Tumekubali kuwa wanyonge

Tumekubali kuwa wanyonge

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,735
Reaction score
4,933
NI KWA SABABU WAALIMU TUMEKUBALI KUWA WANYONGE.
Imezoeleka kuwa kila panapotukia jambo linalokiuka miiko na kudhalilisha utu tunaibuka na maneno mengi mno lakini yanabeba neno "tunalaani "
Leo sijisikii kabisa kutumia neno hilo la kulaani kwa kuwa sasa limezoeleka sana na uonevu unaotokana na aina ya "ulevi mbaya kuliko ulevi wowote ule Duniani alioutaja Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kuupa jina ULEVI WA MADARAKA ".
Leo Waalimu wanacharazwa bakora kisa hawajafaulisha Darasa la saba vizuri,Kiongozi mwingine aliwahi kusema UALIMU NI FANI YA WATU WALIOFELI akasahau kuwa na Yeye alifundishwa na Waalimu haohao anaowaita waliofeli kwa ulevi wa Madaraka aliyodhaminiwa kwa muda tu.
Si hayo tu kuna Mwalimu alipigwa Kofi na Afisa Elimu haujapita mwaka tumesikia kuna Mwalimu aliyepigishwa deki na Mkurugenzi.
Haya ni baadhi tu ya masuala yanayotia FEDHEHA kwa Waalimu yapo mengi mno na yanazidi kukua kutokana na namna Mwalimu anavyoandaliwa na kufundishwa kuwa mnyonge na kibaya siyo kuandaliwa au kufundishwa ila ni KUKUBALI KUWA MNYONGE.
Kuna Kiongozi mmoja niliwahi kujadiliana naye akaniambia "MWALIMU ANAANDALIWA KAMA KICHWA CHA MWENDAWAZIMU AMBACHO KILA MWENYE WEMBE,KIPANDE CHA CHUPA ,KISU,PANGA ANAWEZA AKAJARIBU KUMNYOA AKIJISIKIA KUFANYA HIVYO"
Kibaya zaidi siyo kuandaliwa kuwa hivyo ila nimekitaja hapo juu kibaya ni kwamba Waalimu tumefikia hatua ya "KUKUBALI SISI NI WANYONGE".
Kitendo cha kukubali hali hiyo ya unyonge kwa namna ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja kumetoa fursa kwa Viongozi walevi wa madaraka kutumia rungu la uongozi kumkandamiza Mwalimu.
Ieleweke hakuna Kuongozi atakayekuja kumkwamua Mwalimu wa Kitanzania kutoka katika hali ya unyonge kama Mwalimu mmmoja mmojammoja kwa upekee wake hajaamua kuamka kutoka katika hali ya kuukubali unyonge na kutambua anaowajibu wa kuutetea ualimu wake kwa maslahi yake,ya Taifa lake,ya Jamii inayomzunguka,Ya taaluma ya Ualimu na ya Wateja wake(anaowafundisha).
Ualimu ni zaidi ya kufundisha Darasani na kwa mawanda hayo mapana ya Ualimu Mwalimu anapaswa kuwa MTU wa kuacha alama itakayowahamasisha wengine kupenda kujifunza kupitia Yeye.
Nieleweke kuwa Waalimu siyo malaika hawakosei au wanaonewa tu na wanapaswa kutetewa la hasha!..Inafahamika binadamu tuna udhaifu wa kimaadili"moral weakness"Hall ambayo karibu kila mmoja wetu anayo.Ninachotaka kukijengea msingi hapa ni suala la kutambua kuwa tunao wajibu katika mengi yanayotusibu na maranyingi Sisi ni sababu ya hali hizo kutokana na Kuzikubali.
 
Tatizo hakuna chombo cha kusimamia walimu kwan CWT ni sehemu ya utawala wa nchi.
 
I wish Mods waedit hii thread ianze na neno WALIMU
 
CWT hawana shida ,Shida ni sisi waalimu tulivyo kubali kuwa.
Hakuna atakayetikomboa kama hatutakubali kubadilika kwanza.
 
Hata mimi nimesikitika sana kitendo cha mwalimu kupigishwa deki.. kama adhabu za kiutumishi pale mtumishi wa umma anapokiuka maadili au ametenda kosa zipo kwa mujibu wa kanuni hili ni jambo baya sana kutokea.. yule mwalimu amepewa majukumu makubwa ya kuwalea vijana wetu sasa kupewa adhabu ambayo inadhalilisha utu wake na hasa inakiuka hata kanuni za utumishoi wa uuma ni pigo kubwa sana kwake..

Binafsi namfahamu huyo mwalimu kwa ni class mate wangu tulipokuwa Sekondari A-level, nimeumia sijafurahishwa na hicho kitendo huyo mkurugenzi anatakiwa aondolewe au avuliwe madaraka aende akatumikie cheo chake, kwasababu hana maadili ya uongozi pia ni mlevi wa madaraka kama mtoa uzi alivyosema.. japokuwa nimesikia mamlaka yake ya uteuzi inasema itachua hatua wanaendelea kuchunguza jambo hili.. unachunguza nini wakati jambo limetokea na limemjeruhi mtu..
 
Back
Top Bottom