Tetty
JF-Expert Member
- Jan 6, 2012
- 26,355
- 21,422
Una maanisha nini?
Elimu ipi ni bora kwako? "colonial education?" Muda mfupi baada ya Tanganyika kupata uhuru wake Elimu yetu (watanganyika)ilikuwaje?
Una maanisha hawa wasomi waliopo leo ni mburula tu?
Tumekuwa mashabiki hatufikirii tena.
Ni bora Elimu ya Kikoloni watanganyika walifikiri kwa kutumia akili zao kuliko elimu ya sasa tunafikiria kwa kutumia makalio yetu.Hatuna uzalendo tena.Utaifa ulishafariki na tuliuzika makaburi ya Kinondoni siku nyingi.Watanzania tunafurahia kundi fulani likinyanyaswa na watawala sababu tu watawala wale ni jama,marafiki,baba,mama au ndugu wakaribu.
Tumekuwa na akili ambazo watoto au wajukuu zetu watafukua makaburi yetu kuona kama vichwa vyetu vilikuwa na ubongo au maji.
JF enzi hizo lilikuwa jukwaa ambalo unatamani kila siku usome ajenda zake na hoja zitolewazo na members wake,lakini leo ni matusi ya ajabu,mipasho isiyo na maana,udini,uvyama,ukabila ndivyo vilivyojazana.Kwa ukweli JF imeshuka thamani inabidi MODS wajiangalie upya wapi wameanguka na sababu gani ili walirudishe jukwaa lile la enzi zile.