Tumekosea wapi? Njooni tusaidiane wanaJF

Tumekosea wapi? Njooni tusaidiane wanaJF

mgonjwa

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2013
Posts
514
Reaction score
223
*UKWELI KUHUSU TANZANIA*

1.Tz ilipata uhuru mwaka 1961 ina miaka 54 tangu ipate uhuru ikiwa ni ya kwanza Afrika Mashariki.

2.Tz Kwa miaka 38 imeongozwa na CCM peke yake ambayo ni zao la TANU na ASP.

3.Tz ni nchi ambayo haijawahi kupata majanga makubwa kama matetemeko ya ardhi, magonjwa
ya mlipuko kama ebola, mafuriko na vimbunga au ukame.

4.Tz ni nchi ambayo imekuwa na kitu ambacho nchi za Afrika zimekikosa. Kitu hicho ni AMANI. Kwa miaka yote 54 ya uhuru haijawahi kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe.

5.Tz ina ukubwa wa 945,000 km za mraba yani sawa na uchukuwe Denmark, France, United Kingdom, Netherland, Ireland ujumlishe zote kwa pamoja.

6.Tz ina eneo la bahari lenye ukubwa wa 1,424 km. Bahari inaleta fursa za usafirishaji, uvuvi, utalii na nyinginezo.

7.Tz ni nchi ambayo imepakana na nchi za (Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi, D. R. Congo) ambazo zinategemea bahari yetu kwa usafirishaji wa mizigo na ni fursa nzuri ya kuzipelekea bidhaa za viwanda vyetu.

8. Tz ina maziwa makubwa manne na mengine madogo mengi.
Maziwa matatu makubwa yako kwenye kumi bora za ukubwa duniani na Maziwa makubwa matatu yote yapo Tanzania. Ziwa Victoria ni la tatu kwa ukubwa duniani (la kwanza Afrika) na ziwa
Tanganyika ni la sita kwa ukubwa (la pili Afrika) na la kwanza kwa kuwa na kina kirefu duniani. Ziwa Nyasa ni la tisa kwa ukubwa duniani (ni la tatu Afrika).

9.Tz ina mito mikubwa kumi ambayo ni mto Kagera, mto Ruvuma, mto Rufiji, mto Wami, mto Malagarasi, mto Mara, mto Pangani, mto Ruaha, mto Gombe, mto Mweupe wa Nile na ina mito midogo mengi kama mto Kilombero, mto Mbemkuru n.k

10.Tz ndiyo nchi ya kwanza Afrika kuwa na maji mengi yasio na chumvi yaliyokuwa kwenye uso wa dunia (fresh surface water) kutokana na kuwa
na mito na maziwa mengi na kupitiwa na bonde la ufa.

11.Tz ni nchi ya nne kwa uzalishaji dhahabu Afrika baada ya Afrika Kusini, Ghana na Mali na ipo TOP 20 duniani. Kuna migodi nane inayochimbwa dhahabu na miwili imefungwa. Migodi inayochimbwa ni Buzwagi gold mine- (Shinyanga), Geita gold mine-(Geita), Golden pride gold mine-Nzega (Tabora), Bulyanhulu gold mine- (Shinyanga). New leuka Gold mine- (Mbeya),
Tulawaka gold mine-(Kagera), North mara gold mine-(Mara). Iliyofungwa ni Korandoto gold mine (Shinyanga), Senkenke gold mine-(Shinyanga???).

12.Tz ina madini ya almasi yanayopatikana Mwadui Shinyanga. Mgodi huo ulianza kuchimbwa tangu mwaku 1940. Mpaka leo bado unachimbwa, unamilikiwa na kampuni ya Waingereza.

13.Tz ni nchi ya kwanza na ni nchi pekee inayozalisha madini ya tanzanite duniani. Mkufu wa kuvaa shingoni unatengenezwa na tanzanite na almasi unauzwa hadi shilingi milioni 25 za Kitanzania.

14.Tz ina madini ya chuma yanayopatikana Mchuchuma, Ludewa- Njombe mgodi unamilikiwa na Wachina. Mgodi huo una hifadhi ya madini ya chuma tani milioni 122 ambayo yanawezwa kuchimbwa kwa zaidi ya miaka 100.

