Tumpe nchi kwanza moise katumbi

Tumpe nchi kwanza moise katumbi

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,793
Reaction score
5,053
Unajua wa Afrika mara nyingi tunakosea kupata viongozi imara kwasababu ya ushabiki wetu
Mtu anaweza kujua kabisa huyu bwana credit yake sio nzuri lakini atapenda kutumia ushabiki wake kumchagua tu ndio maana mara nyingi tunachagua viongozi ambao sio sahii
Ila ikiwa tutaanza kutumia akili kuchagua kiongozi imara na amini Afrika tutaendelea saana
Unajua DRC tunahitaji saana moise katumbi kuliko moise katumbi anavyohitaji DRC lakini kwasababu ya ushabiki wetu basi wote tuseme felix anatakiwa kupewa miaka mitano mingine tena

Lakini wenye akili sisi tunaona kabisa hii nchi ata tukija kufukuza wanyarwanda wote ndani ya nchi tutabaki na vita hivi vya makabila
Leo hii kwasababu raisi ni mkasai wakasai wote wanafanya kila asiye msapoti ndugu yao huyo sio mtoto wa nchi huyo ni mgeni huu ni ukabila na upumbavu
Sheria ya ili uwe mkongomani halisi unatakiwa uwe mkongomani wa baba na mama hii ni sheria ya kibaguzi kwani wao hawajui kama kuna wakongomani ambao wameoa wanawake wengine kutoka katika mataifa mengine kwa hiyo watoto wao wataishi kama wageni katika nchi hii
Watu kama wameshindwa kuunganisha watu na kulinda amani ya nchi si bora wa ondoke madarakani tu kuliko kungangania madaraka ambayo wanaona hawayawezi kabisa
Mbona moise katumbi kipindi yupo gavana aliweza kuunganisha wakasai na wakatange na haya ndo makabila ambayo kabisa ni kama moto na maji mpaka sasa kuna wakasai wanazungumza Kiswahili cha katanga kwanini wasitumie njie ile aliyo tumia katumbi kuunganisha hawa watu kuliko kubagua watu wengine

Uvira watu walikufa na maji wakapoteza familia zao na nyumba zao hakuna walicho kipata kutoka kwa serikali ya Kongo zaidi ya pole tu wakasai kule Kongo wamepata hayo hayo majanga wamepewa kila mtu dollars 1000$ huu ni ubaguzi kuthamini baadhi ya watu fulani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaeni kwa kutulia.

Kanisa katoliki linamtaka Martin Fayulu(na hata last time alishinda huyu wakamchakachua) na round hii atapigwa chini tena.

Moise atapigwa zengwe Kama kawa

Tshisekedi by hooks/crooks atashinda uchaguzi huo.
 
Huyo jamaa anautaka Urais sana alianzia kwenye Timu ila lengo lake lilikua huku kwenye siasa sema kwa jinsi alivyochanganya Uraia mara mzambia sijui Muisrael hapo naona patamletea shida kidogo ngoja tuone game inakwendaje...
 
Back
Top Bottom