Enzymes
JF-Expert Member
- Feb 14, 2013
- 4,332
- 3,008
Heshima kwako moderators na wamiliki wa JF,
Heshima kwenu members wote wa status tofauti tofauti,
Naomba niongee na WanaMARA na Watanzania kwa ujumla (wakiwemo wabunge mizigo).
Wana MARA kwa ujumla na hasa hasa wananchi wa JIMBO la MUSOMA VIJIJINI (Musoma Rural) napenda kuwafahamisha kuwa Mbunge wetu mpendwa na Prof. msomi na mahiri (Miamba na madini), Sospeter Muhongo, ambae pia ni waziri wa Nishati na Madini amezindua Wavuti (Tovuti/website) ya JIMBO, amabyo ni www.musomavijijini.or.tz. Ktk wavuti hii kuna MATUKIO na Miradi mbalimbali inayo na itakayo tekelezwa ndani ya JIMBO. Kupitia Website hii utafahamu kinacho tokea Musoma VIJIJINI hata kama upo kwa OBAMA (USA). Pia waweza kushiriki ktk kuendeleza jimbo kwa kuchangia kwa hiari fedha au Mawazo. Ktk website hii kuna sehemu ya kuwasiliana na Waziri LIVE kwa kuuliza swali au kutoa maoni. BIG UP, Prof. Sospeter Mhongo.
Mhe: Prof. Sospeter Muhongo amechangia hadi sasa takribani vitabu 42,000 ktk shule za Msingi na sekondari zote JIMBONI kwake.
Pia Prof. Muhongo amekabidhi AMBULANCE 1 ktk kituo cha Afya Murangi kwa kushirikiana na Ubalozi wa Japan.
Waziri pia amemuomba Waziri wa Ujenzi na uchukuzi Prof. Makame Mbarawa kujenga barabara ya Musoma hadi Busekera (Maprofessa huwa hawatupani kashamkubalia-muda si mrefu tutakuwa na mkeka mrefu na wa maana).
Professa Muhongo pia amezindua Kilimo cha mpunga ktk Bonde la mto Suguti kwa kuwawezesha vijana na wanachi. Pia Mhe: katoa mbegu na Pembejeo nyingine kwa ajili ya Kilimo cha alizeti Bukima. Vile vile Mhe: ameagiza upembuzi yakinifu ufanyike haraka sana wa kuwazesha vijana kulima mbogamboga kandokando ya ziwa Victoria.
Professa pia, ktk juhudi zake hana mchezo kabisa na Elimu. Takribani madawati 8000 yanatengenezwa na SUMA JKT MWANZA. UCHANGIAJI UNAENDELEA KUPITIA website tajwa hapo juu. Shule za Bweni kwa vijana wa kiume na wa kike ziko mbioni kuanza ujenzi wa Mabweni.
Professa Muhongo kwa kuwa ni Waziri wa sekta Nyeti, yupo busy sn. Hivyo basi huwasili Jimboni karibu mara1 kwa mwezi. Kuhakikisha Jimbo halikosi uwepo wake, Mhe: Prof.S. Muhongo ameajiri vijana 5, wa kufuatilia utekelezaji wa miradi na shughuli mbalimbali za Jimbo. Ana walipa yeye binafsi , si serikali. Kawanunulia Pikipiki, Laptop, Modem, Vocha usiseme, na kuwa fungulia ofisi ktk kata mbalimbali. Mmoja yupo Mugango, mwingine, Murangi, Mwingine Busekera, Mwingine Saragana na Mwingine Nyakatende/Ukwayani.
Ni huyu huyu Prof aliye saidia kwa wananchi wa Mara nzima (hasa Majita) kufikiwa na mradi wa REA kwa uharaka, na kwa ufanisi mkubwa akishirikiana na TANESCO musoma. Hili limechochea sana ujasiliamali na vitega uchumi kwa wananchi, hivyo vipato kuongezeka. Vituo vya kuhifadhi samaki kujengwa, nk. (SHAME ON YOU , JOSEPH MSUKUMA UNAYE CHUKIA UMEME).
Nawaomba wanaMARA na wana Musoma Vijijini tuwe na subira, maendeleo hayaji kama mvua bali taratibu na kwa mikakati madhubuti.Tatizo JIMBO LILIKUWA LIMETELEKEZWA, maendeleo yalikuwa ya Upande mmoja tu. Mm nilihudhuria kikao chake cha kujadili Malengo na Maendeleo ya Jimbo mnamo tarehe 23/12/2015 pale MURANGI (Makao makuu mapya ya Wilaya/Jimbo) kweli ana nia ya dhati kwa JIMBO letu, ni mizuri sn.
Najuta sana kwa kuchagua wabunge Wakaa ofisini kwao na si Bungeni kwa miaka iliyo pita hasa 2005 hadi 2015. Mbunge haongei kero za wanachi wake, yeye kila kukicha Madini na Gesi kwa matakwa yake binafsi: Shame on yuo, you LAWYER!! Nachukia sana Wabunge, hasa wa CCM ambao kazi zao ni kusodoa UKAWA badala ya kujikita ktk kuchangia hoja na kuwasilisha matatizo ya wananchi wao!!
Rai yangu kwa Wabunge wengine igeni mfano wa huyu mheshimiwa. Ni awamu yake ya kwanza kama Mbunge wa Jimbo. Budget yake ya kwanza ni ya July 2016/2017. Kuna wabunge wana miaka 20 Bungeni kata mita 5 ya lami hawezi kuonesha wananchi wao!!
Mzee wa HAPA KAZI TU (JPM) anamng'ang'ania kwasabaubu anafahamu fika utendaji kazi wake.
Porojo pelekeni baa za wanzuki!!
Nisiwachoshe sn wana Musoma VIJIJINI. Nawaomba tumuunge mkono Prof. Sospeter Muhongo kwa maendeleo endelevu ya JIMBO la Musoma Vijijini. Changia Dawati kupitia www.musomavijijini.or.tz.