1. Tuliotumbuliwa bila sababu- Tuna Jambo letu 28/10/2020
2. Tuliofukuzwa UDOM tukaitwa vilaza - Tuna Jambo letu
3. Tulioutwa mafisadi kisa tulimuunga mkono Lowasa- Tuna Jambo letu
4. Tuliopigwa kwa sababu ya korosho tulizolima kwa jasho- Tuna Jambo letu
5. Tulionyimwa fidia huko mbezi kimara - Tuna Jambo letu
6.Wafanyakazi tulionyimwa nyongeza ya mishahara- tuna Jambo letu
7. Tuliofikwa na maafa Bukoba tukatelekezwa - tuna Jambo letu
8. Tuliofikwa na maafa Arusha RC akabadili matumizi ya fedha za maafa- tuna Jambo letu
9. Tuliokatwa fedha kujiendeleza kwa maslahi ya Taifa- tuna Jambo letu
10. Tulionyimwa ajira - Tuna Jambo letu
11. Tuliofukuzwa kwenye viti vyetu wakapewa wasiojua uchungu wa chama - Tuna Jambo letu
12. Tuliopigwa mabomu kisa gesi- Tuna Jambo letu
13. Tunaokatwa na bodi ya mikopo mapesa kibao kisa sheria ya Bunge - Tuna Jambo letu
14. Tuliopata mimba tukazuiwa kurudi shule wakati watoto wa vigogo wakipata mimba wanapelekwa shule na vyuo vikubwa- Tuna Jambo letu
Hizi Ni baadhi ya hoja zinazokwenda kwa #tunajamboletu zinazosambaa mitandaoni.
CCM msizipuuze, zina Jambo Tarehe 28/10/2020