Tumrudishe Msigwa tena bungeni

Hapo si kanisa la Nyumbani kwake Ina maana hayo mabango ameyabandika nyumbani kwake yote hayo...?
 
Msigwa juzi tu amepata ubunge amefungua Yard Ya Kuuza Magari Iringa.. Pesa kapata wapi,,ni fisadi sana
 

Hao wadada walioshika vipeperushi amewahonga sh. ngapi?
 
ni
Ni lazima tumrudishe mjengoni!!

Kweli bora arudishwe bungeni ili Iringa iendelee kuonekana bungeni maana majimbo mengine ya Mkoa wa Iringa kama vile hawana Wabunge. Mfano Kalenga yaani kimya kabisa. Iringa Wabunge waliovuma ni Msigwa na Filikunjombe ila sasa Filikunjombe yupo Mkoa mwingine. Mkichagua ccm wabunge wao huwa wanapewa fikra za Mwenyekiti za kwao wanaziacha kwenye majimbo na ndiyo maana kazi kubwa kabisa pale bungeni ni kusema ndiyoooooooo! kazi ambayo hata chekechea wangeifanya na wakalipwa posho kidogo tu.
 
Wapiga kura wa Iringa mtakuwa hamjatenda haki kabisa kutomrudisha mjengoni mchungaji Msigwa. Shime mpeni kura za kutosha arudi bungeni. magamba tupeni kule
 
Huyu ni aina ya mmbunge makini kabisa,Wana Iringa tunamuhutaji sana Msigwa,huyu si wa Iringa tu ni wa nchi nzima.
 
Nalikubali sana jembe langu hilo, Mch. Msigwa.
Ni jembe kuliko hata Ma-Solex, sema tu hajapata fursa ya kusimamia wizara katika serikali kuu. Akipata nafasi ya kuwa ndani ya serikali, nchi nzima watamkubali.
 



Uko sahihi kabisa kamanda..Msigwa ni moja ya wabunge nawakubali sana sababu huwa anazungumza facts sana akiwa mjengon..wairinga by hooks and cooks huyu tumrudishe mjengoni...all the best Jembe msigwa!!!
 
umeona eee!!
 
huyu jamaa si ndio alihoji kwanini zanzibar mchana migahawa inafungwa wakati wa ramadhan , inaelekea inamuuma sana na ingekuwa amri yake angeamuru waislam wasifunge...

ni mdini sana... yaana anachuki za wazi kwa waislam ....

anyways sishangai ni mchungaji .... na ndio maana hatufanyi makosa kumuweka padri slaa madarakani ni hatari kwa taifa
 

Hiyo siyo point Tanzania nchi huru, kufunga kwa mwingine hakuzuii mwingine asile. Tz is neither a Christian nor Islamic nor Pagan. Tia akili, Msigwa arudi tu.
 
Naweza nikasema nihamasa ya wana Iringa kumuunga mkono mbunge wao mchungaji peter Msigwa kwa haiki hii ya watu

Ndugu mchungaji wangu jiandae tu kwenda tena bungeni


Wanairinga wamethibitisha kuwa wanakupenda yani Iringa nzima habari ya mjini ni CHADEMA na ukawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…