Billal Saadat
Senior Member
- Nov 30, 2022
- 169
- 356
Wengi wakubwa wapo humu ila wamesahau tumeshawahi kuunda Tume ya kuchunguza ucheleweshaji wa mizigo bandarini, foleni ndefu ya malori bandarini. mkitafuta mtaona haya yote.
Ucheleweshaji wa mizigo bandari yetu ya Dar umechangia hata kiwango cha forodha kuwa juu kulinganisha na bandari ya Mombasa hata wafanyabiashara wetu ndani walikimbilia Mombasa ukienda Kkoo wengi watakuambia juu ya hali hii, Mwanza pia.
Ukanda wa Afrika mashariki una njia mbili za Usafirishaji kuna njia ya Kaskazini inayounganisha Bandari ya Mombasa kwenda Uganda kupitia mji wa Malaba na Busia.
Njia ya pili ni njia ya kati inayotoka Dar es salaam kupitia Bukoba kwenda katika landlocked countries ambazo ni Uganda, Rwanda, Burundi na Mashariki ya jamhuri ya Congo.
Kwa muda mrefu na ukweli uliowazi Mombasa imedominate karibia asilimia 60 ya mizigo inayosafirishwa kwenda Congo, Uganda, Burundi na Rwanda sababu ni ucheleweshaji wa kupakua na kushusha mizigo katika Meli na mlundikano wa makasha katika gati zilizokuwa chini ya TICTS.
Kwa Takwimu za bandari yetu Meli huchukua siku tatu au nne katika kupakua na kushusha mizigo kwa zama hizi hatuwezi kuwa mshindani wa namna hii katika nchi ambazo wanashindana nasi kama bandari ya Mombasa.
Hali ya kisiasa isiyotabirika katika njia ya Kaskazini ni mwanya kwetu sisi Tanzania kwasababu wakati wote nchi zisizokuwa na bandari zitakuja kwetu je tumejipanga vipi ukipata mshirika kama DP World ni kuokota embe kwenye mzambarau.
Rais Samia ni hofu kwa kwa nchi shindani wameona move zinazofanyika katika awamu hii ya sita katika kukapitalise mapato ya bandari. Kama tukiweza kuisimamia bandari asilimia 60 ya mapato ya nchi yatatoka bandarini na hii ndiyo inaenda kutokea si mchezo.
Rais Samia Ametengeneza diplomatic activity katika nchi zisizokuwa na bandari amesafiri kwenda Rwanda, ameshafika Uganda, Ameshafiki Burundi na Ametembelea Congo hawa ndiyo wateja Wakuu wa business cargo kwa asilimia 80 hatuwezi kuwapoteza ni wakati wetu huu.
Kwa kipindi cha miezi saba Wakuu wa nchi zote hizi za Landlocked wanefika Dar es salaam au kukutana kuimarisha ushirikiano wa kibiashara zaidi kuhusiana na mizigo ya bandari. Huku Serikali ikiwa imempata mbia ambaye anakuja kufanya biashara kwa wepesi zaidi.
Tanzania imefanya mikakati mikubwa kuhakikisha inabakia kuwa namba moja mbia wa kibiashara kwa nchi zinazosafirisha mizigo yake kupitia bandari ya Dar es salaam.
Serikali inahakikisha reli ya kisasa ya SGR kutoka Isaka hadi Kigali na inajengwa na ujenzi upo katika asilimia 25 hali hii inaiweka Bandari ya Mombasa matatani hawatapenda haya yatokee.
Tanzania imeongeza kina cha bandari kuhakikisha tunaweza kupokea Meli kubwa za mizigo hii pia ni kaa la moto kwa bandari ya Mombasa. Ushindani wetu unabakia katika muda na uharaka wa kushusha mizigo na marketing ya kuwafanya wateja wengi kuja kutumia bandari ya Dar.
Kuiendeleza bandari ya Kigoma na kuimarisha bandari Kavu ya Isaka kunaifanya bandari ya Mombasa kuendelea kupata Changamoto dhidi ya bandari ya Dar es salaam. Kutakuwa na uharaka wa Usafirishaji wa mizigo kutoka Isaka kwenda Uganda, Rwanda, Burundi na Congo.
Serikali imeimarisha miundombinu ya barababara ni eneo dogo la kilometer 30 kutoka nyakanazi hadi lusahunga lenye kuhitaji maboresho asilimia 85 ya Barabara katika njia ya kati ipo katika hali nzuri.
Tukikamilisha bandari ya Kigoma itarahisisha usafirishaji wa mizigo kutoka kigoma kwenda Bujumbura ambao ni usawa wa umbali wa kilometer 200 na Mizigo kuelekea Congo sababu tutaisafirisha kwa njia ya reli ya kati hadi bandarini na kuelekea Congo.
SGR inaunganisha Dar na Isaka pia Ujenzi unaendelea kutoka Isaka kwenda Mwanza kuna nafasi kubwa mizigo itakayosafirishwa kwenda Uganda, Rwanda, Burundi na Congo ikasafirishwa hadi Isaka na kusafirishwa kiurahisi kuelekea katika destined country jambo litakaloondoa misongamano na mlundikano wa makasha katika bandari ya Dar.