Tumshauri mdau anaomba ushauri

Tumshauri mdau anaomba ushauri

NANCA

Member
Joined
Jun 23, 2023
Posts
92
Reaction score
100
Mdau anasema alimuachia mkewe mwekundu wa msimbazi kama makadirio ya gharama za matibabu ili ampeleke mtoto mchanga hospitali ya serikali kutokana na mafua. Mdau aliporudi kutoka kazini akamuuliza mkewe Kama alimpeleka mtoto hospital, na maongezi yakawa Kama ifuatavyo:

Mdau: Wamesema shida nini?

Mke: Hawajaona kitu ila wamemwandikia dawa za kunnua

Mdau: mh! Kwani umetumia sh.ngap?

Mke: 6000

Mdau: Mh! Mbna nanusa harufu ya samaki , umennua samaki?

Mke: eeh ile 4000

Mdau: aa sawa, embu nipe hyo bill ya dawa nikannue.

Mke: leo tunakula nn? Tule ndizi?

Mdau: Chochote. Basi mdau akatoka akaenda mishe zake
- Aliporudi akakuta ndizi, samaki ya zaidi ya 4000 na chachandu. Bc maongezi yakaanza upya

Mdau: Vp, leo umetumia sh. Ngapi hospitalini, hizi samaki ni 4000, maana naona ndizi afu sjatoa hela.

Mke: eeeh nshachoka na maswali, hakuna gharama iliyotumika hospitali, watoto wachanga hawalipi kitu.

Mdau: Mbna nlipokuuliza hukusema?

Mke: Hukusikia na kwani huelewi.

Mdau: Kwan ngekua naelewa ngetoa hela ya matibabu, au ngesema nianze kumfuatilia bima sasa? Mbna unakua muongo? Au unadhani ungesema labda ngekwambia lete hyo hela, mbna bado hujanielewa na kunisoma kua napenda ukweli?

Mkee: eeeeh maneno maneno nshachoka
-Sababu ya mdau kumuuliza uliza mke ilikua ni kutaka kujua je hyo bajeti ya ziada imetoka wapi, isije ikawa mke amechota hela za biashara maana mwanamke ni mpenda vitu vizuri sema jamaa anamkazia na kumbana mbana ktk bajeti.

Sasa mdau ananiomba ushauri kua amechoshwa na gubu la mkewe na tabia ya kupindishapindisha maneno na anafikiria kuachana nae, jumlisha mwanamke ni wakujiliza sana kwao na kupenda sana kwao kuliko kwake. Mdau anadai amechoka. Hivyo kabla hajachukua hatua anaomba ushauri
 
Ila vijana wa siku hz mnakosa sana uvumilivu...sasa hapo tatizo la kumuacha mke lipo wapi???

Ndyo maana mnaambiwa wanaume muoe mkiwa walau na 30+ sasa hapo mwanaume wa 2001 mke 2003 kelele zitapungua ndani kweli
 
Sasa hapo ni Samaki na vi bill vya Alf kumi,

Mwambie aache kumanage details mahusiano ya ndoa sio ya watoto wadogo...

Unapotezea likija la kibabe sana ndio unafanya maamuzi.... asidhani watu walikuwa wa bibi na wababu kwasabab ya tabia njema,

Ndoa ni kuvumiliana mengi mno, Lakin zaidi mwambie apambane aongeze kipato.
 
Mambo ya ndani kwa mdau na samaki wao umeyajuaje? Tena unaelezea A-Z?? We ndiyo huyo mdau, au ni jirani mbea ulikuwa unachungulia dirishani mwao?

Mwambie mdau tukiendaga sokoni uwa tunapewa samaki na ndizi za bure
 
Tajiri Mzee hazeeki machoni pa Wanawake!

Mdau aache au apunguze Umama.

Hamna Cha kutaka kujua hiyo nyingine Wala nn, mdau anahisi mkewe anahongwa!.

Mdau anachokitafuta atakipata!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom