Tumekosa ustaarabu katika kusitiri miili ya wenzetu

Nyie mnaolalamika mara oooh sijui wamefunikwa na majani, sijui kiatu kimoja ndio wale mkifika msibani mkipewa msosi mnaulizia kijiko au kachumbari!! Hivi vifo vya wapendwa wetu vimetokea katika hali ya ajali tena mbali na mjini au huduma muhimu.
Waliojitolea kutoa maiti na hata first aid ni wasamaria wema tu sio madaktari. Tena hawakua wamejipanga kua watafute machela au magari.
Kistaarabu na kibinadamu maiti hufunikwa na tulioona hizi picha ni mashahidi kua baadhi walifunikwa na kanga /vitenge kama hazikutosha wewe ulikua unashauri wafunikwe na nini????? Majani haipendezi lakini ndicho kilichofaa kwa muda ule... kuna maiti hua hazipati hata hayo majani zinaachwa wazi unakuta zimejaa nzi, je ulitaka iwe hivyo????
Unafahamu hali ya nchi yetu, mazingira na uchumi in such an emergency hakuna ndege au special cars walifanya walichoweza coz wangewaacha pia mngelaumu.
Tujifunze kushukuru hata kwa madogo tunayofanyiwa esp mtu anapojitolea.
 
Mimi nafikiri wakati umefika wa mamlaka husika kupiga marufuku picha za ajali, majeruhi na wafu na kuziweka mitandaoni. Kuwe na adhabu kali kwa wote watakaokiuka hili. Tuwatendee haki majeruhi na wafu.
Tena me nasema hiviii....'tujitendee haki sisi marehemu na majeruhi', maana sisi sote ni marehemu na majeruhi watarajiwa!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Naomba nikupinge mleta uzi.
Ile ajali imetokea bila kupangwa na eneo ilipotokea ni mbali na makazi ya watu hata ukifuatilia kwa karibu utagundua waliohusika kuchomoa miili kutoka kwenye gari ni wasafiri waliokuta tukio limetokea hivyo hawakuwa na hizo nguo za kufunika miili ile.
Pili ni akili gani itakujia ya haraka kuusitiri mwili ingali kuna miili mingine inahitaji kuokolewa?
Binafsi nimewahi kushuhudia ajali na niliona jinsi gani watu hurukwa na ufahamu wanapookoa miili ya marehemu au majeruhi.
Kosa sio kusitiri bali ni kupiga picha za wafu/majeraha makubwa na kusambaza mitandaoni bila ruksa ya mamlaka husika.
Absolutely, umeongea kwa hekima mkuu. Kosa sio jinsi ya kusitiri marehemu( ukizingatia ile ni ajali na imetokea porini), kosa ni kupiga picha ovyo na kuzirusha mitandaoni.

Hili la kurusha picha ovyo naomba liangaliwe kwa jicho la tatu, it's too much.
 
tusilaumu sana hebu tujiulize pale porini wanaotoa msaada kabla ya taarifa wasamalia wema wasio na taaluma yoyote ya uokoaji mtu amefariki nguo zimevuka anamsitiri vp si atatumia mbinu yoyote hata tu hayo majani hadi wataalamu watakapofika .mbona baadae shuka za msd zilifika pale sematu ubebaji kwenye gari wa marehemu ndo ulikua mbaya ila kusema mtu anaokoa atafute kiatu kingine cha marehemu kiko wapi hali kuna watu bado wanatakiwa kutolewa daah all in all R.I.P Watoto wetu
 
Mazingira Yale yalikuwa ni emergence ya uokoaji
Unategemea khnga Na shuka zingetoka wapi porini pale?
Najua ndg yangu maana ht mm nilishawahi kupata ajali,kutokana na eneo lenyewe nilifika hosp bila nguo.
Mm ishu yangu ilikuwa kwenye kuwalundika kwenye gari km mizigo.
 
Hata ktk mitandao ya jamii watu kutuma pics hizo kila mara sidhani km ni ustaarabu mzuri, na kuwatendea haki hawa malaika pamoja na wazazi, ndg na jamaa !!

Wengine ni waandishi wazoefu kabisa kama akina Michuzi ila wanapost picha za maiti za watoto hadi unashindwa kuelewa tatizo ni nini hasa?
 
