Tumsikilize nani, tumwelewe nani?

Tumsikilize nani, tumwelewe nani?

MANILABHONA

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2015
Posts
462
Reaction score
351
Nimeangalia taarifa ya habari moja siku za hivi karibuni nikashindwa kuielewa: Ilihusu sehemu moja inaitwa Kibondo nafikiri huko ni Kigoma.

Habari iliwaonesha nadhani Mwenyekiti wa halmashauri, kiongozi wa wananchi na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya wakilalamika kuhusu mauaji ya raia,uporaji unyanganyi, utekaji, ujambazi kwa ujumla.

Wakitaja maeneo ya Busunzu, Mabamba na Barabara ya Kakonko kuwa ndiyo vitendo hivi vimekithiri.

Sehemu ya pili ya taarifa hiyohiyo ikamuonesha nafikiri ni RPC wa mkoa huo akisema hali imedhibitiwa ni shwari na wameua majambazi watatu.

Nikiwa raia wa kawaida nimwelewe nani au nishike lipi---Hali ni shwari, imedhibitiwa au Ujambazi umekithiri huko Kigoma ????
 
DC wa kule nahisi wameacha kuchukua wanajeshi kama zamana maan na shida... Nilmskia mtu mmoja akisema ni kibiti ya pili... Tatizo pia linachangiwa na kua karibu na burundi na makambi ya wakimbizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huku kusikie hvyovyo tu ndugu yangu n zaid ya Somalia

Sent using Jamii Forums mobile app
Hee siamini masikio yangu na ninachokisoma hapa, nchi hii hii ya Tanzania yenye amani tele kuna sehemu zinafananishwa na Somalia au kuitwa Kibiti ya pili. Au mmeshajitoa kwenye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pengine mko nchi yenu nyingine. Hii inawezekana kweli na IGP wa Tanzania yupo yupo tu. Yataka moyo
 
Back
Top Bottom