Tumepoteana. Tujirekebishe

Tumepoteana. Tujirekebishe

a4apple

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
927
Reaction score
1,143
Ari kubwa ya makundi mbalimbali kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za udiwani na ubunge zimesababishwa na mambo kadhaa yakiwa ni pamoja na

1. Mabadiliko ya katiba ya CCM (2017) inayowapunguza wajumbe wa kura za maoni kutoka wanachama wote wa kata au jimbo hadi wanachama wachache ambao wengi wao ni viongozi wa CCM kutoka matawini na katika kata
Mabadiliko haya yamewaaminisha watia nia wengi kuwa hakutakuwa na gharama za kuzunguka kila kata na kila tawi.

Bahati mbaya kwa upande wa wenye pesa, walifurahia mfumo huu kwani wanaweza kumudu kuwapa rushwa wajumbe wote. Kwa majimbo yenye wastani wa wajumbe 1000, mgombea alihitaji angalau milioni 10 kugawa angalau 10,000 kwa kila mgombea na kujihakikishia ushindi. Hivyo wagombea hawa walihakikisha wanapata majina yote ya wajumbe pamoja na namba zao zinazopokea mihamala ya pesa.

2. Miongozo na matamko mbalimbali ya kudhibiti na kupambana na rushwa ndani ya chama katika uchaguzi huu
Hili ndo lilikuwa kivutio kikubwa kwa vijana, wasomi, watumishi wa umma na binafsi, wasanii, na makundi mbalimbali ya watu wenye dhamira ya kuongoza lakini hawana uwezo au hawako tayari kutoa rushwa. Hili ni kundi kubwa na ndilo kundi lilosheheni viongozi wazalendo.

Lakini tofauti na matarajio yao, kundi hili limepatwa na mshangao! Kumbe mambo yenyewe ndani ya chama ndo yalivyo. Wengi wao walikuwa ni makada na wanachama wa kawaida. Mshangao huu umeshusha hamasa na upendo kwa chama na wengine wamediriki kusema viongozi vijana na wasomi wana nafasi nzuri ya kulelewa kiuongozi ndani ya vyama vya upinzani kuliko chama hiki.

Mshangao huu unatoa tafsiri ya kauli kuwa CCM ina wenyewe, na wenyewe ni hao washindi walioweza kuwateka wajumbe kwa rushwa. Ina tafsiri kuwa ni kikundi kidogo tu ndani ya chama ndicho kinahitajika katika mzunguko wa uongozi. Mshangao huu ni hatari sana kwa chama.

Mshangao mkubwa walionao viongozi was upinzani waliounga mkono juhudi za JPM unafanya tafakuri ziwe nyingi. Rushwa ni adui wa haki. Bahati mbaya sana wajumbe wanafahamu kuwa hawana mishahara hivyo ujira wao hupata kipindi cha chaguzi ndani ya chama. Hii ni mbaya sana. Kwa mitizamo hii ya wajumbe tusitarajie hata siku moja nchi hii itakuja kupata viongozi bora.

Tanzania ina hazina kubwa ya viongozi wenye maono, bahati mbaya hawapati nafasi ya kupenya kwenye mifumo hii iliyojaa rushwa.

3. Kauli kwamba anaweza kuteuliwa mgombea mwenye kura chache

Hili ni eneo lingine lililovutia makundi mbalimbali kugombea. Ni kweli, CCM iliteua baadhi ya wagombea waliopata kura chache na kuwaacha wagombea waliopata kura nyingi kwa kutumia rushwa katika uchaguzi ndogo. Lakini ukistaajabu ya Musa, baadhi ya hao wanaotolewa mifano uchaguzi huu wanalalamikiwa kushinda kwa kugawa rushwa. Sijui kuna kitu gani ndani ya hiki chama.

Hivyo, kwa ahadi hizi za kuteua yeyote na kukata yeyote ziliwavutia wanasiasa wasio na pesa; wasomi, vijana, watumishi wa umma nk kugombea nafasi hizi. Sasa tunasubiri tuone je, kulikuwa na dhamira kweli ya kupambana na watoa rushwa?

4. Kuvutiwa na utendaji kazi wa JPM

Makundi mengi yalivutiwa na utendaji kazi wa rais. Huku wakifuatilia historia yake iliyojaa uadilifu katika kazi, na aliyetoka katika familia ya mkulima. Watia nia wengi walidhamiria kumsaidia rais katika mapambano yake ya kuujenga uchumi wa nchi.

Bahati mbaya makundi haya hayakujua mlango wa kuingilia katika uongozi wa chama katika kata, wilaya na mkoa ni mfinyu kama tundu la sindano kwa maskini na mpana sana kwa wenye pesa. Hivyo, wasubiri waone huo usimamizi wa maadili unaoimbwa kila uchao na Polepole, Bashiru, na Magufuli. Je, ni kweli kulikuwa na dhamira ya dhati ya kupambana utovu wa maadili ndani ya chama?

Nina mambo mengi ya kuandika, naomba niishie hapa kwa leo. Ombi langu kwa chama, turekebishe hizi kasoro mapema kabla hatujaingia kwenye uchaguzi mkuu ili kukipa afya chama chetu.
 
Huo mfumo mpya wa ccm umewekwa sio kwa ajili ya kujenga uadilifu ndani ya chama, bali ni kwa ajili ya kumpa mwenyekiti na genge lake nguvu ya kumpitisha wamtakaye. Kama kweli hiyo kamati ya mchujo ingekuwa inajali uadilifu, wale wabunge na madiwani walionunuliwa toka upinzani, wasingepitishwa kibabe kwenye hizo kamati bila kushindanishwa.

Kibaya zaidi hao waliopitishwa na chama kihuni, wakati wa uchaguzi wa marudio kulifanyika uhuni, ukatili na uhayawani wa wazi ili wao ndio watangazwe washindi. Ujinga wa wazi huko ccm, kipimo cha uadilifu ni kukubalika na mwenyekiti na genge lake!
 
Bila kupinduliwa meza hakuna wagombea wenye uadilifu ccm
 
Back
Top Bottom