Tumia nguvu zako ungali kijana.

Tumia nguvu zako ungali kijana.

jf user

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2018
Posts
777
Reaction score
625
Naweza sema katika miaka ya ubora ya binadamu basi ni ujana wake kwa sababu anakua na nguvu kimwili na kiakili.
Ndio maana wacheza mpira wengi wanakua hot sana kuanzia miaka 15 hadi 35 atakae zidi hapo basi ana mfupa mgumu na ni blessed kama buffon
Tukija kwenye fani nyingine kama boxing, mbio, kuogelea, kuendesha magari, baiskeli, tennis na almost michezo yote ya kuruka ruka ni ya vijana kwa sababu wanakua active. Wakivuka 40 ndio kwa heri mwili unaanza kuchachamaa.

Uzeeni ni miaka ya taabu na mateso kama hukujitaftia kwenye ujana wako andika maumivu kwani uwezo wa kutoboa uzeeni ni mdogo sana labda ujaliwe na MUNGU. Wengi hawafiki huko kutokana na magonjwa, stress za maisha, dhambi na laana.
Mwili unakua umechoka viungo na sehemu za mwili zinakosa ushirikiano kwa waliosoma bailojia ya mwili wa binadamu watanielewa hapa.

Ni vyema hata ukijaliwa umri ufurahie kazi za ujana wako kuliko kujikokota ukisaka tonge.
Kama kijana ni muda wako sasa kupambana na maisha! Ukishindwa hapa basi jua utapoteza, ukiwekeza kwenye ngono basi magonjwa yatakuchukua vivyo hivyo na dhambi nyingine ukiwekeza huko lazima zikuchukue mapema kabla ya siku zako za kuishi ulizopangiwa na MUNGU hapa dunia uzuri MUNGU kakupa uhuru wa kuchagua upendacho kwa sababu MUNGU wetu sio mchoyo wa fadhila sasa utakayochagua ndiyo utakayovuna.
MUNGU awe nanyi... Maisha ni sasa huko mbeleni hakuna ajuaye kama atafika kwani ni prediction so enjoy praying to your GOD, enjoy life and work hard for now or tomorrow if GOD wish.
 
Nakubaliana na wewe, ila sijaelewa vizuri kivipi uzee ni nyakati za mateso
 
Nakubaliana na wewe, ila sijaelewa vizuri kivipi uzee ni nyakati za mateso
Mwili unakua umechoka viungo na sehemu za mwili zinakosa ushirikiano kwa waliosoma bailojia ya mwili wa binadamu watanielewa hapa.
 
Back
Top Bottom