Tumpe 'sapoti, Spika Ndugai kwenye mapambano yake, madaraka hunoga

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Kuna watanzania (wanaofuatilia na kushiriki siasa za nchi hii) wanakosoa mambo anayoyafanya Spika Job Yustino Ndugai hasa kuelekea kwa CHADEMA, Wabunge wa CHADEMA na viongozi wa CHADEMA. Wanamuona Spika Ndugai kama aliyepotoka na kukengeuka. Hawampendi.

Wapo wanaoziona chuki za wazi za Spika Ndugai kwa CHADEMA na wanaohusika na chama hicho Bungeni. Tangu 'aagizwe' kuwashughulikia wapinzani Bungeni, Spika Ndugai amekuwa akijitahidi kufanya hivyo. Lakini, kadiri muda unavyoyoyoma Spika anajipima na anaona kupelea.

Spika anakimbizana na Juni 18. Anakimbizana na mwisho wa Bunge ambapo Rais na Mwenyekiti wetu wa Bunge atalihutubia na kulivunja rasmi Bunge. Inatabiriwa kuwa Rais na Mwenyekiti wetu atasema jambo kuhusu uchaguzi na utendaji wa Spika. Na labda ahadi ya kuwa Spika tena itatolewa. Lazima kujipanga.

Kujipanga kisawasawa. Kupambana kisawasawa. Kujitokeza front kwelikweli. Ndiyo maana Spika Ndugai kwasasa yuko alivyo. Amekuwa Msemaji wa Bunge; Msemaji wa Wabunge; Msemaji wa CCM; Msemaji wa Rais na Ikulu na kadhalika. Atafanyaje? Hana jinsi. Mbowe na watu wake wamvumilie Spika Ndugai kwasasa. Anapambania mustakabali wake.

Kuna watu wanatajwatajwa chamani kumrithi Jimboni au kitini. Kuna watu wanasema watapewa msaada mkbwa kuwa Wabunge ili Spika awe mpya. Katika hali hiyo, Spika Ndugai kwasasa lazima aweke uelewa pembeni. Aangalie kwanza maslahi yake. Uspika si mchezo! Spika ana marupurupu kuliko mataputapu; ana ulinzi kuliko wazinzi; ana raha kuliko karaha. Si rahisi kuupoteza u-Spika!

Tumpe sapoti Spika Ndugai. Tumshangilie na kumuunga mkono kwakuwa ana maono. Anaiona Juni 18. Anaiona hotuba ya Rais na Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa Bungeni. Anaziona kauli tamu zisizo na damu za Rais na Mwenyekiti. Anaona anatakavyosifiwa kutekeleza agizo la kuwashughulikia wapinzani Bungeni. Atafurahi na kupata amani. Kwasasa hana.

Corona ipo na inaua, tuchukue tahadhari!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha, Tanzania)
 
Cheo kizuri ,si unaona wengine wameanza kulia bungeni baada ya kuona hana uhakika wa kuwa mbunge tena sasa wanaomba Huruma kwa/za spika.Spika na yeye lazima aendelee kusaport anachosupport kukaa kijiweni kugumu asikwambie mtu kwa wanasiasa.
 
Atupishe kwanza ameshajichokea
Hawezi kwendana na kasi ya vijana,tena ashukuru mbereko ya JPM Nina uhakika vijana wa Upinzani bunge lijalo hawatokuwepo kumnyoosha
 
Tunaliona hitaji la kuboresha katiba yetu. Ni jambo la hatari sana kama taifa kutegemea hisani na muongozo wa mtu mmoja, Rais na mwenyekiti wa chama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom