Tumpimeje mwanasiasa wa tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumpimeje mwanasiasa wa tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, Jun 8, 2012.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mara kadhaa siasa za Tanzania zimekua na kukua huku badhi ya vyama vya siasa vikijipatia umaarufu na vingine umaarufu wake ukipungua na hata vingine kufa kabisa. Mimi binafsi sifurahishwi na namna siasa za Tanzania hazimtendei haki huyu mtu wa chini kabisa. Vyama vya siasa vimekuwa na mbwembwe nyingi wakati wa kambeni , vingine vikitumia lugha ya jimbo fulani kukombolewa hasa pale ambapo mabadiliko yanapotokea katika jimbo husika.

  Je, kuna tofauti yoyote kati ya wananasiasa wetu? je kuwa maarufu wa kuongea katika majukwaa ya siasa na bungeni ni kigezo tosha cha mwanasiasa kuwa na uwezo zaidi ya wenzake?

  Nauliza maswali haya kwa makusudi kabisa kutokana na ukweli kuwa sioni maisha ya mtanzania wa kawaida wa jimbo fulani yakibadilika baada ya mabadiliko ya uongozi katika jimbo husika . Nina maana sioni tofauti ya maisha kati mwananchi wa jimbo la KAWE/UBUNGO yanayoongozwa na CHADEMA na mwananchi wa majimbo ya SEGEREA/UKONGA/ ILALA nk yanayoongozwa na CCM, KARATU/ARUSHA yanyaoongozwa na CDM na mwananchi wa MONDULI/NGORONGORO yanayoongozwa na CCM. Nauliza tena ni nani mwanasiasa mwenye uwezo ?

  Napendekeza tupime uwezo wa wanasiasa wetu kwa namna ambavyo wanaleta mabadiliko ya maisha ya mwananchi wa hali ya chini katika maeneo walipo na siyo kwa namna ambavyo wanaongea bungeni au wanavyoifedhesha serikali iliyoko madarakani au namana ambavyo wanamdanganya mwananchi kwa maneno matamu huku maisha yake yakiwa duni tena kupita kiasi ukilinganisha na awali.
   
Loading...