15.Tz ina madini ya makaa ya mawe (Coal) yanayochimbwa Kiwira Mbeya, Mchuchuma na
Liganga Njombe. Unamilikiwa na Wachina. Pia mgodi wa Ngaka kule Mbinga-Ruvuma unamilikiwa na
kampuni ya Tancoal ya Australia. Hifadhi ya madini ya makaa ya mawe iliyopo ni tani bilioni 2. Makaa ya mawe ndio chanzo cha pili cha umeme wa bei nafuu duniani baada ya maji.

16.Tz ina hifadhi ya madini ya Uranium kule Dodoma (Bahi) na ni mgodi ambao unamilikiwa na
Warusi. Pia madini haya yanapatikana Namtumbo (Mkuju), Galapo, Minjingu, Mbulu, Simanjiro, Lake Natron, Manyoni, Songea, Tunduru, Madaba and Nachingwea.

17.Tz ni moja ya nchi tatu Afrika zikiwemo Zimbabwe na Madagascar kwa kuwa na madini mengi ya graphite. Madini haya yapo Tanga, Mahenge-Morogoro, Mererani- Manyara. Madini ya graphite ndiyo yanayotumika
kutengenezea betri za simu, kwenye injini na brake za magari na kwenye karamu za risasi (pencili).

18.Tz ina madini ya nickel yanayopatikana kule Kabanga Kagera, milima ya Uluguru-Morogoro, North Mara, Ngasoma-Mwanza.

19.Tz ni nchi ya tatu duniani kwa kuwa na hifadhi kubwa ya magadi soda duniani baada ya Marekani na Uturuki. Magadi soda hutumika kutengeneza vioo vya aina zote. Vioo vya nyumbani hadi magari pia kutengeneza sabuni na dawa mbalimbali za usafi.

20.Tz ina hifadhi na mgodi wa madini ya niobium uliopo Panda hill Mbeya ambao ndio utakuwa mgodi mkubwa wa kwanza Afrika na wa nne duniani. Mgodi huu unamilikiwa na kampuni ya Australia. Madini ya niobium ni magumu sana
hutumika kutengeneza mabomba pamoja na madini chuma pia hutumika kutengeneza baadhi ya sehemu za injini za ndege na vyombo vinavyoenda nje ya uso wa dunia (mfano Apollo 15 CSM), vioo vya computer na lenzi za camera.

21.Tz ni nchi ya kwanza Afrika na ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii. Ya
kwanza ni Brazil. Nchi zilizokuwa kwenye tano bora kwa utalii Afrika ni Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, Kenya na Zambia.

22.Tz ina mbuga zipatazo 16 na ile mbuga maarufu kuliko zote duniani Serengeti ipo Tanzania, mbuga iliyopakana na bahari iitwayo Saadani ipo Tanzania na mlima mrefu kuliko wote Africa Kilimanjaro upo Tanzania.

24. Tz ina ardhi kubwa yenye rutuba na inayofaa kwa kilimo cha mazao mengi tofauti tofauti. Mashamba makubwa ya mpunga kwa mfano yaliyokuwa chini ya Shirika la NAFCO yalitoa mazao ya kulisha Tanzania na pia nchi nyingine.

24.Tz ina gesi ya asili ya Carbon Dioxide (CO2) inayovunwa kule Kyejo, Rungwe-Mbeya na kampuni ya TOL. Gesi ya asili ya cardon dioxide inatumika sana kutengenezea vinywaji laini kama soda, bia na pia kutengenezea madawa, makaratasi na kutibia maji (water treatment).

25.Tz ina gesi ya asili inayopatikana katika kisiwa cha Songo songo mkoa wa Lindi. Gesi hii imekuwa ikichimbwa na kusafirishwa hadi Dar es salaam tangu mwaka 2004. Inamilikiwa na kampuni ya Songas ya Uingereza.

26.Tz imengundua gesi ya asili yenye zaidi ya meta za ujazo trilioni 55.3 iliyongunguliwa katika maeneo ya bahari ya Hindi na Mtwara.

