Tumshahuri Rais

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,680
8,868
Kutokana na hizi tuhuma zinazo muandama Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam hazina budi kuangaliwa upya,kutokana na kugubikwa na mambo mengi yenye ukakasi sasa yampasa Mh Rais kutoa maamzi magumu! japo yatamuumiza,kuna kila dalili kuwa hizi kashifa zinamchafua Rais wetu kutokana na hizi tuhuma zilizotolewa katika mitandao ya kijamii maana hata hii mitandao ya kijamii siyo yakubeza!kuhusu mali anazomiliki na utata juu ya usajili wa hizo mali na na mjina hakuna shaka kuna uchafu umegubika swala hilo!tuache mambo ya vyeti ila katika utumishi wa umma nilazima uwe msafi na kwakuwa hajadhibitisha basi kuna ukakasi katika vyeti.Mh Rais kuendelea kufunika kombe nikuendelea kujaza funza katika kombe hilo lilofunikwa.Japo yawezekana kuna dhana kuwa wanaomwandama ni wapinzani au wabaya wake na wale wanaodhoofisha vita dhidi ya madawa ya kulevya ila kwa maneno yaliyopo tafunta njia nyingine huyo kijana kwa sasa asafishiki.
Huo mimi ndiyo ushauri wangu kwa Mh Rais wangu najisikia vibaya nikipita mtaani nakuzomewa kuwa tumeshindwa kutoa maamzi ila ukweli unao wewe.
 
hivi unapotaka kumshauri rais unamaanisha nini?

inamaana mmesahau kwamba kushauri unahaki ya kukubaliwa ama kukataliwa?
mangapi mmeshauri afu hayajakubaliwa afu leo hii mwone hili la makonda litasikilizwa.
acheni kupeta pumba kwenye upepo.
jitizameni nyie na nafsi zenu.
afu sitoshangaa apo baadae nikaskia mmeichagua tena CCM
 
Hili la Makonda/Bashite litamgharimu Magu akiendelea kulifumbia macho.atambue kuwa nchi hii ina watu 50 m na wote wanamlilia Mungu ili watawala wetu watende haki kwa raia wote.Endapo watawqla hawa watapuuza kutenda haki, maombi haya ya watanzania yatageuka laana kwao.
 
Ukitoa ushahuri hautakiwi kuchoka hivyo niyule anayeupokea na mimi kwakuwa ni muumini mzuri wa Serikali yangu na Rais wake JMT na katiba inaruhusu kutoa uhuru wa mawazo basi mimi nanitaendelea kushauri kupitia platform hizi maana ndiyo sehemu pekee naweza kukutana na Mh Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hili dada yangu na rafiki wa siku nyingi gfsonwin naomba nikueleze haya niliyoyasema kwaleo na kuichagua CCM ni imani ya mtu na mimi nitaendelea kuichagua mpaka kwakuwa na mimi ni muumini wa CCM.
 
unafkir hata mimi napinga kuchaguliwa kwa CCM?
ichaguliwe tuu ila sioni haja ya kupoteza muda kutoa ushauri ambao hata kusomwa tu hausomwi.

hivi unadhani kungekuwa na kitu cha kumshawishi rais kutokana na tuhuma za makonda angekuwa amekaa kimya hadi leo?
lazima angekuwa ameyafanyia kazi sasa inapotokea kwamba amekaa kimya na mnamshinikiza afanye yale mnayotaka nyie afanye basi ndo mana anakaa kimya. na hata mseme vipi hawasikilizi
 
Nikweli lakini sisi tumetimiza wajibu kinacho baki ni yeye kuuchukua au kuacha maana Urais ni taasisi ina washauri wa kila idara.
 
Back
Top Bottom