Nimeona wazazi wakisikitika na kuomba picha hizo zifutwe mitandaoni zinawaumiza wakiziona
 
Mimi nafikiri wakati umefika wa mamlaka husika kupiga marufuku picha za ajali, majeruhi na wafu na kuziweka mitandaoni. Kuwe na adhabu kali kwa wote watakaokiuka hili. Tuwatendee haki majeruhi na wafu.
Indeed!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kumbukeni pale ni porini sijui nguo au shuka zingetoka wapi za kuwafunika kwa hataka lakini nilichoona baadae magari ya hospital yalipofika walifunikwa na shuka za msd, watu wanahangaika kuwaondoa kuvua soksi na viatu siyo jambo la dharura wangevuliwa tu, pia kubeba maiti kwenye ambulance ni jambo la kawaida kwenye uwingi mkubwa hivyo wa maiti hata kwenye lori ili mradi kuwawahisha kuhifadhiwa ili wasiharibike
 
Ni kweli ambulance haibebi maiti ulishaingia ndani ya ambulance ukaone ilivyo? Pickup ndio huwa zinabeba maiti fuatalia mahospitalini watakupa jibu tunaelimishana wakuu siyo ugomvi
 
Unajua wote tunaumia hasa wazaz ambao tuna watoto.. Kuna mazingira ambayo hata ufanye nini huwez kuzuia hali halisi,,,tunalalamika sababu aidha kujua au kutokujua,,, porin gar imepata ajali kwamba wangewasitiri na nini?? Wingi wa waliokufa unapata wap shuka au kanga za kuwastiri wote na kuna wengine wapo hai wanaohitaji kuwahishwa hospitali? Mazingira gan ajali imetokea mpka tuone kwamba tumewakosea heshima?heshima ni ipi kuwaacha waz au kuwafunika na majani? Hiv meshakumbana na ajali ukaona kinavyotokea ukiwa na akili timamu?? Mnasema gar wamerundikwa je wangewaweka vip ktk gar maiti zote hata kama zingepakiwa kumi kumi? Kwa hyo wakiwaweka sehem moja ili kuwapeleka mochwari kuna kosa lipi?

Tupo tofauti sana kimtazamo kwa yyte ambae anaheshimu maiti kuliko mtu hai simuhukumu

Na yyte anaeheshimu mtu hai kuliko maiti namweshimu vile vile maana hakuna msaada unaoweza kumpa maiti... So tuheshimu wote waliofanya juhudi za kuwatoa ktk korongo wote waliokufa.. Mungu uwapumzishe kwa aman viumbe hawa sio kama tutakavyo sisi bali utakavyo wewe maana wewe unajua kila kitu.
 
Amina
 
Ndugu wanaJF,

Katika ajali iliyotokea juzi Arusha,kila mtu atakubaliana nami kwamba utaratibu mzima uliotumika katika kuwasitiri wenzetu haukuwa mzuri na sahihi.Jana katika kipindi maalumu cha Clouds TV,mmoja wa wazazi pia alilalamikia hili.Maiti za watoto zilizivyotolewa kwenye korongo,wengine wana kiatu kimoja,wengine wana soksi moja mguuni na wengine nguo zao zimevuka kabisa.

Mbaya zaidi hata uondoshaji maiti eneo la tukio mpaka mortuary,kwa kutumia pick up na miili ya watoto imepandana hapakuwa na ustaarabu hata kidogo.Niombe tu mamlaka husika ijue kwamba,machungu ya mzazi yanaongezeka sana hasa baada ya kuona mwili wa mwanae ukiwa katika state ya namna hiii.

Mtoto wa mwenzio ni mwanao.
 
Nakubaliana na wewe asilimia zote.. Watanzania wengi wana moyo wa kusaidia wakati wa ajali. Lakini wengi hawajui nini cha kufanya wakati huo.

ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU

Umma upewe elimu inayohusiana na ajali na uokozi..
Picha nyingi zinapigwa na kusambazwa bila hata tahadhari wala kusitiri sehemu zisizostahili kuonekana.. Wengine wamefunikwa majani daah!

TCRA... Mamlaka husika where are you?? Ondosheni hizo picha kwenye mitandao ya kijamii
N kwel kabisa hizo picha zinatuongezea machungu n bora zikatolewa kabisa kwenye mitandao
 
Wakati mwingine inalazimu kulingana na mazingira. But huo ni mwili tu roho ilishaenda mahali salama. R.I.P. ANGELES
 
Back
Top Bottom