Mungo Park
JF-Expert Member
- Sep 14, 2010
- 2,112
- 1,831
Nimefungua huu uzi ili kuweza kumshauri Naibu Waziri Hussein Bashe katika Wizara yake ya Kilimo. Kama alivyosema Kilimo ni Biashara lakini Kilimo kina changamoto za kutosha ambazo Watendaji na Mawaziri ama hawazielewi au hawazitilii maanani.
Huu ni ushauri tu kwa Naibu Waziri Bashe. Akiuzingatia tutakwenda mbele, akipuuza atakuwa kama Mawaziri wengine waliopita.
Katika Tanzania Kilimo kinachangia asilimia karibu 29% katika GDP na Watanzania karibu asilimia 65.5% - 70% ni Wakulima ama wanajishughulisha na bidhaa za Kilimo. Nitatumia neno Asababishe kwani najua Waziri ndiyo yupo juu yake.
Ushauri wenyewe ni huu..
Huu ni ushauri tu kwa Naibu Waziri Bashe. Akiuzingatia tutakwenda mbele, akipuuza atakuwa kama Mawaziri wengine waliopita.
Katika Tanzania Kilimo kinachangia asilimia karibu 29% katika GDP na Watanzania karibu asilimia 65.5% - 70% ni Wakulima ama wanajishughulisha na bidhaa za Kilimo. Nitatumia neno Asababishe kwani najua Waziri ndiyo yupo juu yake.
Ushauri wenyewe ni huu..
- Asababishe kufanyika kwa sensa ya maeneo ya Kilimo Tanzania(kwa kiwango cha kata) na mahitaji yao.
- Asababishe yale maeneo maarufu kwa Kilimo yana angalau matrekta 2 kwa kila kata yakiwa na vifaa vyake kama majembe,'planters','harrows',harvesters',n.k. ili wakulima waweze kulima kwa bei nafuu na kwa haraka Zaidi.
- Asababishe Mbolea inafika maeneo ya mashambani kwa wakati kabla ya msimu wa kupanda.
- Asababishe mawasiliano na Wizara ya Nishati ili kujua ni kwa nini Mbolea ya Minjingu haipendwi na Wakulima na madhara yake.
- Asababishe utoaji wa haraka wa Pembejeo za Kilimo Bandarini ili kuwahi misimu ya Kilimo.
- Asababishe kuanzishwa kwa ofisi ndogo za Wizara ya Kilimo Mipakani ili kurahisisha utoaji wa Vibali vya mauzo ya mazao nje.
- Asababishe kurahisisha biashara ya Mazao nje hasa nchi jirani.
- Asababishe kuangaliwa kwa utaratibu mzuri wa kurudisha hela za Sukari('15% Import Duty Refunds') kwa viwanda vikubwa kwa kuwa Viwanda vinataabika sana na vingine viko mbioni kusimama. Hili ni kubwa kwani linaathiri utendaji wa baadhi ya Viwanda.
- Asababishe kuundwa kwa Kamati ya Uratibu ya Wizara ya Kilimo, Viwanda(SIDO) na Fedha ili kutatua changamoto zinazojitokeza katika shughuli za Ujasiriamali na Viwanda vidogovidogo.
- Asababishe kuanzishwa kwa Idara ya Masoko ambayo itafanyanya kazi na Bodi za Tumbaku, Sukari, Chai, Korosho, Pamba, Kahawa, Katani, Pareto, Nafaka na Mazao Mchanganyiko ili kupata masoko katika Nchi Jirani na penginepo na taarifa kupatikana mtandaoni - E-Masoko.
- Asababishe upitiaji upya wa ufanisi na uongozi wa Bodi hizi.
- Asababishe upatikanaji wa mapema na kwa haraka kwa Takwimu za Mazao ya Kilimo kwa mtandao - E-Takwimu.
- Asababishe Uondoshaji/Upunguzaji wa vizuizi vya barabarani kwa mazao ya Kilimo.
- Asababishe elimu zaidi, matumizi na matangazo kuihusu 'Tanzania Mercantile Exchange Plc'.
- Asababishe Serikali kununua ziada ya mazao toka kwa Wakulima.
- Asababishe uangaliwaji kwa jicho la upendeleo Sekta ya 'Horticulture' kwani inataabika sana hasa biashara ya maua n.k.
- Asababishe uanzishwaji wa utaratibu wa mara kwa mara wa kukutana na Wakulima ('Round Table') ili kufanya utatuzi wa haraka wa matatizo yao.