Tumesubutu, tumeweza kwenye miundombinu na uchukuzi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumesubutu, tumeweza kwenye miundombinu na uchukuzi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by babalao 2, Aug 2, 2012.

 1. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #1
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,218
  Likes Received: 1,271
  Trophy Points: 280
  Kila siku viongozi wetu wanatuimbia wimbo mzuri ya kuwa miundombinu ya nchi iko imara na ya kujivunia. Sasa ktk hali ya kawaida tukiangalia shirika la reli linakatisha tamaa hali yake sio nzuri kabisa, Kwa toka enzi za mkoloni mpaka leo tumeshindwa kuunganisha angalau Mikoa yote Tz Bara kwa mtandao wa reli. Sasa ni vp tutaweza kuunganisha mtandao wa reli na nchi majirani kama ndani tunashindwa nje tutaweza? Hivi ndio ilani ya ccm inataka kutudanganya WaTz? Tukitazama usafiri wa ndege tujivunie kutoka ndege 9 hadi sifuri mpaka mkodisho mwisho tumeshindwa hakuna kitu tena. Hapa ndiyo unakosa jibu maana wanatuambia uchumi unapaa 9 mpaka 0 tunapaa kweli? Huko kwenye usafiri wa majini ndiyo hakuna kitu si meli wala bandari chenye kuleta ufahari kwa nchi yetu, hebu tazama mshindani wetu ambaye ni bandari ya Mombasa hakuna kulala mpaka sisi wenyewe tunaitumia sasa hii nini maana yake nani kikwazo chetu ktk kufikiri kwetu tunakosea wapi mbona ziara za kujifunza nje kila siku zipo kwa viongozi wetu jamani! Nimalizie na barabara hapa napo ni fumbo maana leo kumfikia mzalishaji aliyeko kwenye baadhi ya maeneo ya Wakulima na Wafugaji ni mtihani mwingine, barabara zinapitika kwa muda mfupi kwa mwaka tena zikiwa ni mbovu ajabu sasa hii ndiyo tanzania ya kupaa kiuchumi? kwa nn ushauri wa Wataalam unakuawa nyuma ya Wanasiasa wanaojijali na koo zao? Je Watanzania tukae kimya tuangalie wanavyoua miundombinu yetu? Uchukuzi kwenda nje ya nchi na ndani utafanikiwaje kama miundombinu wanaimaliza? Tumesubutu, tumeweza na tunasonga mbele kweli? Sasa tupaze sauti kwa pamoja tuseme Tanzania sio nchi changa tena kama mmeshindwa kaeni pembeni Tunataka mawazo mapya ya vitendo viva Tanzania. Tunashindwa kwa nini? Maoni yako tafadhali.
   
Loading...