonga sana (na mumeo vivyo). Woga wetu kujaribu vitu ndio hulka yetu, kuogopa kwetu wanasiasa hutafsiri kama "AMANI na UTULIVU" Tunao uvumilivu kupita kawaida, Nenda Kenya au Kongo DRC hapa hapa karibu kwa majirani zetu au Burundi au Ruanda, utaelewa naeleza nini. Zaire askari ndiye kidume mahala popote na wakati wowote. Anapoingia kijijini mwana wa Kongo hupiga risasi hovyo hewani suruali lake likifungwa juu ya kitovu chake karibia nyonyo zake. Watu wanaulizana nani kidume huyo? Wakitoka kumwona wanammwagia sifa kwamba wamepata mtoto kwelikweli.

  Watanzania tunaambiwa tule nyasi na tunanung'unikia mvunguni. Sasa nikwambie, hata maswali yako unayouliza hapa, nchi nyingi huweza kuuliza ama sivyo kichwa sio chako. Sasa unaweza kumtukana rais wako na kusitokee neno, zamani ilikuwa huwezi kufanya hivyo. Waulize wahariri wa magazeti na Redio, habari haitoki mpaka Ikulu wameiruhusu kutoka. Kina Rostam wanaiba na kuibuka wajanja, yote haya miaka ya JKN angeswekwa ndani akaozea huko, maana angeitwa mhujumu uchumi anayestahili kuchapwa viboko akiingia gerezani na anapotoka gerezani akamwonyeshe mkewe. Leo UVCCM wanawasema kina Lowasa, Chenge na Rostam waziwazi eti wakitoe CCM, nani angesema maneno hayo zamani. Kweli tunayo mengi ya kujivunia Tanzania.

  Ushindwe wewe tu leo, ukitaka take a risk a nd you move foward. Zamani hufanyi hivyo, kumbuka yule mhindi aliyepewa masaa 24 kuondoka nchini alikuwa anatamba kwamba alikuja TZ bila senti hata moja lakini katika miezi 6 ni tajiri kupindukia. Tulipomtimua sisi, akapokelewa Zaire, sasa huko ni mungu mdogo kiuchumi, anaifadhili serikali. Unapotema wewe ukidhani ni uchafu, wenzako wanalamba dume na kukuchekea. Lakini tena, wengi tumesoma enzi za ng'walimu bure bureshi, tulipoona wasomi wanaongezeka tukaanza kuweka vikwazo ili kuwapunguza kasi, ndio maana leo lazima uwe tajiri ili kusoma au kusomesha mwanao. Ukibisha unaambiwa hustahili kuzaa, unatakiwa uhasiwe. Kwa nini tusijivunie yote hayo?

  Angalia, Muhimbili Medical School zama hizo maprofessa walikuwa wachache sana, ili uwe professa ilikuwa uandike papper tu kadha baada ya ddegree yako moja au mbili. Hao walipopata wakaanza kudhibiti wanaoibukia, wakaweka mkwara kwamba lazima pia uwe na PhD hata kama umepublish papper 10,001.265. tena maprofesa wengi waliochangamkia kuwa profesa wakati huo walikuwa wa coppy and paste. Ilikuwa kama unataka kufanya utafiti lazima upate kibali cha mwalimu wako, naye anakuambia ni lazima umwahidi utaliweka na jina lake utakapopublish kazi yako ama sivyo kafie mbali. Kwa hiyo wapo maprofesa ambao hata ukiingia kwenye mtandao hupati jina lake likiw first author, yeye ni wa 3 au wa 12 kwenye orodha ya authors wa papper fulani. Leo hii lazima kieleweke, bila PhD hupati uprofessa. Vijana wengi wanachangamkia, lakini vikwazo vinaongezwa kimoja baada ya kingine. Tunayo mengi ya kujivunia, kuna mambo ambayo yanawezekana kufanyika Tanzania tu na sio kwengineko duniani.

  Hapa Tanzania viongozi wa nchi hubadilishana uongozi kama njugu siku hizi, zamani haikuwa hivyo. Uliza Museveni atatoka lini madarakani kama hujakatwa kichwa. Lazima tujivunie. SImalizi hapa, bora niende uani maana nimebanwa na haja ndogo. Nikirudi nitaendelea.
   
 7. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hamna dalili ya kufika, nasema hatufiki, bora boda zifunguliwe watanzania watimue nje wakahangaike palipo na usalama, mtandao wa nyumbani hauruhusu mabadiliko yoyote, ubishi mwingi
   
 8. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 9. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2011
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  tunajivunia rais mbovu
  serikali mbovu,
  viongozi wabovu,
   
Loading...