Pamoja na sifa zote hizi lakini Tz ni nchi iliyo kwenye kundi la nchi maskini duniani ambayo asilimia kubwa ya raia wake wanaishi chini ya Dola moja za Marekani na hali ya huduma za kijamii ikiwa duni.

TUJIULIZE, TATIZO LIKO WAPI??
 
Maono ya watanzania siyo endelevu kabisa.Tunaishi maisha ya kuiga iga tu yasiyokuwa na tija.Watu wenye upeo mkubwa wa uongozi kutufikisha kunakostahili hawana mwanya huo kwa sababu ya mfumo mbaya wa kuwapata na hata kuwandaa viongozi wa kuliongoza Taifa.Mathalani chukulia uchaguzi Mkuu uliopita 2015.Jinsi gani tulivyompata kiongozi aliyeko madarakani.Ni kwa bahati nasibu tu! Hakukuwa na maandalizi au matayarisho ya mtu mwenye kubeba maono ya kitaifa(Tena nayo kwa bahati mbaya hayapo).Ni kama vile tulikurupushwa usingizini ghafla tu Dr.JPM huyu hapa.Mwenyewe wala hakujiandaa kuwa kiongozi wa Nchi.Tena kwa maneno yake alisema alichukua fomu kujaribu kugombea.Sasa huyo ndiye kiongozi tuliye naye.Kwa hiyo Mifumo mibovu wa kuwapata Viongozi wakuu bado ni kitendawili ambacho kinahitaji kuteguliwa.Na siyo siri hapo Katiba inahusika kikamilifu.

Pili, Ili tuwe na muelekeo mzuri wa kimaendeleo sera zetu za matumizi ya rasilimali zetu zisibaki kutungwa na wachache bali ziwe shirikishi na za muda mrefu.Matamko ya kisiasa yasiwe sera .

Viongozi wenye maono huandaliwa ili kusimamia yale yaliyoko kwenye katiba ,dira na mwelekeo wa Taifa.Tutabaki kusema tumelaaniwa ilihali rasilimali tunazo za kutosha,Pia nguvu kazi ipo isiyotumika vizuri.Mchawi wetu yu hai bado kama hatutabadili fikra zetu kuwa na mtizamo chanya wenye kuhitaji mabadiliko ya dhati, Akifa mchawi wetu tutahangaika miaka mingi vizazi na vizazi maendeleo kwetu ni ndoto za mchana kweupee!
 
Mfumo wetu wa mikoa hauwezi kutuletea maendeleo. Tunatakiwa kuwa na mfumo wa majimbo. Hili ni jambo naona Mbowe aliona mbali sana sema watanzania kwa sababu ya ujinga walishindwa kumuelewa.
 
tulipokukosea ni ukosefu wa elimu....nchi hii suala la elimu linapewa kipaumbelae cha maneno tu lakini kivitendo no.

mfano ni mtu mwenye gari lakini hana maarifa/elimu ya udereva mtu huyo anaweza kutembea kwa muguu haliyakuwa ana gari wakati huo huo kunamadereva ambao hawana magari lakini hapati shida ya usafiri anaendesha magari mazuri na bado analipwa mshahara na malupulupu mengine na sometimes na uchakachuzi juu.
hapo utaona kinacho msaidia huyu dereva ni elimu ya udereva.

kwa bahati mbaya sana madhara ya kutoipa kipaumbele elimu hayaonekani ghafla huonekana baada ya miaka mingi baadae,hivyo basi hichi ulichokiona mtoa mada ni madhara ya kukosa elimu.

elimu ya bongo imeegemea watu kufaulu na kupata vyeti tu na sio ujuzi kwa hali hii utampata mtu mbunifu wa kutumia vizuri rasilimali.

walimu wengi ni failures wa kidato cha nne,walimu wanafanya kazi katika mazingira magumu,shule hazina miundombinu ya kutosha nk hvyo ufundishaji na ujifunzaji unakuwa mgumu.

unataka mwalimu aliyopo kwenye mazingira kama hayo afundishe kwa moyo wakati mshahara kiduchu,haki zake za msingi kama incriminate na madaraja unampiga pending muda mrefu!

kuna mambo mengi sana yanayo ashiria elimu yetu inashida nawezangu mnaweza mkaongezea.
 
Back
Top Bottom